Rosam Sports

Rosam Sports

Share

Sports News, Results, Fixture and Rumours

06/07/2024

Kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos ametangaza kustaafu soka la ushindani baada ya timu ya taifa Ujerumani kutolewa katika kombe la Euro 2024 dhidi ya Hispania.

Kuna vitu tunavikosa miguuni mwake pasi za magoli, ubunifu, krosi, faili za hatari na kila kitu kilichopo miguuni mwake.

Kwaheri Legend.

01/07/2024

Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji Kelvin De Bruyne ameeleza kuwa bado yupo katika klabu ya Manchester City sababu ni bado mwajiriwa wa klabu hiyo.

De Bruyne ameeleza hayo nchini Ujerumani katika mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa anasikia tetesi nyingi za kwenda Uarabuni lakini kwa upande wake haijaja ofa yoyote mezani.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa endapo kocha wake Pep Guardiola ataridhia kuondoka basi ataanza kupokea ofa za timu mbalimbali ila kwa sasa afikirii jambo hilo.

01/07/2024

Kiungo kutokea taifa la Scotland na klabu ya Newcastle United ya nchini England, Elliot Anderson amejiunga na klabu ya Nottingham Forest ya nchini humo

Nottingham wametoa ada ya pauni milioni 35 kwa klabu ya Newcastle na kupata saini ya kiungo huyo kwa mkataba wa miaka mitano yaani mpaka mwaka 2029.

Elliot inakuwa ni klabu yake ya tatu tangu kuanza kwa maisha yake ya mpira akitokea Bristol Rovals ambapo alikuwa kwa mkopo akitokea Newcastle United.

14/06/2024

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania ameeleza wazi ya kuwa yupo tayari kupokea ofa kutoka katika klabu yoyote endapo itaonesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Morata aliyewahi kutamba na baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya k**a Juventus na Chelsea ameeleza hayo baada ya kuona kuwa hakuna mazungumzo yoyote kati yake na klabu ya Atletico Madrid hivyo imempasa kueleza hayo.

Katika mkataba wake kuna kipengele cha kusajiliwa kwa dau la Euro milioni 12 kwa timu itakayomuhitaji kwa kipindi hiki cha kiangazi.

14/06/2024

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Luciano Spalleti ametoa onyo kali na kuweka sheria ngumu kwa wachezaji wa timu hiyo kuelekea michuano ya kombe la Euro 2024 yanayotarajiwa kuanza leo nchini Ujerumani.

Spalleti amewaeleza wachezaji wote kupitia mkutano na waandishi wa habari na kusema wazi kuwa ameweka sheria tano ambazo.

1. Kutochelewa katika mikutano yao yote.

2. Hakuna kutumia simu wakati wa chakula cha mchana na chakula cha usiku.

3. Wachezaji hawatakiwi kutumia head phones kwa ajili ya kusikiliza music na vitu vingine.

4. Hakuna kutaniana kupita kiasi kati ya wachezaji kwa wachezaji na hata benchi la ufundi.

5. Hakuna kuweka Playstation katika kila chumba cha wachezaji isipokuwa kutakuwa na playstation moja tu ya wote.

Je haya mambo yangekuwa katika timu ya taifa yetu tungeweza?

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Dar Es Salaam