31/05/2025
INAELEZWA, Rais wa Simba SC, Mohammed 'MO' Dewji ameridhishwa na utendaji wa Kocha Fadlu Davids katika msimu huu kwanza.
Tajiri amemtaka asalie kikosini huku akimhakikishia usajili mzito dirisha kubwa; baada ya Kocha kumjuza kuwa anahitaji mastaa wapya wa maana.
(Mwanaspoti)
31/05/2025
🚨| AISHI SALUM MANULA UPDATES
- Klabu ya APR FC ya nchini Rwanda imeonesha nia ya kuhitaji saini ya golikipa wa Simba SC, Aishi Manula (29) ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika klabu ya Simba SC
- APR FC inamfatilia Aishi Manula ili kutambua uwezo wake ili kufanya maamuzi sahihi na ya haraka kwa maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao lakini bado hawajaweka ofa rasmi mezani katika Menejimenti ya Aishi Manula
- Aishi Manula anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru ( Free agent ) na bado hajajua mustakabali wake ndani ya Simba SC, na deal lipo on mpaka sasa akifatiliwa na APR FC.
31/05/2025
🚨GUINEA IMEKATA RUFAA TENA DHIDI YA TANZANIA KUFUZU AFCON.
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) litafanya kikao cha kusikiliza rufaa inayohusu Timu ya Taifa ya Guinea 🇬🇳 na Taifa Stars 🇹🇿 mnamo Juni 11 saa 5:00 asubuhi.
Kikao hicho kitafanyika katika makao makuu ya CAF yaliyopo Nchini Misri 🇪🇬 Cairo.
Fahamu hili: Guinea inapanga kuandaa ujumbe wa watu 20 kwenda Misri kukutana na Kamati ya Rufaa ya CAF.
Ikumbukwe kuwa : Guinea wanadai kuwa Tanzania ilimchezesha mchezaji ambaye hakutambulika na ambaye namba ya jezi yake haikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa siku ya mechi, katika mchezo uliochezwa tarehe 19 Novemba 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kesi ya awali ya Guinea ilikataliwa, lakini wamekata rufaa, na CAF imepanga kusikiliza hoja zao tarehe 11 Juni.
Source : Micky Jr
30/05/2025
Mwamuzi mwenye beji ya FIFA, Ahmed Arajiga ameteuliwa kuwa mwamuzi namba moja katika mchezo wa nusu fainali kombe la TFF kati ya Singida Black Stars FC watakaobiliana na Simba SC katika dimba la Tanzanite Kwaraa mjini Babati hapo kesho.
Wakati huo huo Mwamuzi Msaidizi, Glory Tesha atakuwa miongoni mwao Waamuzi wasaidizi kwenye mchezo wa huo akiwa k**a Mwamuzi Msaidizi namba moja.
Ukisikia kiatu kipya ila mguu wa zamani , ndio hii sasa.
30/05/2025
⚫💎| UPDATE: ARTHUR BADA
- Mazungumzo ya Singida Black Stars na Young Africans 🇹🇿 kuhusu uhamisho wa Arthur Bada (22) yapo very serious 🔥
- Young Africans SC tayari wametuma ofa rasmi mezani (undisclosed fee)
- No problem on player side, It’s up to Singida Black Stars.
30/05/2025
UPCOMING TRANSFER WINDOW 🪟 UPDATE
Klabu ya waydad Casablanca wapo kwenye mazungumzo na klabu ya Ittihad Tanger kwa ajili ya kumsajili winga wao HAMZA EL OUASTI lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa wala usajili uliokamilika.
Mazungumzo yanaendelea na wakifikia muafaka kila kitu kitamalizwa.
30/05/2025
Steven Mguto amesema kuwa wao hawatishiki na wanaoandika mabango ya kutocheza.Wao k**a Bodi ya Ligi wanachojua mechi ipo pale pale. "Wao waandike tu kwenye Tshirt.
Sisi tumeshapanga tarehe basi" Steven Mguto, Mwenyekiti anayekaribia kumaliza muda wake bodi ya Ligi.
30/05/2025
NOW! 🚨🚨
Kocha wa Simba Fadlu Davids ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Mei kwenye Ligi Kuu ya NBC akiwashinda Miloud Hamdi kutoka Yanga na Rachid Taoussi wa Azam FC.
Kocha Fadlu ameiwezesha timu yake kushinda mechi zote tano kwenye ligi kuu hivyo kuibuka kinara katika tuzo hiyo.
Aidha , Mshambuliaji wa Simba Steven Mukwala ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei kwenye Ligi Kuu akiwashinda Jean Charles Ahoua wa Simba na Japhary Kibaya wa Mashujaa
Mukwala amehusika kwenye mabao manne kwa mwezi Mei, akifunga matatu na kutoa assist moja hivyo kuibuka kidedea kwenye tuzo hiyo.
Kwa mtazamo wako unaona wamestahili?
30/05/2025
Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs 🇿🇦, Nasreddine Nabi 🇹🇳, anaonyesha nia kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Simba SC 🇹🇿, Kibu Denis.
Nabi anamtaka mchezaji huyo kujiunga na kikosi chake kwa msimu ujao licha ya kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika baina ya klabu na klabu wala klabu na mchezaji bali limekuwa pendekezo la kocha na hivi karibuni atawasilisha pendekezo hilo kwenye uongozi wa klabu ( Kaizer Chiefs ).
30/05/2025
MOHAMED HUSSEIN TRANSFER UPDATE🔴
- Simba SC imemaliza makubaliano na beki wa kushoto, Mohamed Hussein kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo
- Mohamed Hussein atasaini mkataba mpya na Simba SC hivi karibuni, na nafasi ya mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein ya kujiunga na Kaizer Chiefs ni ndogo sana
- Mohamed Hussein ambaye amekuwa na muendelezo bora sana katika klabu ya Simba SC, ni miongoni mwa mabeki watatu wa kushoto wanaohitajika na Kaizer Chiefs.
30/05/2025
🎯Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Faisal Salum Fei Toto ameridhia kujiunga na klabu ya Simba baada ya kupewa ofa kubwa ya milioni 800 k**a ada ya usajili, mshahara wa milioni 50 kwa mwezi na atapewa nyumba na gari pia atapewa bonasi kila akifunga goli au kutoa usaidizi wa goli (assist).
-Kwa sasa Simba wanamalizana na Azam. Pia Azam haina shida yoyote kuhusu kumwachia nyota huyo akifuata masharti ya kimkataba pamoja na hayo meneja wa Fei Toto amesema kuwa hakuna kipengele chochote iwapo Feisal akiuzwa Tanzania klabu ya Yanga inapewa hela
29/05/2025
WYDAD CASSABLANCA KUKIPIGA NA FC PORTO YA URENO TAREHE 31 MEI.
👉Timu ya nyota kutoka Tanzania na mchezaji aliyeondoka Yanga,Stephan Aziz Ki itawakarbisha mabingwa wa ULAYA Mwaka 2004, FC Porto katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Mohamed wa 5
👉Huu ni muendelezo wa michezo ya kirafiki ya kujiandaa na Kombe la dunia la vilabu litakaloanza mwezi WA 6 Nchini Marekani ambapo Klabu hiyo itashiriki.
👉