05/06/2026
π¨ UPDATE: Golikipa wa Klabu ya Simba SC, Yakoub Suleiman, amefanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuendelea kusumbuliwa na jeraha alilolipata wakati wa AFCON 2025 nchini Morocco π²π¦.
Upasuaji huo umefanyika Ijumaa, Mei 22, 2026, katika Hospitali ya Ebrahim Haji, Dar es Salaam.
Yakoub alikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano bila kupata nafuu kabla ya hatua hiyo ya matibabu kufanyika.
Kwa sasa, atakosa michezo yote iliyosalia ya msimu huu, na pia sehemu ya mwanzo wa msimu ujao kutokana na kipindi cha kupona.
05/06/2026
MZEE MAGOMA KAPIGA KWENYE MSHONO πΈ
"Kwenye mazuri Simba tuwasifie ili na wewe upate nguvu za kununua la kwako, Simba wana Iriza Yanga ndio wana Bus tena aina ya TATA sasa utakaa na Tata mpaka lini?
"Hoja ya kusema Iriza ya Simba ni Used wewe unalo? Mimi naona waende na hoja ya kuhoji kwanini kiwanja hakijengwi mapaka sasa na sio Iriza ya Simba, Yanga wana Bus ila Simba ana Iriza tuwapongeze" Mzee Magoma
04/06/2026
π¨πΏπ¦ ππππππππ: Kaizer Chiefs imefanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa kumsajili Neo "Gift" Maema, duru zinaonyesha.
Maema kwa sasa yuko kwa mkopo wa mwaka mmoja Simba SC akitokea Mamelodi Sundowns na anatarajiwa kuwa mchezaji huru mara tu baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo.
kwa hali ilivyo, Simba SC bado haijatoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na mustakabali wa Maema klabuni hapo
Hali ya mchezaji huyo inafahamika inategemea kwa kiasi kikubwa mipango ya kocha mkuu Barker ambaye anatarajiwa kutathmini kikosi chake kabla ya hatua yoyote ya uhakika kufanywa.
Vyanzo vya habari zaidi vinasema kuwa Kaizer Chiefs tayari wameanzisha mawasiliano ya awali na wawakilishi wa Maema ili kuchunguza masharti ya mkataba unaowezekana.
Hata hivyo, hakuna makubaliano yaliyofikiwa na kwa sasa hakuna mazungumzo ya juu kati ya pande zote
Mustakabali wa neo Maema bado upo wazi, huku Afrika Kusini na Tanzania zikiendelea kufuatilia hatua inayofuata katika taaluma yake
04/06/2026
Nani amependeza kuliko wenzie hapoπ€£π€£π€£?
04/06/2026
GONGOWAZI WAMEUMIA VIBAYA MNOOOO MAMAEEE
02/06/2026
Siku Ile Yanga Wana tangaza kuanza ujenzi wa uwanja wengi tulipongeza Kwa hatua Ile, na wengi tulipongeza Kwa sababu ya kuhakikishiwa kuwa uwanja unaanza ujenzi kesho yake, tuliona ni kitu chenye uhakika ndiyo sababu tulimpost sana Raisi wa Yanga kumpongeza alionekana ni mtu anaye leta mapinduzi makubwa ya kimpira hapa nchini.
Leo Mwekezaji wa Simba kaachia picha ya basi alilo waahidi Simba, kitu Cha kushangaza Alikamwe akachukua picha hizo na kuandika kuwa "kumbe basi lenyewe Used"
Simba Wana hitaji pongezi Kwa kupata basi hili la Kifahari haijarishi ni used au vipi, ni Bora basi lao lina onekana na siyo la kwenye Laptop.
31/05/2026
π πππππ ππππππ πππ πππππππππ! πΉπΏ
Simba Queens have been crowned the 2025/26 Tanzanian Womenβs Premier League champions.
Hongera kwao. π
30/05/2026
Mustakabali wa Fiston Mayele bado haujaamuliwa.
Wawakilishi wa mshambuliaji huyo wamethibitisha kuwa kuna nia kutoka kwa Al Ahly ya kumsajili, ingawa kwa sasa klabu hiyo ya Misri inaweka kipaumbele katika kutafuta mshambuliaji mwenye umri mdogo zaidi.
Iwapo Al Ahly watashindwa kupata wachezaji waliowalenga kwanza, Mayele anaweza kuwa chaguo muhimu na la dhati kwao.
Kwa sasa, nyota huyo wa DR Congo ameweka akili yake yote kwenye Kombe la Dunia la FIFA, na uamuzi kuhusu klabu yake inayofuata unatarajiwa kufanyika baada ya mashindano hayo kukamilika.