25/07/2023
🕸..WATAALAMU WA SHERIA WANASEMA...
Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika
"Kanuni ya 62 (4) - Kanuni za Ligi Kuu, Toleo la mwaka 2022 inasema;
“Mchezaji wa kigeni anayeruhusiwa kusajiliwa kwenye Ligi Kuu ni yule anayecheza katika timu ya Taifa ya nchi yake au Ligi Kuu ya nchi husika.
Mchezaji kutoka Amerika ya kusini na Ulaya, lazima awe anacheza angalau kuanzia Ligi Daraja la Tatu (Kitaifa, kutegemea mfumo kwa nchi husika).
Mazingatio ya Daraja mchezaji analocheza kabla ya usajili wake kwenye Ligi ni kwa wakati husika au kipindi kisichozidi miezi sita tokea ameachana na timu yake ya mwisho kwa mchezaji aliye huru” Mwisho wa kunukuu..
Sasa k**a mchezaji katoka kwenye Ligi ya Mkoa au Ligi daraja la 4 huko Amerika ya kusini, usajili wake utakuaje hapa nchini? Naombeni kuelimishwa😎".
25/07/2023
DEAL DONE✅
KAZE ➡️➡️ NAMUNGO
23/07/2023
Emmanuel Mahop kwenye picha mbioni kujiunga na Yanga
Pichani ni katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya Cameroon
08/01/2023
Manchester United wameripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Cameroon, Vincent Aboubakar kwa mkopo.
United wako sokoni kutafuta mshambuliaji mpya wa kati baada ya kukatisha mkataba wa Cristiano Ronaldo mwishoni mwa mwezi uliopita, Aboubakar akihusishwa kuchukua nafasi hiyo.
Klabu ya Al-Nassr imeripotiwa kuvunja mkataba na mchezaji huyo raia wa Cameroon ili Cristiano Ronaldo aruhusiwe kucheza na kuingia katika orodha ya wachezaji wa klabu hiyo.
Aboubakar (37) aliwahi kucheza Porto na Besiktas, ametumia miezi 18 iliyopita na Al-Nassr na amefunga mabao 13 katika mechi 39 katika michuano yote, ikijumuisha mabao manne katika mechi 12 hadi sasa msimu huu.
03/01/2023
... 🚨 BREAKING
Klabu ya Simba imemuajiri aliyekuwa kocha wa klabu ya Vipers 🇺🇬, Robert Oliviera kuwa kocha wao mkuu hadi 2025.
Klabu ya Simba imeeleza kuwa, Juma Mgunda na Selemani Matola wataendelea kuwa makocha wasaidizi wa klabu hiyo.
25/12/2022
.... 🚨 Rasmi klabu ya Gwambina FC ya Mwanza imejiondoa Automatically kwenye ligi daraja la kwanza CHAMPIONSHIP baada ya kushindwa kutokea uwanjani katika mechi tatu tofauti za ligi hiyo mfululizo.
Mmiliki wa klabu hiyo, mbunge wa Misungwi Mwanza, Alexander Mnyeti aliilalamikia (TFF) kwa kuufungia uwanja wao na kuwapangia kiwanja kingine cha nyumbani ugenini akidai uwanja wao hauna tatizo lolote na kuwa gharama zinakuwa kubwa kwa wao muda wote kuishi ugenini.
Aliahidi ni bora ajitoe kwenye ligi, uwanja wake huo alioujenga kwa Billions of money AFUGIE KUKU.
KIKUNDI kimoja cha wavuta bangi kinataka kutuharibia mpira wetu TIFUTIFU Nyieeee 😥😢
21/12/2022
ThankYou Ahsante sana, Ibrahim Ajibu, kwa kuwa sehemu ya familia yetu.
✍️Mkono wa kwaheri kwa kiungo fundi Ibrahim Ajibu akiondoka Azam FC
Kila lakheri mwamba kwenye makazi yako mapya
Sayarimichezo_
18/12/2022
Msimamo wa Ligi Kuu ya National Bank of Commerce] 2022/23.
17/12/2022
INAUMA DAAH!!
✨Hakika amini Soka ni mchezo wa kupokezana vijiti ili maisha mengine yaendelee lazima umpe mwingine aendelee
✨Imetokea kwa kiungo mkongwe fundi wa mpira Mido ya boli Sergio Busquet ametangaza rasmi kuacha kuzea timu yake ya Taifa ya Hispain
✨Mawazo yake yamekuja Mala baada ya timu yake hiyo Taifa kutolewa katika hatua ya 16 bora katika michuano ya Kombe la dunia inayoendelea huko Qatar
Nilifurahi Sana nikikuona unavyoupiga mwingi pale Kati.. All the best Busquet 🙌🏿
17/12/2022
✍️ DEAL DONE!!
✨George Mpole rasmi ni mali ya St. Lupopo
✨Hii ni Mala baada ya kumwaga wino wa kukubali kujiunga na klabu hiyo yenye makazi yake huko Lubumbashi Congo
✨Rasmi atavuta mkwanja wa maana wenye thamani ya Tsh. M10+ yani na ushekhe.. na nyongeza ya mshahara
Hongera kwa uongozi wake na yeye mwenyewe binafsi, atuwakilishe vizuri kimataifa🙏
..
16/12/2022
IMESHINDIKANA
Dili la Cesar Manzok la kutua Simba SC lagonga mwamba
Mchezaji huyo amekataa ofaa ya Kuja kujumuika na timu ya msimbazi akiondoka na kutimkia zake China
Timu moja ya China imempa Mchezaji huyo mpunga wa maana ambao ni mkubwa kulinganisha na wa Simba SC
Simba atapindua Meza kumvuta Manzok toka kwa Wachina... STAY TUNED 📌