Watani wa Jadi

Watani wa Jadi

Share

Official Page ya Watani wa Jadi. Habari zote Exclusive za Yanga na Simba utazipata hapa 24/7. Hii ni Official Page ya Watani wa Jadi kwenye Mtandao wa Facebook.

Habari zote Exclusive kutoka kwenye klabu za Yanga na Simba utazipata hapa muda wote 24/7
Habarika na Sisi

11/05/2026

Mashabiki na Wanachama wa Young Africans SC wameendelea kuonyesha mshik**ano mkubwa kwa klabu yao baada ya kuibuka na ombi la kuchangia fedha za kulipa faini ya Sh milioni 30 iliyotolewa na Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi.

Faini hiyo ilitokana na uamuzi wa Yanga kutotumia vyumba vya kubadilishia nguo katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC uliochezwa Mei 3 kwenye dimba la Isamuhyo.

Kufuatia mwitikio huo mkubwa kutoka kwa Wananchi, uongozi wa klabu umeweka wazi utaratibu rasmi utakaowawezesha wanachama na mashabiki kuguswa kuchangia fedha hizo kwa hiari.

Hatua hiyo imeendelea kuonyesha utamaduni wa mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa pamoja kila inapohitajika kuisaidia klabu yao katika nyakati mbalimbali.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

07/05/2026

Simba SC imeamua kubadili tena makazi yake ya mechi za nyumbani baada ya kutangaza rasmi kuachana kwa muda na Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kurejea katika dimba la KMC Complex walilotumia msimu uliopita.

Uamuzi huo umetangazwa kupitia taarifa rasmi ya klabu hiyo mapema leo, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni hali mbaya ya uwanja wa Isamuhyo kutokana na matumizi makubwa sambamba na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Mbali na Simba, uwanja huo pia unatumiwa na timu za JKT Tanzania pamoja na JKT Queens, jambo lililosababisha nyasi zake za asili kushindwa kuhimili ratiba ya mechi na mazoezi ya mara kwa mara.

Katika taarifa hiyo, Simba imeeleza kuwa mechi zote zilizobaki za nyumbani za Ligi Kuu NBC msimu wa 2025/2026 zitachezwa katika Uwanja wa KMC Complex hadi hapo hali ya uwanja wa Isamuhyo itakapotengemaa.

Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons unaotarajiwa kupigwa Jumapili Mei 10 utakuwa wa kwanza kwa Wekundu wa Msimbazi kurejea rasmi katika dimba hilo la KMC Complex.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

07/05/2026

Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, alilofunga kwenye Kariakoo Derby dhidi ya Yanga SC limeendelea kuteka mijadala mikubwa ndani na nje ya Tanzania, huku mashabiki wengi wakidai kuwa ni bao linalostahili kuwania tuzo ya FIFA Puskás ya goli bora la mwaka.

Katika derby hiyo iliyokuwa na presha na ushindani mkubwa, Chama aliandika historia kwa kufunga bao la kuvutia dakika ya nane, bao ambalo limewasisimua wadau wa soka kutokana na ubora wake wa kiufundi, ubunifu na umaliziaji wa kiwango cha juu.

Mitandao ya kijamii imefurika video na mijadala ya bao hilo, huku wachambuzi wa soka wakilitaja k**a moja ya magoli bora kuwahi kuonekana katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Wapo wanaoamini kuwa likipelekwa rasmi kwenye mchakato wa mapendekezo, linaweza kabisa kuingia kwenye ushindani wa tuzo ya Puskás.

Taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa Simba SC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa soka wanaendelea kufanya jitihada kuhakikisha bao hilo linafika kwa waandaaji wa tuzo hizo za kimataifa, wakati video yake ikiendelea kusambazwa na kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani.

Mchezo huo wa Kariakoo Derby ulihitimishwa kwa sare ya mabao 2-2, lakini bao la Chama limeonekana kuwa gumzo kubwa kuliko matokeo yenyewe.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

06/05/2026

Kuna nyakati soka huacha mashabiki na wachambuzi vinywa wazi na hii ni moja ya hizo. Licha ya kuiongoza Young Africans SC kileleni mwa msimamo wa ligi, kocha Pedro Gonçalves amejikuta akiondolewa madarakani katika uamuzi unaozua mjadala mpana.

Takwimu zake hazina utani: michezo 21, alikusanya pointi 51, akifunga mabao 47 huku akiruhusu mabao 5 pekee rekodi inayodhihirisha uimara wa safu ya ushambuliaji na ukuta thabiti wa ulinzi. Chini ya uongozi wake, Yanga haikuwa tu inashinda, bali ilikuwa inatawala mechi kwa namna ya kuaminika.

Lakini pamoja na mafanikio hayo yote, bado haikutosha kuokoa kibarua chake. Uamuzi huo unafichua sura halisi ya soka la kisasa mahali ambapo matokeo mazuri hayatoshi peke yake, na mara nyingi vigezo vya ndani ya klabu hubeba uzito mkubwa kuliko takwimu uwanjani.

Kuondoka kwa Gonçalves kunaacha maswali mengi hewani: Je, kulikuwa na mambo ya nje ya uwanja? Au matarajio yalikuwa makubwa zaidi ya kile alichowasilisha?

Hata hivyo, jambo moja linasalia wazi hii ni simulizi nyingine ya kushangaza katika dunia ya soka, ambapo hata ukiwa kileleni, bado unaweza kuanguka ghafla. “Crazy football,” k**a wengi wanavyosema.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

06/05/2026

Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imetangaza rasmi kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya kiufundi kuelekea hatua za mwisho za msimu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo, Yanga imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya tathmini ya ndani, huku ikitoa shukrani kwa kocha huyo kwa mchango wake ndani ya timu katika kipindi chote alichokuwa madarakani. Uongozi huo umesisitiza kuthamini juhudi na kazi aliyoifanya Gonçalves na kumtakia mafanikio mema katika safari yake ijayo ya ukocha.

Katika kipindi hiki cha mpito, majukumu ya kukinoa kikosi hicho yatasimamiwa na makocha wawili, Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi, ambao watashirikiana hadi mwisho wa msimu wa mashindano.

Hatua hiyo inaashiria mwanzo wa sura mpya ndani ya benchi la ufundi la Yanga, huku macho ya mashabiki yakielekezwa kuona namna timu hiyo itakavyojipanga katika mechi zilizosalia, ikilenga kumaliza msimu kwa mafanikio.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

06/05/2026

HEBU TUSAIDIANE KUJIBU SWALI

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

05/05/2026

Mjadala haujaisha—Mchome ameendelea kuishinikiza Kamati ya Saa 72 kutoa majibu ya kina, huku macho na masikio yote yakielekezwa kwenye uamuzi unaosubiriwa kuhusu tukio tata la Loemba dhidi ya Boka katika Dabi ya Kariakoo iliyomalizika kwa sare ya 2-2.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

05/05/2026

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, ameonyesha msimamo thabiti kuwa mbio za ubingwa bado hazijaisha, licha ya timu yake kuwa nyuma kwa alama tano dhidi ya vinara wa ligi, Yanga.

Barker ameweka wazi kuwa bado kuna alama 30 zipo mezani, hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha hawapotezi alama katika michezo iliyosalia.

“Bado tuna nafasi kubwa. Kuna alama 30 za kupigania, hivyo tunachotakiwa ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mchezo,” alisema Barker.

Akizungumzia maandalizi yao, alisisitiza kuwa watachukua kila mechi kwa uzito wake, wakianzia na mtihani ujao dhidi ya JKT Tanzania. “Tunaangazia mchezo mmoja baada ya mwingine. Kwa sasa akili zetu zote ziko kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania,” aliongeza.

Barker pia alikiri kuwa haitakuwa kazi rahisi, akieleza ubora wa wapinzani wao. “Ni mechi ngumu. JKT Tanzania wana kocha mzuri na wachezaji wanaopambana kwa nguvu, hivyo tunapaswa kuwa makini katika mbinu na mipango yetu,” alisisitiza.

Simba itashuka dimbani kesho Jumatano saa 12:15 jioni kumenyana na JKT Tanzania, ikiwa ni siku chache tangu wapambane na Yanga katika dabi iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

05/05/2026

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello, ameanza kuacha alama yake kwa kishindo baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi (NIC Player of the Month) kwa April 2026.

Okello ameibuka mshindi wa tuzo hiyo kufuatia kiwango chake cha juu uwanjani, akichangia moja kwa moja mafanikio ya timu kupitia mabao na pasi za mwisho zilizozaa magoli.

Hii ikiwa ni tuzo yake ya kwanza tangu atue Jangwani katika dirisha dogo la usajili, ishara tosha kwamba tayari ameanza kulipa imani ya benchi la ufundi na mashabiki wa klabu hiyo.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

04/05/2026

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2, mjadala umechukua sura mpya huku Mchome Mapovu akiibuka na maswali mazito yanayolenga Kamati ya Saa 72 chombo kinachosimamia tafsiri ya kanuni za ligi na utoaji wa adhabu kwa vilabu pamoja na waamuzi.

Je, hoja zake zina uzito unaostahili majibu ya kina, au ni kelele za kupuuzwa katika joto la ushindani?

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

03/05/2026

Beki wa kulia wa Young Africans SC, Israel Mwenda, ameonyesha ujasiri wa kuwajibika hadharani baada ya mchezo uliopita kutokwenda k**a alivyotarajia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwenda alikiri wazi kuwa hakuwa na siku nzuri uwanjani, akieleza kuwa makosa yake yaliigharimu timu na kuwaumiza wachezaji wenzake pamoja na mashabiki. Hakutafuta visingizio, bali alikubali lawama zote huku akiomba radhi kwa kile kilichotokea.

Aliweka wazi kuwa mashabiki hawakustahili kuona juhudi zao zikimalizika bila furaha, akiahidi kujifunza kutokana na makosa hayo na kurejea akiwa imara zaidi.

Kauli hiyo imepokelewa k**a ishara ya ukomavu na dhamira ya kupambana, huku ikionesha wazi kiu ya mchezaji huyo kurekebisha makosa na kurejesha imani ya Wananchi.

NB: USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YA WATANI WA JADI YOUTUBE
*********************************************

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Dar Es Salaam
255