Michael Noel

Michael Noel

Share

This page is personal, based on professional journalist

07/05/2025

KUKOPESHA WASANII WASIO NA ELIMU YA FEDHA SERIKALI IMEKOSEA- MUSUKUMA

Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Musukuma wakati akichangia kwenye bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekosoa kitendo cha serikali kupitia mfuko wa sanaa kukopesha mabilioni ya fedha wasanii ambao wengi wao wameshindwa kurejesha mikopo hiyo.

Amesema Wasanii wengi hawana elimu ya fedha, hivyo wengi wao wameitumia mikopo hiyo kununua magari ama kuoa na hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo ya mikopo waliyopewa.

Mbunge Msukuma amesema ni vyema mikopo hiyo ikatolewa kwa watayarishaji (producers) badala ya kukopesha wanaoonekana kwenye Tv (Luninga) kwa kuangalia mionekano yao (shape) kitendo kinachosababisha serikali kukosa marejesho ya mikopo hiyo.

07/05/2025

KISA DERBY MUSUKUMA ATAKA BODI YA LIGI IVUNJWE

Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Musukuma amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuja na Majibu yanayoeleweka kuhusiana na mvutano unaoendelea baina ya Klabu ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba sc baada ya kuahirishwa mchezo wa Watani wa Jadi Yanga sc vs Simba sc Machi 08 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam na Yanga sc kuweka msimamo wa kutocheza tarehe nyingine iliyopangwa.

Katika sehemu ya mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wakati wa wasilisho la Bajeti ya Wizara hiyo, Musukuma ameshauri iundwe bodi mpya ya ligi iliyo huru badala ya hii inayopokea maelekezo.

Nini maoni yako juu ya Mchango huu wa Msukuma? Tuandikie

07/05/2025

PROF KABUDI AOMBA BAJETI YA TSH BIL. 519,660,073,000

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia kwa Waziri wake Prof. Palamagamba Kabudi imeliomba Bunge kuridhia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 ikiwa na makadirio ya shilingi bilioni mia tano kumi na tisa milioni mia sita sitini na elfu sabini na tatu (519,660,073,000).

Bajeti ya wizara hiyo imesomwa leo Mei 07, 2025 na Waziri Prof. Kabudi Bungeni Jijini Dodoma.

04/11/2024

Early voting is coming to a close today in the United States as the nation gears up for election day tomorrow. Who is the most suitable candidate for enhancing Africa's diplomatic relations and development?

01/11/2024

KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED

Ni Ruben Amorin aliyekuwa akiinoa Sporting ya Ureno.

30/10/2024

UKIAMBIWA MWANAUME ATAKULA KWA JASHO NDIO HII SASA.

HT' Singida BS 0-0 Yanga sc.

28/10/2024

Asipopewa Ballon d'or itakuwa ni dhulma na ukatili.

Ni usiku wa Leo Paris Ufaransa. K**a watafanya uporaji na kumpa Rodri itakuwa ni anguko la hizi tuzo.

Photos from Michael Noel's post 27/10/2024

BOCCO, DILUNGA, NDEMLA WAJERUHIWA AJALINI

Basi la klabu ya JKT Tanzania limepata ajali leo eneo la Mbweni wakati kikosi kikirejea Dar es salaam kutoka mkoani Dodoma baada ya mchezo wa Jana dhidi ya Dodoma Jiji.

Taarifa iliyotokewa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Jemedari Said Kazumari imeeleza kuwa basi hilo lilikuwa likiendeswa na Capl Hassan Bakari ambapo liliacha njia na kutumbukia mtaroni.

Wachezaji waliopata maumivu kufuatia ajali hiyo ni John Bocco, Dany Lyanga, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Hassan Kapalata, Maka Edward, Mohamed Bakari, Hassan Machezo, Salum Gado na Gamba Matiko.

Wachezaji hao waliopata maumivu wapo chini ya uangalizi wa madaktari.

Mungu awaponye na kuwarejesha katika Afya yao ya kawaida waendelee na majukumu ya kuipambania timu yao.

Photos from Michael Noel's post 27/10/2024

REAL MADRID WALAANI VITENDO VYA KIBAGUZI

"Real Madrid inalaani vikali tabia yoyote inayohusisha ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni au vurugu katika soka na michezo, na inajutia sana matusi ambayo mashabiki wachache waliyatoa jana usiku kwenye moja ya kona za uwanja.

Klabu ya Real Madrid imefungua uchunguzi ili kuwasaka na kuwabaini wahusika wa matusi hayo ya kusikitisha ili hatua stahiki za kinidhamu na kimahak**a zichukuliwe"

Chapisho la Real Madrid kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya mchezo wa Jana dhidi ya Barcelona ambao Madrid walipigwa chuma nne wakiwa nyumbani huku baadhi ya mashabiki wake kwenye baadhi ya Kona za uwanja wakiwatupia maneno makali wachezaji wake kwa kuonesha kiwango dhaifu kwenye mchezo huo.

Photos from Michael Noel's post 20/10/2024

NGORONGORO HEROES MABINGWA CECAFA.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa Miaka 20 Maarufu Ngorongoro Heroes imeichapa Kenya mabao 2-1 na kutwaa Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U20) katika Fainali iliyopigwa uwanja wa KMC uliopo Mwenge Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.

Pamoja na matokeo hayo, Tanzania na Kenya zote zimefuzu kushiriki AFCON U20 2025.

19/10/2024

Hadi saa 1 jioni leo Msimamo huu wa Ligi utabadilika kidogo!

Je, Yanga sc kuishusha Simba sc au Simba sc kupanda juu zaidi kwenye msimamo?

Ni leo saa 11:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Simba sc vs Yanga sc.

18/10/2024

NGORONGORO HEROES HAOOOOO AFCON 2025

Timu ya Taifa ya Tanzania Vijana chini ya umri wa Miaka 20 maarufu k**a Ngorongoro Heroes imefuzu kushiriki mashindano ya AFCON yatakayofanyika 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa nusu Fainali dhidi ya Uganda Michezo ya mchujo wa kupata wawakilishi kutoka Ukanda wa CECAFA.

Bao la jioooooni dakika ya 119 kati ya dakika 120 katika uwanja wa KMC, limeiwezesha Ngorongoro kutinga Fainali hizo za Cecafa na kukata tiketi ya kushiriki AFCON 2025.

FT' Uganda 1-2 Tanzania U20

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


6404
Dar Es Salaam