29/05/2026
# # Real Madrid Waongoza Orodha ya Vilabu Vyenye Thamani Kubwa Duniani
Jarida la biashara la Forbes limetoa orodha mpya ya vilabu vya soka vyenye thamani kubwa zaidi duniani, huku Real Madrid wakiongoza kwa thamani ya dola bilioni 9.5. Wapinzani wao wa jadi FC Barcelona wamefuata nafasi ya pili wakiwa na thamani ya dola bilioni 7.5.
Katika nafasi ya tatu ni Manchester United wenye thamani ya dola bilioni 7.2, wakifuatiwa na Liverpool wenye dola bilioni 6.2. Mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain wamek**ata nafasi ya tano kwa dola bilioni 5.8 huku Bayern Munich wakishika nafasi ya sita kwa dola bilioni 5.7.
Ligi Kuu England imeendelea kutawala orodha hiyo kwa kuwa na vilabu 11 ndani ya 30 bora duniani. Manchester City wameorodheshwa nafasi ya saba kwa dola bilioni 5.5, Arsenal nafasi ya nane kwa dola bilioni 5.4, huku Chelsea wakishika nafasi ya tisa kwa dola bilioni 4.2.
Orodha hiyo inafungwa kwenye Top 10 na Tottenham Hotspur wenye thamani ya dola bilioni 3.0. Ripoti hiyo inaonyesha jinsi biashara ya soka ilivyozidi kukua duniani, huku vilabu vikubwa vikiendelea kuongeza mapato kupitia udhamini, haki za matangazo, mauzo ya bidhaa pamoja na nguvu kubwa ya mashabiki duniani kote.