09/05/2026
๐จBARKER AFUNGUKA COMBO YA CHAMA NA MPANZU SIMBA
Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amepongeza kiwango na muunganiko wa viungo Clatous Chama na Elie Mpanzu baada ya wawili hao kuendelea kuwa tishio katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Barker amesema uzoefu na ubunifu wa Chama umeongeza tofauti kubwa ndani ya kikosi hicho huku Mpanzu naye akiendelea kuimarika kadri msimu unavyoendelea.
โChama ana utulivu mkubwa na ubunifu wa hali ya juu. Mpanzu naye ameendelea kukua na sasa wanasaidiana vizuri kutengeneza mashambulizi hatari,โ alisema Barker.
Katika michezo ya karibuni, wawili hao wamehusika moja kwa moja kwenye mabao muhimu dhidi ya Singida Black Stars, Young Africans SC na JKT Tanzania.
fans
06/05/2026
06/05/2026
04/05/2026
02/05/2026