17/01/2025
"Kuna Sauti Ina niambia kwamba Yanga Watabakia Wanalia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Kesho, Hii ni Dalili ya MC ALGER kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Huenda Safari ikafika Tamati Kesho"
Halisi Media Sports Halisi
21/12/2024
WALLACE KARIA AONGOZE TFF HADI KIFO
Laiti ningekua na uwezo ningeweza kumbakiza Wallace karia aendelee kusimamia changamoto za soka hapa Tanzania naaamini ipo siku angezimaliza kabisa.
Katika kipindi chake amefanya makubwa kwenye soka la Tanzania hata ambae haoni basi ni kipofu, Tanzania tuko mbali kidogo japo bado juhudi zinahitajika lakini watu k**a hawa huwa hawajirudii.
hapa ushabiki ni pembeni uhalisia lazim uchukue mkondo wake, Mafanikio ya Mpira yaliyopatikana Katika utawala wake kuanzia Katika Vilabu na Timu ya Taifa kufuzu AFCON mara tatu mfululizo Hilo sio jambo Dogo Lazima apewe Maua yake, Tunatakiwa kufanya maandamano ya amani kushinikiza Wallace Karia awe Rais wa kudumu TFF Ndugu zangu aminini kwamba tutaenda kubaya baada ya Karia
Huyu baba amefanikiwa kupeleka timu mbili robo fainali klabu bingwa, katika utawala wake Yanga pia imefika Mpaka Fainali ya kombe la Shirikisho siyo jambo jepesi
Katika Msafara wa Mamba Hata kenge wapo kwahiyo Hakuna Mtu anayependwa na Watu wote Hata ufanye Nini Lazima uchukiwe na Watu
All In All k**a Kuna Uwezekano Karia aongezewe Muda Hata k**a katiba inasema Muda wake umeisha ifanyiwe marekebisho atawale Mpaka kifo
23/09/2024
JE HUYU KAKA KUCHELEWA KUPATA MAFANIKIO DHIDI YA MDOGO WAKE NI KUBWA JINGA?
"Kaka alizaliwa Mwaka 1935 Mwaka Mmoja Baadae Mdogo wake Naye Akazaliwa ikabidi kaka amuachie Ziwa Mdogo wake
Baada ya Miaka Kadhaa Mdogo wake alipata Mafanikio Zaidi hasa kwenye Anga ya Kimataifa Huku Kaka yake akisubiri Miaka zaidi ya 88 kufikia Mafanikio ya Mdogo wake kwenye Anga ya Kimataifa
Kitu Cha ajabu Baada ya kaka Kuanza Nae kung'aa Kimataifa akaanza kumzodoa Mdogo wake kuwa amechukua Muda Mchache zaidi kukaribia Mafanikio ya Mdogo wake hakumbuki yeye Ndie aliyemuachia Ziwa Mdogo wake na yeye Ndie alipaswa kuwa mstari wa mbele kumuonyesha Njia ya Mafanikio Mdogo wake!!!
Je Huyu kaka Ni Kubwa jinga? Miaka 88 alikuwa wapi muda wote kuyafikia Mafanikio ya Mdogo wake??
Bila kuwa na "D 2" Huwezi Kuelewa 😀
22/09/2024
MASHABIKI WA YANGA MNA MATATIZO GANI?
Licha ya Kuwa na Uongozi Imara Engineer Hersi Said na Arafat Haji Chini ya Udhamini wa Muwekezaji Gharib Said Mohamed (GSM) ambao Umeifanya Yanga kuwa Moja ya Timu Tishio kukutana nayo Barani Afrika lakini Bado Mashabiki wa Yanga hawaonekani Kuisapoti Timu Yao Asilimia 100% Hasa Kwenda Uwanjani
Unadhani Mashabiki wa Yanga wana matatizo Gani kwanini hawapendi kwenda Uwanjani? Uwanja Mdogo k**a New Aman Complex Mashabiki wameshindwa Kuujaza Full House
Mashabiki wa Yanga mnataka Nini 😢
10/08/2024
NIMEOTESHWA AZAM BINGWA WA NGAO YA JAMII
" Failasufi ana Jambo lake siku ya Kesho nimeoteshwa Ndie atakuwa Man of the Match kwenye Mchezo wa Kesho na Azam FC itaibuka Bingwa wa Ngao ya Jamii Kwa Ushindi wa Magoli 2-1 yote yakifungwa na Feisal salum FEITOTO "
08/08/2024
WANA SIMBA TEMBEENI KIFUA MBELE
Imagine hii ni Timu Mpya yaani performance waliyoionyesha Leo Dhidi ya Yanga SC ndio Mchezo wa kwanza wa kimashindano Katika Kikosi kipya Cha Simba SC
Good performance Katika Mchezo wa Leo kiukweli Wana Simba Mwaka huu Timu ipo.. Inahitaji muda kidogo Ili Kuweka Muunganiko ulio Bora Zaidi coz wachezaji wote waliperfom vizuri sana
Yanga Wajipange Msimu huu, Simba hii ikikaa Sawa Nahisi Kitawaka
06/08/2024
DEVORA MAVAMBO NDIE MVP MSIMU UJAO "MKUNDA"
Kwa Mujibu wa Ahmad Mkunda
" Debora Fernandez Mavambo Ndie atakuwa MVP wa Msimu Ujao wa Ligi Kuu NBC PREMIER LEAGUE 2024/2025
Nyie Hii machine ni hatari katika sajili bora msimu huu Debora Mavambo Fernandez ni sajili Bora sana ntakuja kunambia"
04/08/2024
UPANGAJI WA MATUKIO NI MBOVU "MKUNDA"
" Upangaji wa Matukio kwenye Siku ya Wananchi ni Mbovu Matukio yasiyo na Msingi ni Mengi na Muda hauzingatiwi, mechi ilipangwa Saa 2:30 Usiku Hadi muda huo Wachezaji hawajamaliza kutambulishwa, Poor kabisa" Ameandika
Unakubaliana na Ahmad Mkunda??
31/07/2024
TOP FOUR YANGU YA MSIMU UJAO 2024/2025
1. Simba SC
2. Yanga SC
3. Azam FC
4. Mashujaa FC
5. Singida BST
30/07/2024
YALE YALE YA SIMBA SC NDIO YANATOKEA KWA YANGA SC
Kipindi Cha Nyuma Waandishi wa Habari za Michezo na Mashabiki wengi wa Yanga walikuwa wakipiga kelele sana Dhidi ya MO DEWJ kuwa anatumia Jezi za Simba SC kutangaza bidhaa zake MO XTRA na nyinginezo Bila Kujua Simba SC inafaidikaje
Jezi za Yanga zimetoka tunaona Hii Boost Energy Drink Nyuma kwenye Jezi ya Yanga lakini Hatujaambiwa Mkataba umesainishwa Lini na GSM wameilipa Yanga kiasi gani Kutangaza kinywaji hichi, watu wapo kimya ???
27/07/2024
MSIMU HUU YANGA WAMEFUNIKWA NA SIMBA KWENYE JEZI
" Nimezitazama Jezi zote za Simba na Yanga zitakazotumika Msimu ujao wa 24/2025 kiukweli Bila Unafiki Simba SC wametisha sana kwenye upande wa Jersey "
" Nimechukizwa sana na Yanga Kwa sababu Wanaanza Kubadilisha Uhalisia Wao wa kijani na Njano, Yanga Ina hama Sasa hivi inageuza Rangi ya Orange kuwa Njano na pia imeongeza Rangi ya Kijivu...Pia Mbunifu wa Yanga SC ametumia Ushamba Kuweka Mkono akimaamisha Matokeo ya waliyoyapata Dhidi ya Simba SC"
"Jezi inatakiwa kuwa classic haitakiwi kuwa na Vikolombezo vingi tazama mfano kutoka Katika jezi za wenzetu huko Nje hicho tu ndio nampa maua yake Mbunifu wa Jezi za Simba SC ametisha sana"
30/06/2024
YANGA IUITE UWANJA WAO YUSUPH MANJI STADIUM
Ili kuenzi Makubwa aliyoyafanya Mfadhili na Mwenyekiti wa Zamani wa klabu ya Yanga SC Yusuph Mahboob Napendekeza Yanga Imuenzi vilivyo Tajiri Huyo alietoa Yanga shimoni Hasa kiuchumi
Nashauri Yanga Impe Heshima Kwa Kuupa Uwanja wao ambao wanataraji kuujenga pale mkabala na Makao makuu ya Klabu hiyo Jangwani Jina la YUSUPH MANJI STADIUM Ili kizazi Kijacho na wapenzi wa klabu hiyo waweze kukumbuka mchango Mkubwa Alioutoa Tajiri huyo Katika Klabu hiyo