Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu tasnia ya mchezo wa Masumbwi Tanzania ikose kumuona ulingoni bondia mashuhuri na tishio Selemani Salum Kidunda maarufu k**a โJini Makata".
Kidunda alizaliwa Januari 2, 1984 katika Hospitali ya St. Joseph Mission Peramiho mkoani Ruvuma Wilaya ya Songea japo asili ya upande wa baba ni Mzaramo huku upande wa mama akiwa ni Mngoni. Safari ya maisha ya bingwa huyu alikulia maeneo ya Mburahati Barafu jijini Dar es Salaam ambako ndipo alianza kuvutiwa na mchezo wa ngumi akiwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mianzini Mburahati mwaka 1996.
Wakati huo familia yake haikuwa ikiunga mkono mchezo wa ngumi kwani waliuchukulia k**a mchezo wenye hatari kwake hali hiyo ilimfanya Kidunda kujifunza kwa siri kwa kumfuata kocha wake wa kwanza Shaban Amos ambaye alianza kumfundisha misingi ya mchezo huo maeneo ya Mburahati.
Baada ya kumaliza elimu ya msingi Kidunda alianza kucheza ngumi rasmi bila kificho na mwaka 2006 alijiunga na klabu ya Jeshi ya Ngome kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya ngumi za ridhaa na katika kipindi chake akiwa anacheza ngumi za ridhaa Kidunda aliwakilisha Tanzania kwenye mashindano mbalimbali makubwa k**a Mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka 2010 na 2014 pamoja na mashindano makubwa duniani ya Summer Olympics mwaka 2012.
Mwaka 2019 Kidunda aliingia rasmi kwenye ngumi za kulipwa na mpaka anacheza pambano lake la mwisho dhidi ya Asemhale Wellem wa Afrika Kusini mwaka 2024 alikamilisha rekodi ya kuwa na idadi ya mapambano 11, akishinda 9, ushindi wa KO'S 7, kupoteza 0 na sare 2 huku akifanikiwa kutwaa mikanda mbalimbali ya ubingwa ikiwemo Ubingwa wa Taifa wa TPBRC, PST, WBF International na ubingwa wa East and Central mikanda yote hiyo aliipigania katika uzani wa Super Middleweight kg 76.
Hadi sasa haijafahamika rasmi k**a Jini Makata amestaafu rasmi au bado ana mpango wa kurejea ulingoni hata hivyo mwaka 2025 aliongeza ukurasa mwingine kwenye taaluma yake baada ya kuhitimu kozi ya ukocha ya daraja la nyota moja kimataifa kupitia Shirikisho la Ngumi Duniani IBA Mafunzo ambayo aliyapata kwa kujifunza kwa njia ya mtandao kuanzia Julai 28 hadi Agosti 6, 2025.
Bondia Selemani Kidunda amebaki kuwa moja ya simulizi kubwa katika historia ya ngumi nchini Tanzania.
Mn Boxing Media Tanzania
Mn Boxing Media Tanzania
I'm Gentleman
Karibu kwenye ukurasa bora wa Mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwa habari za ndani na Kimataifa hapa ndo nyumbani kwake sisi ni Familia ya Masumbwi.
๐น๐ฟ๐ฐ๐ช๐บ๐ฌ๐ฟ๐ฆ๐จ๐ฉ๐ฌ๐ญ๐ฟ๐ผ๐ฟ๐ฒ๐บ๐ฒ๐ด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ๐ฏ๐ต
Ndani ya kipindi kifupi kuanzia mwisho wa Julai hadi mwanzoni mwa Agosti 2026 mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini Tanzania na Nigeria wameshuhudia mapambano mawili tofauti yaliyofanana na yaliyoibua mijadala kwa mashabiki baada ya kumalizika kwa matokeo ya Disqualification (DQ) kufuatia faulo za mara kwa mara kutoka kwa mmoja wa wapiganaji.
Alhamisi ya Julai 30, 2026 bondia Mtanzania Johnson Kiwia maarufu k**a 'Fundora' alipanda ulingoni kupambana na Simon Dladla wa Afrika Kusini kuwania ubingwa wa PST katika uzani wa Super Welterweight kg 69 kwenye usiku wa "Knockout Ya Mama Season 9" uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo lilimalizika katika raundi ya nne baada ya Dladla kuonywa mara kadhaa kwa kucheza faulo na hatimaye refa Modest Rashid aliamua kulisitisha pambano na kumtangaza Johnson Kiwia kuwa mshindi kwa matokeo ya Disqualification (DQ).
Wakati huo huo usiku wa Julai 31 kuamkia Agosti 1 nchini Nigeria kulitokea tukio jingine lenye kufanana na tukio k**a hilo katika pambano la maonyesho (Exhibition Boxing) lililowakutanisha watu mashuhuri kati ya muigizaji na mchekeshaji Charles Okocha maarufu k**a 'Igwe 2Pac' dhidi ya msanii wa Hip Hop Habeeb Okikiola Badmus maarufu k**a 'Portable'.
Pambano hilo la marudiano lililopewa jina la "Chaos in the Ring Unfinished Business" la raundi nne ubingwa wa Celebrity Boxing Championship lilifanyika katika ukumbi wa Balmoral Convention Centre, Federal Palace Hotel, Victoria Island jijini la Lagos nchini Nigeria.
Na mtanange huo ulimalizika mapema katika raundi ya kwanza baada ya Portable kuonywa kwa kucheza faulo kadhaa kabla ya kuondoka ulingoni na kutokana na kitendo hicho refa aliamua kumaliza pambano na kumtangaza Charles Okocha kuwa mshindi kwa matokeo ya Disqualification (DQ).
Matukio haya mawili yaliwashangaza wadau wengi wa masumbwi huku wakiyataja kuwa miongoni mwa matukio ya nadra ambapo mapambano muhimu yanamalizika kwa Disqualification kutokana na ukiukwaji wa sheria za mchezo badala ya ushindi wa kawaida ulingoni.
Mn Boxing Media Tanzania
Mapambano ya Knockout Ya Mama Season 9 ya mwaka 2026 yalifikia tamati usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam huku Wadau wa mchezo wa masumbwi walipata burudani kupitia mapambano makubwa yaliyowakutanisha mabondia wa ndani nawa kimataifa.
Jumla ya bout 15 zilipigwa huku baadhi ya mabondia wakionyesha viwango vya hali ya juu na wengine wakilazimika kulamba canvas baada ya kupokea makonde mazito yaliyowashusha mbele ya mashabiki na miongoni mwa nyota waliovutia zaidi ni vijana wa kizazi cha Gen Z ambao ni Yusco Bedu miaka 18, Abdulrahmani Magoma miaka 19, Said Hakimu miaka 19 na Salim Hussein miaka 19.
Vijana hawa walionyesha uwezo mkubwa wa kiufundi, matumizi mazuri ya akili ya mchezo (Ring IQ), nguvu, uvumilivu na ulinzi imara jambo linaloonyesha kuwa wanaweza kuwa miongoni mwa mabondia wa kutazamwa kwa miaka ijayo.
Yusco Bedu alicheza pambano lake la kwanza la kimataifa dhidi ya bondia Yamikani Mtambo raia wa Malawi na kuibuka mshindi kwa TKO, Abdulrahmani Magoma naye aliibuka mshindi kwa pointi dhidi ya bondia Lawrence Owino raia wa Kenya.
Said Hakimu aliendeleza ubora wake kwa kuibuka mshindi kwa pointi dhidi ya bondia Asiphe Ntshili raia wa Afrika Kusini huku Salim Hussein akishinda kwa TKO dhidi ya bondia Sem Matheus raia wa Namibia katika pambano lake la kwanza la kimataifa nala ubingwa wa PST Super Featherweight kg 59.
Kwa upande wa Kato Machemba bondia huyu ambaye amekuwa akipanda na kushuka kimchezo alionyesha maboresho kwa kurekebisha baadhi ya mapungufu yake ya awali na kuibuka mshindi kwa pointi dhidi ya bondia Keisham Luckysun raia wa India.
Naye Salim Mtango maarufu k**a "Messi wa Ngumi" alituma ujumbe mzito kwa wapinzani wake baada ya kumaliza kazi mapema kwa kumchapa kwa KO bondia Hussein Makumbi.
Mwishoe ni Ibrahim Mafia na Yohana Mchanja ambao waliandika historia nyingine ya kutwaa mikanda ya WBC International Silver katika uzani wa Bantamweight kg 53 na Flyweight kg 50 ambapo Mafia alimshinda kwa pointi bondia Samuel Laryea raia wa Ghana huku Mchanja naye akiibuka mshindi kwa pointi dhidi ya bondia John Lauriaga raia wa Ufilipino.
Mn Boxing Media Tanzania
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii siku ya jana kocha wa ngumi za kulipwa na mazoezi gym, Kocha Mlosi ametangaza kuwa yeye pamoja na kambi yao wapo tayari kwa uwezekano wa pambano la marudiano kati ya bondia wao Juma Choki maarufu k**a "King Choki" na mpinzani wake Tony Rashid maarufu k**a "AK 47 Bad Belle."
Ikumbukwe kuwa Julai 24 mwaka huu Choki na Tony walikutana katika pambano la raundi 10 wakipambania zawadi ya gari aina ya Toyota Crown Athlete New Model lililofanyika kwenye ukumbi wa East and Central Logistics Centre Ubungo jijini Dar es Salaam.
Pambano ambalo lilimalizika kwa Choki kuibuka mshindi kwa uamuzi wa pointi, baada ya majaji wawili kumpa ushindi yeye huku jaji mmoja akimpa ushindi mpinzani wake Tony Rashid (Spilt Decision).
Kocha Mlosi ambaye ni miongoni mwa makocha wanaomnoa Juma Choki sambamba na kocha mkuu Hamza "Bad Shindo" amesema kuwa wao wapo tayari kurejea ulingoni iwapo kutapatikana promota yoyote atakayefanikisha kuandaa pambano hilo na pande zote mbili zikafikia makubaliano.
Kwa mujibu wa Mlosi, hawana pingamizi lolote kuhusu pambano la marudiano, akisisitiza kuwa litakuwa nafasi nzuri ya kutoa majibu ya mwisho kuhusu ubora wa mabondia hao wawili baada ya mjadala mkubwa uliozuka kufuatia pambano lao la kwanza.
Kauli hiyo imeendelea kuongeza hamasa kwa mashabiki wa mchezo wa masumbwi wengi wao wakiamini kuwa pambano la marudiano kati ya Juma Choki na Tony Rashid ndilo pambano linaloweza kusubiriwa kwa hamu kubwa ili kuondoa kabisa mjadala ulioibuka baada ya pambano la kwanza.
Mn Boxing Media Tanzania
Mapambano ya Dar Boxing Derby kwa mwaka 2026 yaliweza kutamatika siku ya Ijumaa iliyopita kwenye ukumbi wa East Africa Commercial Logistics Centre Ubungo jijini Dar es Salaam na hakika wadau wa mchezo wa Masumbwi hapa nyumbani walipata kujione baadhii ya mabondia waliopata kujitangaza kwenye jukwaa hilo kubwa huku wakionyesha Viwango vyenye kuvutia.
Na hapa nimekuletea list ya Mabondia ambao kwa hakika walipata kuibwa kwenye mapambano hayo kwa kuonyesha Viwango vizuri na mabondia hao ni :
Mohammed Chappo ๐๏ธ Bakari Kibiki
Lilikuwa ni pambano zuri ambalo Chappo aliweza kuutawala mchezo (Dominance) dhidi ya mpinzani wake Kibiki kwa kuonyesha kiwango kizuri kiuchezaji.
Kucheza kwaku Box ndani na nnje, Timing (Wakati sahihi wakupiga ngumi), Good Defence (Kujilinda Vizuri), Hand Speed (Kasii ya mikono), Footwork (Matumizi mazuri ya Miguu), Counter Punches (Ngumi za kujibu Mashambulizi) na Ring IQ (Uwelewa wa kuusoma Mchezo) ni vitu vilivyo mfanya Chappo kuwa bora sana ndani ya ulingo.
Juma Tondola ๐๏ธ Hamza Mengo
Bonge moja la pambano lililokuwa na ushindani kwa mabondia wote wawili japo Tondola aliweza kung'aa zaidii kiufundi na kimbinu kwa kumzidi kete kidogo mpinzani wake Mengo kwa kuonyesha kiwango kizuri kiuchezaji ambapo alikuwa anacheza mfumo waku Box ndani na nnje, Timing, Good Defence, Footwork, Counter Punches na Ring IQ mwamba alikuwa bora sana ndani ya ulingo.
Adam Peter ๐๏ธ Issa Molel
Pambano ambalo Adam aliweza kuutawala mchezo dhidi ya mpinzani wake Molel kwa kuonyesha kiwango kizuri kiuchezaji huku akicheza kwaku Box ndani nakucheza kwa kufuata nakupigana Timing nzuri, Good Defence, Footwork, Counter Punches, Combination Punches (Mchanganyiko wa Ngumi) Ada Boy aliweza kung'aa.
Dorosia Mazige ๐๏ธ Sarah Alex
Pambano ambalo lililoteka hisia za mashabiki kwa upande wa bondia Dorisia licha ya kupoteza pambano hilo dhidi ya bondia mzoefu na mkalii zaidi yake ila aliweza kuonyesha ukomavu mzuri na kuonyesha mchezo mzuri kimbinu kucheza kwa kubox ndani nakucheza kwa kufuata nakupigana, Timing, Good Defence, Footwork, Combination Punches Zuu Wizard aliziteka hisia za mashabiki.
Hakika walifanya kazi nzuri waendelee kujihimarisha na kujituma ili wapate kuwa bora zaidi hongera sana kwao.
Mn Boxing Media Tanzania
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Juma Choki Julai 24 aliweza kuibuka na ushindi dhidi ya mpinzani wake Tony Rashid kwenye Mapambano ya "Dar Boxing Derby" huku akifanikiwa kunyakua tuzo ya zawadi ya gari aina ya Toyota Crown Athlete New Model waliokuwa wakiwania.
Choki aliweza kupata ushindi wa matokeo ya Point ya Majaji wawili kwa mmoja (SD)
1) John Chagu : 94 - 96
2) Josmo Mlundwa : 96 - 94
3) Pembe Ndava : 93 - 97
Matokeo ambayo yalileta ukakasi kidogo kwa baadhii ya wadau wa mchezo wa Masumbwi hapa nyumbani.
Ila turudi darasani kidogo kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa majaji hutumia vigezo vinavyokubalika kimataifa kwenye kutoa alama za matokeo kupitia mapambano na vigezo vinavyo angaliwa ni hivi :
Clean Punching (Mapigo safi) : Kupiga ngumi safii inayotua kwa usahihi kwenye maeneo halali ya mwili kichwani na sehemu ya mbele ya mwili na juu ya mkanda.
Effective Aggression (Mashambulizi yenye matokeo) : Kushambulia na kufanikiwa kupiga ngumi zenye nguvu na zenye madhara, Kumkata mpinzani njia na kumpeleka kwenye kona au kamba.
Ring Generalship (Udhibiti wa pambano) : Bondia anayelazimisha pambano liende kwa mtindo anaoutaka kwa kudhibiti umbali, kasi, na mwelekeo wa pambano.
Defence (Ulinzi) : Uwezo mzuri wa kukwepa kwa kuzuia (block), kuteleza (slip) na aina nyingine za ulinzi ili mpinzani akose kulenga shabaha sahihi.
Kwa kulizingatia hilo Choki na Tony lilikuwa ni pambano kalii sana lenye ushindani mkubwa kwa mabondia wote wawili lililo karibiana sana kimatokeo (Close fight).
Na binafsi kwenye jicho langu la kuona mpaka raundi ya tisa inatamatika mabondia hawa waliachana kwa raundi moja na zilivyo tamatishwa raundi zote kumi mabondia wote wawili waligawana raundi 5 / 5.
Tony alinufaika na vipengele vya Clean Punches, Defence na Effective aggression huku Choki alinufaika na vipengele vya Clean Punches, Defence na Ring Generalship.
Kwa mantiki hiyo Jaji wa mwisho ilibidi afanye maamuzi magumu kwa kuangalia vipengele muhimu vilivyo mshawishi yeye kutoa maamuzi ya mwisho ya mshindi kwa sababu mshindi ilikuwa lazima apatikane kutokana na tuzo ya gari iliyokuwepo mezani na mwishoe akatoa maamuzi yaliyo pelekea kupatikana kwa mshindi wa pambano hilo.
Mn Boxing Media Tanzania
Mabondia wa ngumi za kulipwa nchini Tony Rashid maarufu k**a 'Bad Belle' na mpinzani wake Juma Choki maarufu k**a 'King Choki' wamekamilisha zoezi la kupima uzito leo kuelekea pambano lao kubwa la "Dar Boxing Derby" litakalopigwa kesho.
Tony na Choki watavaana katika pambano kuu la raundi 10 kwenye uzani wa Super Featherweight kg 59 huku wakiwania zawadi ya gari aina ya Toyota Crown Athlete New Model ya mwaka 2010 / 2012 kwa mshindi wa pambano hilo mbali na malipo yao ya kawaida ya kupigana.
Mapambano hayo yameandaliwa na Peak Time Promotion na yatafanyika katika ukumbi wa East Africa Commercial and Logistics Centre, Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Zoezi la kupima uzito limefanyika leo katika Uwanja wa Las Vegas, Mabibo karibu na Soko la Ndizi Engo ambapo iliwapa mashabiki nafasi ya kuwaona mabondia hao wakikamilisha taratibu muhimu kabla ya kupanda ulingoni siku ya kesho.
Na hizi ndizo kg walizopata mabondia hao wote wawili kwenye zoezi hilo la kupima uzito :
Tony : kg 59.3 โ๏ธ
Choki : kg 59.2 โ๏ธ
Tony ana jumla ya Mapambano 24, Ushindi 17, Ushindi wa 'KO'S' 11, Kupoteza 4 Sare 3.
Choki ana jumla ya Mapambano 13, Ushindi 11, Ushindi wa 'KO'S' 4, Kupoteza 1 Sare 1.
Sasa hakuna kilichobaki zaidi ya kusubiri kengele ya pambano na Mashabiki wa ngumi wanatarajiwa kushuhudia ushindani wa hali ya juu ufundi wa kipekee na burudani ya kuvutia huku bingwa wa pambano hilo akiondoka na taji la ushindi pamoja na gari la Toyota Crown Athlete.
Mn Boxing Media Tanzania
Promotion ya ngumi za kulipwa nchini Three T Sport imefanikiwa kukamilisha kwa mafanikio makubwa mapambano ya "Usiku wa Punch To Punch" yaliyofanyika Julai 18, 2026, katika Ukumbi wa Mrina Hall, Tip Top Manzese, jijini Dar es Salaam.
Jumla ya mapambano 15 yalipigwa siku hiyo yakitoa burudani ya hali ya juu kwa mashabiki wa mchezo wa masumbwi chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu na Promota Madam Latifah Jabir akishirikiana na Matchmaker wake Ramadhani Cholila walionyesha kiwango cha juu cha maandalizi na usimamizi wa tukio hilo.
Mbali na ubora wa mapambano waandaaji walihakikisha huduma muhimu zinapatikana kwa viwango bora k**a Usalama wa mashabiki uliimarishwa kupitia uwepo wa Security na Askari, huku huduma za vyakula na vinywaji zikiandaliwa kwa ustadi ili kuhakikisha kila aliyehudhuria anapata huduma bora.
Miongoni mwa mapambano yaliyovuta hisia za mashabiki ni pambano kati ya Jafet Herman na Jack Lupiya, ambapo Jafet aliibuka mshindi kwa matokeo ya pointi baada ya pambano kali lenye ushindani mkubwa.
Pambano jingine lililosisimua ni kati ya Abdul Kubira na Steven Anastazi ambalo lilimalizika kwa matokeo ya sare baada ya mabondia hao kuonyesha ufundi na mbinu za hali ya juu naye Samora Jonas alimshinda Peter Damian kwa matokeo ya pointi akionesha kiwango bora kilichowavutia mashabiki wengi.
Kwa upande mwingine Lutengano John aliibuka mshindi kwa matokeo ya pointi dhidi ya Ally Athumani katika pambano lililojaa ushindani mkubwa ambapo tofauti ya ushindi ilikuwa ndogo kutokana na uwezo wa karibu wa mabondia hao wawili.
Sasa ni siku tano baada ya kufanyika kwa mapambano hayo matokeo yote rasmi tayari yameingizwa katika mtanda wa BoxRec tovuti inayohifadhi takwimu na rekodi za mabondia wa kulipwa duniani.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Promota Madam Latifah aliwashukuru wadhamini wote waliounga mkono mashindano hayo wakiwemo Cleopatra Casino Jackpot, Robby One Pharmacy na Alfa Fitness pamoja na uongozi wa TPBRC kwa ushirikiano wao mkubwa uliochangia mafanikio ya Usiku wa Punch To Punch.
Hongera Promota Madam Latifah Jabir na Matchmaker Ramadhani Cholila kwa kazi nzuri ya kuendeleza mchezo wa masumbwi nchini Tanzania.
Mn Boxing Media Tanzania
Tarehe 24/07/2026 Mabondia wa ngumi za kulipwa nchini Juma Choki a.k.a 'King Choki' na mpinzani wake Tony Rashid a.k.a 'Bad Belle' wanatarajia kupanda ulingoni kwenye mapambano ya "Dar Boxing Derby".
Choki na Tony watacheza pambano kuu la raundi 10 kwenye uzani wa Super Featherweight kg 59 huku wakiwania tuzo ya gari aina ya Toyota Crown Athlete New Model ya mwaka 2010 / 2012 kwa mshindi atakae shinda pambano hilo lililoandaliwa na Promotion ya Peak Time na litafanyika kwenye ukumbi wa East Africa Commercial and Logistics Centre Ubungo jijini Dar es Salaam.
Naam na hapa nimekuletea Uchambuzi Yakinifu kuelekea kwenye pambano hilo kwa kuangazia machache ya kiufundi kiuchezaji kutoka kwa mabondia hao wote wawili
Kiufundi Choki na Tony wote ni mabondia wanaocheza mguu wa kulia (Southpaw) kwenye kutanguliza miguu yao mbele na kiasili kiuchezaji Choki ni 'Boxer' pia ni 'Counter Puncher' mzuri aliyejaaliwa ufundi (Skills) na matumizi ya kucheza kwa Akila na Maarifa (Ring IQ) mwenye kupendelea zaidii kucheza mfumo waku 'Box' kwenye kufanya mitembeo (Movement) ndani ya ulingo huku akicheza kwa umbali dhidi ya wapinzani wake.
Kupanga ngumi za mahesabu huku akitegemea zaidii matumizi ya mashambulizi ya ngumi ya Jab, Right Hook na Counter Punching ni miongoni mwasilaha yake kubwa jambo linalomfanya kuwa hatari akiwa ndani ya ulingo.
Tony ni 'Boxer Puncher' ni bondia aliyejaaliwa ufundi, nguvu na uvumilivu anaeweza kucheza michezo yote miwili kucheza kwaku Box kwa umbali nakucheza kwa kufuata nakupigana huku akiwa mpiganaji zaidii hubadilika kulingana na aina ya mpinzani anaye kabiliana ndani ya ulingo kwenye swala la kiuchezaji.
Matumizi ya kupiga ngumi zenye nguvu k**a Right Hand Punch, Body Punch, Combination's ni miongoni mwasilaha yake kubwa kwenye uchezaji wake jambo linalomfanya kuwa hatari akiwa ndani ya ulingo.
Choki ana jumla ya Mapambano 13, Ushindi 11, Ushindi wa 'KO'S' 4, Kupoteza 1 Sare 1.
Tony ana jumla ya Mapambano 24, Ushindi 17, Ushindi wa 'KO'S' 11, Kupoteza 4 Sare 3.
Pambano zuri lenye ushindani wenye kushiba mabondia wote wawili jiandaeni vizuri mje kuonyesha mchezo mzuri utakaoacha alama na historia tunawatakia maandalizi mema na kila kheri kwenu.
Mn Boxing Media Tanzania
MN Boxing Media Tanzania chini ya mchambuzi na mwandishi wake wa masuala ya mchezo wa masumbwi Munir Nadri, inapenda kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa promota George Shao maarufu k**a Gadaphy "The Friend You Need" pamoja na promota Madam Latifah Jabir kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuandaa mapambano ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania katika mwaka huu wa 2026.
Gadaphy Sports Promotion chini ya promota wake George Shao ameweza kuandaa mapambano mawili makubwa yaliyovutia mashabiki wengi wa masumbwi hapa nyumbani ambapo tarehe 21/03/2026 waliandaa mapambano ya "The Eid Battle" na kufuatiwa na mapambano ya "The June Battle" yaliyofanyika tarehe 27/06/2026 burudani zote hizo mbili zilifanyika katika ukumbi wa Lamasia Village, Dege Mchikichini, Kigamboni jijini Dar es Salaam na ziliacha alama kubwa kwa wadau wa mchezo huu.
Kwa upande wa promota Madam Latifah Jabir chini ya promotion yake ya Three T Sports naye ameendelea kuonyesha dhamira ya kukuza mchezo wa masumbwi kwa kuandaa mapambano mawili ndani ya mwaka huu.
Tarehe 28/03/2026 waliandaa mapambano ya "Usiku wa Majabali" yaliyofanyika katika ukumbi wa Brightstone Hall, Mbezi Beach, Tangi Bovu kisha tarehe 18/07/2026 aliandaa kwa mafanikio makubwa mapambano ya "Usiku wa Punch to Punch" yaliyofanyika katika ukumbi wa Mrina Hall, Manzese, Dar es Salaam mapambano hayo yalitoa burudani ya kiwango cha juu na kuwavutia mashabiki wengi wa ngumi.
Kutokana na juhudi, ubunifu na kujituma kwa mapromota hawa wawili, MN Boxing Media inaamini kuwa wana mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza mchezo wa masumbwi nchini ni mapromota wenye maono makubwa na uwezo wa kuandaa matukio yanayozidi kuimarisha hadhi ya ngumi za kulipwa Tanzania.
Aidha, MN Boxing Media inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Gadaphy Sports Promotion, Three T Sports Promotion, Everybody Can Punch Promotion na Mitra Boxing Promotion kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kutupa kwa kuwatangazia mapambano yao katika kukuza mchezo wa masumbwi nchini tunasema ahsanteni kwa kutuamini.
Hongereni sana kwa kazi kubwa mnayoifanya tunawatakia mafanikio zaidii kwenye kuanda mapambano ya ngumi za kulipwa.
Mn Boxing Media Tanzania
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mabibo
Dar Es Salaam