Sokalabtz

Sokalabtz

Share

📊 Football Analysis & Insights
🔊 Fan-based content | Unofficial stats
🔁 Recaps • Player insights • Team analysis

*Independent football contents*

05/06/2026

Nani una muachia apige Faulu Dakika za jioni ili timu ishinde?

🎯 Chama: Magoli/Asisti 8 (Mwamba wa akili nyingi!)
🎯 Libasse: Magoli/Asisti 6 (Mzee wa kupiga kamba!)
🎯 Oura: Magoli/Asisti 4 (Kasi na macho juu!)
🎯 Maema: Goli/Asisti 1 (Fundi wa mipira iliyokufa!)

Hapa ukiruhusu tu faulo karibu na 18, ni sawa na kujifunga mwenyewe maana hawa jamaa hawana huruma kabisa. Je, unadhani hii ndio safu hatari zaidi ya "set-pieces" kwenye Ligi Kuu yetu kwa sasa au kuna wanaowazidi?

Angusha maoni yako hapo chini tufanye uchambuzi! 👇

Follow kwa burudani zaidi na share post hii na washkaji zako wote wa soka! ⚽🚀

05/06/2026

nani anakukosha zaidi kwenye utendaji kazi wake? 🔥👇

Mambo ni moto sana kule Yanga SC! Hawa mafundi watatu wamekichafua sana na kuhusika kwenye jumla ya MAGOLI 16 hadi sasa msimu huu:

⚽ Prince Dube: Magoli/Asisti 9 (Mashine ya mabao!)
⚽ Maxi Nzengeli: Magoli/Asisti 5 (Kasi na chenga za maudhi!)
⚽ Duke Abuya: Magoli/Asisti 2 (Mzee wa kazi chafu!)

nani anakukosha zaidi kwenye utendaji kazi wake? Acha maoni yako hapo chini! 👇

Unasubiri nini? Follow kwa uchambuzi zaidi na share post hii na Wananchi wenzako! 🎯

04/06/2026

Kwa kauli hii ya Muheshimiwa Waziri itakuwa suluhisho la kulinda vipaji vya vijana wadogo kisoka?

04/06/2026

Umemtambua Mchezaji gani kwenye hii picha?

03/06/2026

Eliud Ambokile wa Mbeya City ameshacheka na nyavu za wapinzani wake! Tayari ashafanya umafia huu kwa kutupia ⚽ Mabao 4 kwenye mechi dhidi ya Namungo, Tanzania Prisons, Dodoma Jiji, na Mtibwa Sugar.

Je, unamuona Ambokile akimaliza top scorer wa msimu huu? Shusha comment yako hapo chini! 👇

Gonga Like, Follow kwa mchongo mzima wa soka, na Share post hii kwa washkaji!

03/06/2026

Kwenye Ratiba Yao Hii Ya Mechi 5 Zilizobaki (vs JKT Tanzania, Dodoma Jiji, Tanzania Prisons, Simba, Fountain Gate), Mzunguko Wa Kwanza Walifanikiwa ✅ kupata ushindi katika Mechi 2 (Fountain Gate, Tanzania Prisons) 🤝 Walisare Mechi 1 (Dodoma Jiji) ❌ Walipoteza Mechi 2 (JKT Tanzania, Simba Sc)

Huu Mziki Sio Wa Kitoto! 💯 Tumeona Wana Uwezo Wa Kuzimaliza Timu Ngumu K**a Dodoma Jiji, Ila Wakikutana Na Simba/Yanga Mambo Yanaanza Kuwa Magumu. Wana Vipaji Vingi Sana, Swali Ni Je, Wanaweza Kubadilisha Sare Hizi Kuwa Ushindi Ili Kuchuana Na Vinara Hawa? Huu Mzunguko Wa Pili Hautakuwa Rahisi Kabisa Kwao.

Nini Maoni Yako? Je, Wanaweza Kubadilisha Sare Hizi Kuwa Ushindi Ili Kuchuana pale Top 4? Angusha Comment yako! 👇

Usisahau Kutufufatilia Na Ku-Share Post Hii Kwa Mashabiki Wengine Wa Mpira Wa Bongo! 📲

02/06/2026

Michezo 5 iliyobaki kwa Azam FC, Je watamfunga Yanga, Fountain na Mashujaa waliotoa nao sare mzunguko wa kwanza? 🔥

Kwenye mzunguko wa kwanza NBC Premier League 2025/26, "Wanalambalamba" wamevuna pointi 9 kutoka kwa hizi timu zilizobakia.

🏆 Ushindi: Dodoma Jiji na Coastal Union walifanikiwa kuondoka na alama zote 6.

🤝 Sare: Fountain Gate, Mashujaa FC, na Yanga SC walitoka suluhu na kuondoka na point 3 pekee.

Je, Azam wataweza kuondoka na point zote kwa Fountain Gate, Mashujaa FC, na Yanga SC? Angusha comment yako hapa chini! 👇

Gonga Follow na Share uchambuzi huu wa kishabiki kutoka ! 📲

02/06/2026

Huyu Jephte Kitambala kashasoma mchezo mapema! 👇

Mshambuliaji wa pale Azam FC, Jephte Kitambala, anaendeleza spidi yake. Mpaka sasa, kashatupia magoli 6 na kutoa assist 1 tayari. 🔥 Hii siyo kazi ndogo, kwani orodha ya timu alizozifanyia uharibifu ni ndefu: amewanyoa hadi miamba k**a Simba, Coastal Union, JKT Tanzania, na wengine! 🥅

Anaonyesha ana njaa ya mabao na uwezo mkubwa wa kucheza na timu. Ni wazi anaweza kuwa mshambuliaji kiongozi ndani ya kikosi cha Azam Fc. 🏃‍♂️💨

Je, katika michezo hii 5 iliyobaki ana uwezo wa kuongeza mabao mengine au amuachie hiyo kazi Feisali? 👇? Tuambie maoni yako hapa chini! 👇

FOLLOW NA USHARE POST HII KWA WADAU WENZAKO! 🤝

02/06/2026

Hivi Azam FC wanajua kweli wana dhahabu benchi au wanajifanya hawaoni? 🤔

Mwamba aliamua kuwasha moto dhidi ya timu yake ya zamani, Dodoma Jiji! Alipiga mbili peke yake, akatoa asisti moja na kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa mechi (MOTM). Yaani katili kabisa! Suala la kushangaza ni kuwa hapati nafasi ya kutosha kikosini Chamazi. Kiwango hiki kiko benchi? Huku ni kuchezea kipaji aisee!

Je, unadhani Zidane Sereri anastahili kuanza kikosi cha kwanza Azam FC mfululizo au aendelee kusubiri benchi? Shusha comment yako hapa chini!

👉 Follow kupata chambuzi tamu k**a hizi na share post hii kwa mdau wa soka!

02/06/2026

Wananchi Kuna wakumzuia Yanga sc kuondoka na point 15 hapa?

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dar Es Salaam