10/05/2026
➡️ Habari za ndani kabisa zinasema wachezaji 4 wa Azam FC wameugua ghafla baada ya mechi ya jana, mpaka leo baadhi yao wamepelekwa hospitali. Miongoni mwao ni
1. Ashrafu Kibeku ambaye hali yake inaelezwa si nzuri sana.
2. Pascal Msindo ambaye pia inaelezwa anapata shida kwenye kupumua na kooni kwake
3. Feisal Salum
4. Lusajo Mwaikenda.
➡️ TAARIFA za awali zinasema huenda wachezaji hao wakawa wamevuta hewa yenye sumu au kula chakula/kinywaji chenye sumu jana baada au kabla ya mchezo wa jana na TRA United.
➡️ Taarifa zaidi zitawajia kadiri tutakavyozipokea juu ya afya ya wachezaji hao.
𝗦𝗼𝘂𝗿𝗰𝗲: JEMEDARI SAID
08/05/2026
🚨ALLY KAMWEE AFUNGUKA
🗣️“Chama anajua Boli hata juzi nimchati nae nimempongeza amefunga goli zuri sana, japo mengine ni AI mnadanganywa”
🗣️“Clatous Chama ingekuwa Ulaya tungesema ni ‘world class’ utake usitake Chama anajua boli”
🗣️ Ahmed Ally Kombe lake ni la Mapinduzi na Muungano
08/05/2026
➡️ Ombi la kumtoa Kylian Mbappé ndani ya Real Madrid limesainiwa na watu wengi zaidi kuliko ombi lolote la haki za binadamu kuwahi kurekodiwa katika historia!
➡️ KARIBU WATU MILIONI 50 WAMESHALISAINI!
07/05/2026
Mashabiki wa klabu ya soka ya Young Africans sports club,Sasa wapo katika taharuki kubwa kufuatia majeraha aliyopata beki mwenye viwango vya juu ,yanayosababisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo kuyumba kwa kiasi.Nafasi Yake Sasa inashikikiwa na Frank Assinki ambaye ameonekana kuwa vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni lakini akiwa na makosa kadhaa yanayopelekea safu hiyo kukosa utulivu.
Mashabiki wa klabu hiyo,wanamuombea beki wao kipenzi Dickson Job arejee katika utimamu wa mwili ili kukamilisha na kuitumikia nembo ya klabu ya Yanga.
06/05/2026
Yanga imemfukuza Kocha Pedro ila scouting/Anayeamua Wachezaji wa Kusajiliwa naye ana shida sana.
Kina Ikangalombo, Ecua, Bubah wamefeli kwasababu Ni Wachezaji Wazuri kwenye Mechi za Counter attacks Hawawezi kupiga Chenga wakicheza Mechi na Timu inayojilinda.
Saivi nako inahusishwa na Huyu winger Ambaye ukiangalia Magoli yake Yote ni ya Kwa njia ya Transition/Counter Attack.
06/05/2026
Huyu Yao Kouas Atoula ni mchezaji ambaye kwa uchezaji wake anaonekana kuwa na mchango mkubwa sana uwanjani. Kila anapopewa nafasi, hujitahidi kutoa kila kitu katika kushambulia na pia kusaidia upande wa ulinzi kwa ufanisi mkubwa.
Kinachowashangaza mashabiki wengi ni namna ambavyo kocha anaonekana kumuamini zaidi Israel Mwenda, ilhali Yao akiwa uwanjani mara nyingi huonesha nidhamu, nguvu na uwezo wa kusaidia timu pande zote mbili za mchezo.
Kwa mtazamo wa baadhi ya mashabiki, Yao Kouas Atoula anaonekana kuwa na uthabiti na ubora wa juu zaidi, hasa kutokana na uwezo wake wa kuchangia mchezo wa kushambulia na pia kurudi kusaidia kukaba. Hii inafanya kuwepo kwa mjadala wa nani anastahili nafasi ya kuanza zaidi.
Kwa maoni yangu ya kawaida, Yao anaonesha potential kubwa na anaweza kuwa chaguo imara sana k**a ataendelea kupewa muda zaidi wa kucheza na kujiamini uwanjani.
06/05/2026
UPDATE
Mahusiano ya Célestin Ecua na wakala wake kutoka Morocco yamevunjika❌
Ecua na wakala wake wametofautiana pakubwa kiasi kwamba hakuna mawasiliano baina yao.
Ecua ni mchezaji wa Yanga ambae anacheza JS Kabylie kwa mkopo na mwishoni mwa msimu anatarajia kurejea Yanga.
06/05/2026
𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Klabu ya Simba SC kupitia Rais wao wa heshima, Mohammed Dewji wameanza mchakato wa kupata saini ya kiungo Feisal Salum (28) 🇹🇿 kutoka Azam FC kwa msimu ujao wa 2026-27
Kipengele cha Yanga SC kupewa Tshs BILIONI 1 kwa Feisal kinakwisha mwishoni mwa msimu huu .
06/05/2026
🚨 Ifikapo mwezi June mwaka huu Fiston Mayele atakwenda kuwa mchezaji huru na hii itakuwa ni baada ya kumaliza mkataba wake na Pyramids FC.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Misri inasemekana kuwa mchezaji huyo ananyatiwa kwa karibu mno na klabu ya Al Ahly SC..! 🇪🇬
Hata hivyo, kuongeza mkataba na klabu yake ya sasa, Pyramids FC, ndio chaguo analolipa kipaumbele zaidi kwa sasa.
Je, ni uamuzi gani utakuwa sahihi kwa Mayele katika msimu huu wa kiangazi…?! Kubakia Pyramids au kutimkia Al Ahly…?🤔🇨🇩
29/04/2026
Baada ya kuonekana kuwa kimya tangu alipoachana na Yanga msimu uliopita, ameweka wazi mipango yake ya kurejea dimbani msimu wa 2026-2027.
Mkude amebainisha kuwa msimu huu wa 2025-2026 ameamua kuupumzika uwanjani, lakini si kufanya mazoezi. Kiungo huyo anapiga tizi la nguvu gym, ufukweni, na kukimbia ili kulinda utimamu wake asianze upya atakaporejea.
🗣."Kufanya mazoezi nje ya timu inahitaji uvumilivu, lakini natambua kazi yangu inahitaji nini," amesema Mkude huku akificha jina la timu mpya atakayoitumikia msimu ujao.
28/04/2026
🚨_|| 𝗨𝗣𝗗𝗔𝗧𝗘𝗦:
Beki wa kushoto wa Young Africans 🇹🇿 Mohamed Hussein (Tshabalala) ataikosa mechi ya kesho ya Fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Simba Sc kutokana na majeraha yanayomkabili.