Mabondia wa Ngumi za Kulipwa nchini Lulu Kayage a.k.a 'Anaconda' na mpinzani wake Jennifer Bernard Sige a.k.a 'Jennifer Zugo' almaarufu 'Kiboko Ya Warembo' Tarehe 27/06/2026 wanatarajia kupanda ulingoni kwenye mapambano makali ya Usiku wa Vyuma Vitaumana.
Kayage na Jennifer watacheza pambano la raundi 6 za Moto kwenye uzani wa Super Bantamweight kg 44 lililoandaliwa na Mitra Boxing Promotion huku likifanyika kwenye ukumbi wa Heinken Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Hili ni pambano lenye mvuto zaidii lenye Heshima na Kisasi ndani yake upande wa Kayage ni bondia mkongwe aliyeingia kwenye mchezo huu tangu mwaka 2017 mwenye uzoefu wakutosha aliyewahii kushea ulingo mmoja dhidi ya mabondia mashughuli kwenye upande wa ngumi za kulipwa kwa Wanawake k**a Stumai Muki, Jesca Mfinanga, Halima Vunjabei n.k huku akicheza mapambano kadhaa ya kimataifa nnje ya mipaka ya Tanzania.
Jennifer ni bondia damu changa anayechipkia kwenye mchezo huu anaesimamiwa na Zugo Boxing Gym chini ya kocha wake Selemani Zugo na hapa kuna kisasi ndani yake kwani itakumbukwa bondia Kayage alishawahii kuwa chini ya mikono ya kocha Zugo kabla ya kutengana kwao na kwa kipindi cha miaka kadhaa bondia huyo amewahii kuwapiga mabondia wengi kutoka kwa kocha wake huyo na safari hii anaenda kukutana na kiboko ya Warembo Jennifer miongoni mwamabondia wakali wanaokuja nakufanya vizuri kwenye mchezo huu.
Kiufundi kiuchezaji Kayage na Jennifer wote ni mabondia wanaocheza upande sawa wa kushoto (Orthodox) kwenye kutanguliza miguu yao ya mbele na kiasili Kayage ni bondia ambaye ni Pure Fighter mwenye kucheza mfumo wakufuata nakupigana na Jennifer ni bondia ambaye ni Boxer mwenye kucheza mfumo waku Box ndani ya ulingo huku akifanya mitembeo na kuweka gepu la nafasi kwa ajili ya score point's za ushindi.
Kayage ana Total Fight's 27, Win's 8, 'KO'S' 2, Lose 15 Draw 4.
Jennifer ana Total Fight's 2, Win's 1, 'KO'S' 1, Lose 0 Draw 1.
June 27 hapa Anaconda pale Kiboko ya Warembo unipe heshima yangu au niichukue kwa nguvu tukutane ndani ya Mtoni Kijichi tukaone mikono ikisema usikose familia.
Mn Boxing Media Tanzania
Mn Boxing Media Tanzania
I'm Gentleman
Karibu kwenye ukurasa bora wa Mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwa habari za ndani na Kimataifa hapa ndo nyumbani kwake sisi ni Familia ya Masumbwi.
🇹🇿🇰🇪🇺🇬🇿🇦🇨🇩🇬🇭🇿🇼🇿🇲🇺🇲🏴🇯🇵
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini M***a Ally a.k.a 'Champion M***a M***a' Tarehe 27/06/2026 anatarajia kupanda ulingoni kwenye Mapambano makalii sana ya 'The June Battle' yenye hash tag ya .
M***a ni bondia anaesimamiwa Fitness Kwanza Gym iliyopo maeneo ya Kibada Kigamboni na June 27 anatarajia kucheza pambano la raundi 6 kwenye uzani wa Featherweight kg 57 dhidi ya bondia Noel Sabugo kutoka maeneo ya Kimara.
Pambano hilo limeandaliwa na Gadaphy Sports Promotion chini ya promota wake George Shao a.k.a 'Gadaphy The Friend You Need' na litafanyika kwenye ukumbi wa Lamasia Village uliopo maeneo ya Dege Mchikichini Kigamboni huku likidhaminiwa na Robby One pharmacy , Lamasia Village, Isangaleli Stitching, Mtondo Boxing Revolution, Ourevent Luxe, YasTanzania, Shaosons furniture's na Mn Boxing Media Tanzania.
Bondia M***a ameaminiwa nakupewa nafasi na Promota Gadaphy ambapo ataenda kupiga hatua yake ya kwanza ya kutengeneza njia ya kuelekea kuwa bondia rasmii wa ngumi za kulipwa maana iliuwe na vigezo vya kucheza pambano la kwanza la ngumi za kulipwa na liingie kwenye mtandao wa kuhifadhii Data na Rekodi za Mabondia wote Duniani Boxrec kwa mujibu wa kamisheni ya mchezo wa ngumi za kulipwa nchini (TPBRC) inabidi bondia awe amecheza ngumi za ridhaa au awe amecheza mapambano matatu ya ngumi za kulipwa ya kujipima baada ya hapo ndipo atakuwa amefaulu kuingia rasmii kwenye mchezo huu.
Na bondia M***a akiwa na njaa kalii ya mafanikio anaenda kupanda ulingoni dhidi ya mpinzani wake Noel Sabugo kwenye pambano lake la kwanza la kipimo kuelekea kwenye safari yake ya kuwa bondia rasmii wa ngumi za kulipwa huku akiwahaiidi mashabiki zake ushindi wa mapema wa Knockout dhidi ya mpinzani wake Sabugo mwenye we anakwambia anaingia nakutoka.
Gadaphy kawaamini vijana nguvu mpya kazi mpyaa tukutane ndani ya Lamasia Village June 27 yani Acha Zipigwe usikose familia.
Mn Boxing Media Tanzania
Zimebakia siku 4 pekee kwa bondia wa ngumi za kulipwa nchini Hassani Mwakinyo Jr a.k.a 'Champez Onetyme' kupanda ulingoni Tarehe 10/06/2026 kucheza pambano la Kimataifa nala Ubingwa nchini Ivory Coast.
June 10 Mwakinyo Jr anatarajia kucheza pambano la Kimataifa nala Ubingwa wa Dunia wa IBO (International Boxing Organization World Middleweight kg 72) dhidi ya bondia Michel Soro raia wa Ufaransa na Ivory Coast linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Parc Des Exposition jijini Abidjan nchini Ivory Coast huku likiandaliwa na Dream Ring Boxing Promotion.
Mpinzani wake Mwakinyo Jr bondia Soro licha ya kwamba yeye ni mkazi wa nchini Ufaransa ila tayari ameshatua mda sana nchini Ivory Coast tangu mwezi watano mwaka huu ambapo ni ardhii ya nyumbani kwao alipozaliwa October 30, 1987 jijini Abidjan na maandalizi ya mazoezi kuelekea kwenye pambano lake na Mwakinyo Jr yameshaanza na baadhii ya clip zimekuwa zikipostiwa nakuonekana kwenye baadhii ya kurasa za mitandao ya kijamii kutoka nchini humo.
Lakini hiyo ipo tofauti kwa bondia Champez Onetym ambaye ana mda sana yupo kimya kwenye maandalizi yake ya pambano hili huku tetesi kadhaa zikieleza ya kwamba bondia huyo amejikita kwenye kambi nzito akijianda kwa usiliasi mkubwa mno kwenda kuandika historia ya kuwa Mtanzania wapili kuutwaa Ubingwa wa Dunia wa IBO.
Nasii hivyo tu nchii ya Ivory Coast ina mabondia k**a Ryad Merhy, Kalilou Camara Souhali Bamba na huyu Michel Soro ambaye endapo Mwakinyo Jr atafanikiwa kumpiga basi atakuwa amempiga miongoni Mwamabondia Malejendari wa mchezo huo nchini humo kwenye hiyo list niliyokutajia hapo juu wenye kupewa heshima kubwa kutokana na yale yote waliyowahii kuyafanya kupitia mafanikio yao waliyopata kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa Duniani.
Ambapo kwa upande wa Soro amewahii kupata nafasi ya kuwania mikanda mikubwa ya ubingwa wa Dunia wa WBO na IBO kwenye uzani wa Super Welterweight kg 69 mwaka 2012 pia ni bingwa wa zamani aliyewahii kuushikilia mikanda ya WBO Europe na WBA International kwenye uzani wa Super Welterweight kg 69.
Soro ana rekodi ya Total Fight's 44, Win's 38, 'KO'S' 27, Lose 4 Draw 2.
Mwakinyo Jr ana rekodi ya Total Fight's 28, Win's 25, 'KO'S' 18, Lose 3 Draw 0.
Waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo zimebakia siku 4 pekee ngoma inasoma Tiktaki Tiktaki Tiktaki ⏰.
Mn Boxing Media Tanzania
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Abdallah R Hassani a.k.a 'Tagawa' Tarehe 27/06/2026 anatarajia kupanda ulingoni kwenye Mapambano makalii sana ya 'The June Battle' yenye hash tag ya .
Tagawa ni bondia anaesimamiwa Man Pamba Boxing Club iliyopo maeneo ya Mbezi na June 27 anatarajia kucheza pambano la raundi 6 kwenye uzani wa Bantamweight kg 53 dhidi ya bondia Heri Lutani Mbilinyi kutoka maeneo ya Mbezi.
Pambano hilo limeandaliwa na Gadaphy Sports Promotion chini ya promota wake George Shao a.k.a 'Gadaphy The Friend You Need' na litafanyika kwenye ukumbi wa Lamasia Village uliopo maeneo ya Dege Mchikichini Kigamboni huku likidhaminiwa na Robby One pharmacy, Lamasia Village, Isangaleli stitching, Mtondo Boxing Revolution, Ourevent Luxe, Yas Tanzania, Shaosons Furniture na Mn Boxing Tanzania.
Bondia Tagawa mixer Mbongo mixer Mjapan usishangaee ni bondia mzoefu kidogo aliyeingia kwenye mchezo huu tangu mwaka 2017 ana miaka 9 kwenye game ambapo amewahii kushea ulingo mmoja dhidi ya mabondia mashughuli k**a Ally Ngwando, Mukhsin Kizota, John Chuwa, Ramadhani Pido n.k na June 27 ameaminiwa nakupewa nafasi na Promota Gadaphy ambapo ataenda kucheza pambano lake la kwanza ndani ya mwaka huu wa 2026.
Kiufundi kiuchezaji Tagawa ni bondia anaecheza mguu wa kushoto (Orthodox) kwenye kutanguliza mguu wake wa mbele na kiasili huyu ni 'Pure Fighter' bondia anaecheza mfumo wakufuata nakupigana zaidii huku akicheza ndani ya zone ya mpinzani kwa ajili ya kufanya mashambulizi.
Mashambulizi yake pendwa ni Jab, One Two Combination, Left Hook, Right Over Hand & Combination Punches na kwenye swala la kujilinda hutumia Defense za High Guard, Parry na Blocking na hapo chini ndiyo asilimia za ubora wake kwenye kila engo muhimu za upiganaji wake :
Nguvu za Mikono : 40%
Uvumilivu : 60%
Kasii ya Mikono : 50%
Ulinzi : 40%
Ubora wa Miguu : 50%
Ufanisi Ulingoni : 40%
Rekodi : Total Fight's 12, Wins 3, 'KO'S' 1, Lose 8 Draw 1.
Gadaphy kumuamini Tagawa mixer Mbongo mixer Mjapan tukutane ndani ya Lamasia Village June 27 yani Acha Zipigwe usikose familia.
Mn Boxing Media Tanzania
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Rahimu Athumani Nyanyage Tarehe 27/06/2026 anatarajia kupanda ulingoni kwenye Mapambano makalii sana ya 'The June Battle' yenye hash tag ya .
Rahimu ni bondia anaesimamiwa B Combination Gym iliyopo maeneo ya Mbagala na June 27 anatarajia kucheza pambano la raundi 6 kwenye uzani wa Super Featherweight kg 58 dhidi ya bondia Rajabu Salum Lukemo kutoka maeneo ya Chamazi.
Pambano hilo limeandaliwa na chini ya promota wake George Shao a.k.a 'Gadaphy The Friend You Need' na litafanyika kwenye ukumbi wa Lamasia Village uliopo maeneo ya Dege Mchikichini Kigamboni huku likidhaminiwa na Robby One pharmacy, Lamasia Village, Isangaleli stitching, Mtondo Boxing Revolution, Ourevent Luxe, Yas Tanzania, Shaosons Furniture na Mn Boxing Tanzania.
Rahimu ameaminiwa nakupewa nafasi na Promota Gadaphy ambapo ataenda kucheza pambano lake la kwanza la ngumi za kulipwa kirekodi na hapa tutamuangalia kwenye yale machache aliyokuwa nayo kwenye uchezaji wake kupitia idadi ya mapambano yake mawili aliyowahii kucheza kabla ya kuingia rasmii kwenye ngumi za kulipwa moja alishinda kwa matokeo ya Point na moja alitoka Sare (Draw).
Kiufundi kiuchezaji Rahimu ni bondia anaecheza mguu wa kushoto (Orthodox) kwenye kutanguliza mguu wake wa mbele na kiasil huyu ni Boxer bondia anaecheza mfumo waku Box kwenye kufanya mitembeo ndani ya ulingo huku akiweka gepu la nafasi kwa ajili kuscore point's za ushindi na kujilinda pia.
Mashambulizi yake pendwa ni Jab, One Two Combination, Straight Right Hand Punch, Left Hook & Counter Punching na kwenye swala la kujilinda hutumia Defense za footwork, Slip na Blocking.
Na hapo chini ndiyo asilimia za ubora wake kwenye kila engo muhimu za upiganaji wake :
Nguvu za Mikono : 40%
Uvumilivu : 50%
Kasii ya Mikono : 50%
Ulinzi : 50%
Ubora wa Miguu : 50%
Ufanisi Ulingoni : 40%
Rekodi : Debut
Gadaphy kawaamini vijana nguvu mpya kazi mpyaa tukutane ndani ya Lamasia Village June 27 yani Acha Zipigwe usikose familia.
Mn Boxing Media Tanzania
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Mohammed Salum Tarehe 27/06/2026 anatarajia kupanda ulingoni kwenye Mapambano makalii sana ya 'The June Battle' yenye hash tag ya .
Mohammed ni bondia anaesimamiwa Sparta Boxing gym iliyopo maeneo ya Kigamboni June 27 anatarajia kucheza pambano la raundi 6 kwenye uzani wa Middleweight kg 70 dhidi ya bondia Vicent Philipo Matoboki kutoka maeneo ya Mbagala Rangi Tatu.
Pambano hilo limeandaliwa na Gadaphy Sports Promotion chini ya promota wake George Shao a.k.a 'Gadaphy The Friend You Need' na litafanyika kwenye ukumbi wa Lamasia Village uliopo maeneo ya Dege Mchikichini Kigamboni huku likidhaminiwa na Robby One pharmacy, Lamasia Village, Isangaleli stitching, Mtondo Boxing Revolution, Ourevent Luxe, Yas Tanzania, Shaosons Furniture, Mn Boxing Tanzania, Kilimanjaro Expeditions na Paradiso Hotel.
Na hii ni bout ya tatu kalii tunaimailizia kuelekea kwenye mapambano makali ya The June Battle ambapo tutamdadavua bondia Mohamed Salum baada ya hapo jana kutoa taarif ya tambo za mpinzani wake Vicent Matoboki na kumchambua kiufundi zaidii ambao wote kwa pamoja wanaenda kucheza pambano lao la kwanza la ngumi za kulipwa.
Kiufundi kiuchezaji Mohammed ni bondia anaecheza mguu wa kushoto (Orthodox) kwenye kutanguliza mguu wake wa mbele na kiasili yeye ni Fighter hajajaliwa sana Ufundi kwenye uchezaji wake ila ni bondia anaecheza mfumo wakupigana kwa kupiga ngumi moja moja nzito na kalii.
Mashambulizi yake pendwa ni Jab, One Two Combination, Right Hand Punch na Left Hook na kwenye swala la kujilinda hutumia Defense za High Guard na Blocking.
Na hapo chini ndiyo asilimia za ubora wake kwenye kila engo muhimu za upiganaji wake kupitia idadi ya mapambano yake manne aliyowahii kucheza kabla ya kuingia rasmii kwenye ngumi za kulipwa matatu alishinda kwa Knockout na moja alishinda kwa Point :
Nguvu za Mikono : 60%
Uvumilivu : 50%
Kasii ya Mikono : 40%
Ulinzi : 40%
Ubora wa Miguu : 40%
Ufanisi Ulingoni : 40%
Rekodi : Debut
Gadaphy kawaamini vijana tukutane ndani ya Lamasia Village June 27 yani Acha Zipigwe.
Mn Boxing Media Tanzania
Tarehe 27/06/2026 mabondia wa ngumi za kulipwa nchini Ramadhani Mkwakwate a.k.a 'Sugu Mtata' na mpinzani wake Medrick Mohammed Mwarugaja wanatarajia kupanda ulingoni kwenye mapambano makali ya 'Vyuma Vitaumana'.
Mkwakwate na Mwarugaja mabondia hawa wawili wanatarajia kucheza pambano kalii la raundi 8 kwenye uzani wa Middleweight 72 lililoandaliwa na Promotion ya Mitra Boxing Promotion litakalo fanyika kwenye ukumbi wa Heinken Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam huku kiingilio kikawa ni Sh 5000 tu kwa pesa ya Kitanzania.
Kiufundi hili ni pambano linaloenda kuwa kutanisha mabondia wenye kucheza upande sawa wa kushoto (Orthodox) kwenye kutanguliza miguu yao ya mbele waliojaaliwa ufundi wa daraja la kati kwenye uchezaji wao wana nguvu, uvumilivu, wepesi na kasii na kiasili kupitia uchezaji wa Mkwakwate ni bondia anaetokea kwenye kundi la staili ya Boxer Puncher mwenye uwezo wa kucheza michezo yote miwili kucheza kwaku Box kwenye kufanya mitembeo ndani ya ulingo huku akipanga ngumi kwa ajili ya kuscore point's za ushindi na kucheza ndani ya zone ya mpinzani huku akifuata nakupigana nakuweka mitego ya knockout's akiwa mpiganaji zaidii.
Mwarugaja ni bondia anaetokea kwenye kundi la staili ya Pressure Fighter na kiasili jamaa ni Pure Fighter mwenye kucheza mfumo wa kufuata nakupigana huku akicheza ndani ya zone ya mpinzani muda mwingi kwa ajili ya kuscore point's za ushindi nakuweka mitego ya knockout's.
Kwa hiyo tunaweza kushuudia pambano kalii sana kati ya mabondia hawa litakalo kuwa na mabadiriko ya kiuchezaji na kimbinu kupitia mashambulizi makali ya kupigana sana kwa kubadilishana ngumi na kucheza pia kwa kutumia akili na maarifa kwenye mfumo waku Box ambapo hapa bondia Mkwakwate anaweza kuwa anabadirisha rhythm ya uchezaji kwa nyakati tofauti tofauti kwenye pambano hilo.
Mkwakwate ana rekodi ya Total Fight's 17, Win's 12, 'KO'S' 7, Lose 4 Draw 1.
Mwarugaja ana rekodi ya Total Fight's 3 Win's 1, 'KO'S' 0, Lose 0 Draw 2.
June 27 Ugali Moto Mboga Moto Zitapigwa Kiume hii sii ya kukosa familia ya Masumbwi na Wakazi wa Wilaya ya Temeke.
Mn Boxing Media Tanzania
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Ally A Mulenga Tarehe 27/06/2026 anatarajia kupanda ulingoni kwenye Mapambano makalii sana ya 'The June Battle' yenye hash tag ya .
Mulenga ni bondia anaesimamiwa na B Combination B iliyopo maeneo ya Mbagala chini ya kocha wake Babu Ally na June 27 anatarajia kucheza pambano la raundi 6 kwenye uzani wa Super Lightweight kg 63 dhidi ya mpinzani wake Samuel Mputi a.k.a 'Mdudu' kutoka maeneo ya Mbezi Stendi Magufuli.
Pambano hilo limeandaliwa na Gadaphy Sports Promotion chini promota wake George Shao a.k.a 'Gadaphy The Friend You Need' na litafanyika kwenye ukumbi wa Lamasia Village uliopo maeneo ya Dege Mchikichini Kigamboni huku likidhaminiwa na Robby One Pharmacy, Village, Isangaleli stitching, Mtondo Boxing Revolution, Ourlevent Lex, Yas Tanzania, Shaosons furniture, Mn Boxing Tanzania, Kilimanjaro Expedition, Paradiso Hotel na Artwork Burudika.
Na hii ni bout ya pili kalii ambapo tunamalizia kumdadavua bondia Mulenga na tambo zake baada ya hapo awali kuchapisha sehemu ya kwanza ya mpinzani wake Mputi kuelekea kwenye mapambano ya kibabe ya The June Battle.
Kiufundi kiuchezaji Mulenga bondia anaecheza mguu wa kushoto (Orthodox) kwenye kutanguliza mguu wake wa mbele mwenye kucheza mifumo ya kuchanganya kwenye swala uchezaji wake kucheza kwa kufuata nakupigana huku akicheza ndani ya zone ya mpinzani huku akiwa mpiganaji zaidii nakucheza kwaku Box ndani kwa kuibiaibia kidogo huku akiscore point za ushindi na uchezaji wake haujatofautiana sana na mpinzani wake Mputi jambo linalofanya pambano hili kuwa tamu zaidii.
Mashambulizi yake pendwa ni Jab, One Two Combination, Left Hook, Double Hook's, Right Over Hand na Combination Punches na kwenye swala la kujilinda hutumia Defense za High Guard, Bobbing na blocking.
Na hapo chini ndiyo asilimia za ubora wake kwenye kila engo muhimu za upiganaji wake kupitia idadi ya mapambano yake aliyocheza kwenye rekodi yake hadi hivi sasa :
Nguvu za Mikono : 50%
Uvumilivu : 60%
Kasii ya Mikono : 50%
Ulinzi : 50%
Ubora wa Miguu : 50%
Ufanisi Ulingoni : 40%
Rekodi : Total Fight's 8, Win's 4, 'KO'S' 2, Lose 2 Draw 2.
Gadaphy kawaamini vijana tukutane ndani ya Lamasia Village June 27 yani Acha Zipigwe.
Mn Boxing Media Tanzania
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mabibo
Dar Es Salaam