Yanga one's again

Yanga one's again

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Yanga one's again, Sports, Avic town, Dar es Salaam.

21/03/2024

Viongozi wa Klabu yetu hawana tamaa ya fedha, ndio maana tumepunguza na kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha wengi waje Uwanjani. Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa basi tunawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi. Kiasi cha fedha ambacho ungelipia tiketi ya mzunguko basi utatumia k**a nauli ya usafiri wa kukufikisha uwanjani na baada ya mchezo wetu uweze kurudi nyumbani salama" Ally kamwe.

Updates

21/03/2024

Kuna vitu vya kuvikomalia na kuna vingine vya kuacha vipite tu.

Bao la pili la Azam FC, ni offside ama si offside???

Majibu ya Frank Komba (Mwamuzi Msaidizi namba moja) si offside.....maamuzi yaliyomshawishi Heri Sassii kulikubali bao, kwa maana Sassii naye amekubali kuwa si offside.

Maamuzi ya Miguel Gamondi (Kocha Mkuu wa Yanga) ni offside (isivyo bahati Gamondi hana maamuzi ya kuamuru lolote kwa wachezaji 22)......!!!

So, Gamondi abaki na msimamo wake na akina Komba na wenzake wabaki na msimamo wao.

Huku kwetu sasa (mitandaoni) bado tunasaka kitu cha kuzima sakata la Prince Dube...tunalazimisha hilo bao liwe mjadala kitu ambacho hata tupate matokeo gani kwenye ajenda hii maamuzi yetu hayataathiri maamuzi ya Komba na Sassii kwenye Dar es Salaam Derby.

K**a tunaamua kulijadili hilo bao, tujadili kwa kufuata misingi.

✍️Nafasi aliyosimama Mwamuzi Msaidizi namba moja (Frank Komba) ilikuwa sahihi???

Yaan alikuwa sawa na mlinzi wa pili kutoka mwisho (second last defender). K**a jibu ni NDIYO, basi yuko sahihi 100% na k**a jibu ni HAPANA basi maamuzi yake yana utata, anaweza kuwa sahihi ama vinginevyo.

✍️Huo mstari uliochorwa, urefu kutoka mstari wa kati hadi mstari uliochorwa kule juu, je, ni sawa na urefu kutoka mstari wa kati hadi ulipochorwa???

K**a jibu ni NDIYO, basi hiyo ni onside, na k**a jibu ni HAPANA, basi itakuwa ni offside.

✍️Kwenye hiyo picha, mguu wa mtoa pasi umegusa mpira??

K**a jibu ni NDIYO, baada ya kupata NDIYO kwenye swali la kwanza na la pili, basi hiyo si offside kabisa, lakini k**a jibu ni HAPANA, hakuna namna ya kutetea bao la pili la Azam, kwa maana hiyo itakuwa ni clear offside.

NB:- kwa walioangalia kwa Tv, ni angles gani wamezitumia kugundua kuwa hilo bao ni offside???

Yaan kulikuwa na aina tofauti za angles kuonesha hilo bao lilivyotengenezwa hadi kufungwa?? Binafsi sijaona.

Halafu aliyelalamikia offside ni Kocha, ambaye hana dhamana yoyote ya kuwasiliana na Bodi ya Ligi kuhusu maamuzi, Viongozi wamekausha, maana yake hawapo pamoja naye katika hili.

Labda kwa kukubali kuwa ni bao halali, ama hawaoni impact hata wakilalamika.

Nafikiri tuheshimu mpira tu, kwamba Yanga wamepasuliwa na Azam basi, tusitafute vichaka.

30/11/2023

We Seleee mimba yako hiiiii

14/07/2022

Leo ndio atatambulishwa Azizi Ki
MPO TAYALI MSILALE WANANCHI

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Avic Town
Dar Es Salaam