Muigizaji Filamu na Mshawishi wa Mitandao abaye ni Mpenzi wa Star wa Muziki Kutoka Tanzania akiwa kwenye Mashindano ya riadha Nchini Nigeria.
said_luambano
⛳️HEAD OF DIGITAL BONGOFM
⛳️ PRODUCER TBC
⛳️STORI ZA MASTAA 🇹🇿 🇰🇪🇺🇬🇺🇸🇮🇳
⛳️ FOLLOW MY PAGE
Mapokezi ya Staa wa Muziki Baada ya Kuwasili Nchini Kenya.
17/10/2025
Professa wa Boli amejiunga na Wananchi Mazoezini kwa ajili ya Mchezo wa ligi ya Mabingwa dhidi ya Silver Striker Nchini Malawi.
Umewahi Kumuona Kwenye tamthilia gani Bongo?
Muigizaji wa filamu Grace, Maarufu kwenye tamthilia ya SIKITU akipiga Ndizi Nyama, Vitu ambavyo huwa anavipenda 🙌
Muigizaji maarufu wa filamu, ZaiyLissa, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuchapisha picha mpya bila kuambatanisha maelezo yoyote, hatua iliyozua minong’ono miongoni mwa mashabiki wake. Wengi wameonekana kumpa pongezi wakimuita “Mrs. Side”, wakimaanisha kuwa ameolewa tena na mume wake wa sasa anayefahamika kwa jina la Side.Ikumbukwe kuwa mnamo Januari 24, 2024, ZaiyLissa alifunga ndoa na Haji Manara, lakini wawili hao walitengana Aprili 2025, baada ya ndoa yao kuvunjika. Hii ilikuwa ni baada ya kuvunjika pia kwa ndoa yake ya awali na Dulla Makabilla, iliyodumu kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja tu.Kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki wamekuwa wakimtania na wengine kumsifia kwa kile wanachokiita “nyota ya ndoa.” Hata hivyo, ZaiyLissa mwenyewe amewahi kueleza kuwa ameyasamehe na kuyaweka nyuma yote yaliyowahi kutokea katika maisha yake ya ndoa, na sasa anaendelea kujiweka katika hali ya amani huku akijitafutia riziki.Ameongeza kuwa anaomba hii iwe ndoa yake ya mwisho, na amejikita zaidi katika maisha mapya yenye matumaini na utulivu.
Kila mtu ameachia Wimbo, Utaenda kwa nani?
16/10/2025
Mchezaji wa klabu ya Young Africans (Yanga SC) na timu ya taifa ya Ivory Coast, Pacom Zouzoua, ametoa shukrani za dhati kwa mashabiki wake wote waliomuunga mkono wakati wa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliofanyika katika uwanja wa Ébimpé nchini Ivory Coast.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zouzoua aliandika:
“Ningependa kutoa shukrani kutoka moyoni mwangu kwa watu wote waliokuja kuniunga mkono wakati wa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Ivory Coast katika uwanja wa Ébimpé. Shukrani kubwa kwa vilabu vyangu vya mashabiki vya Azaguié, Bagnon, na hasa mashabiki wa Yanga (Wananchi), pamoja na majirani zangu na bila kusahau familia yangu kwa uwepo na moyo wa kunitia moyo.”
Ujumbe huo umevuta hisia za mashabiki wengi wa Yanga na wapenzi wa soka barani Afrika, wakionyesha furaha na fahari kwa mchezaji huyo ambaye amekuwa tegemeo muhimu katika safu ya kiungo cha Yanga na pia anaiwakilisha nchi yake kwa mafanikio makubwa.
Zouzoua amekuwa akitamba na klabu ya Yanga kwa muda sasa, akijizolea umaarufu kwa uwezo wake mkubwa wa kucheza, nidhamu na kujituma ndani ya uwanja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amewataka mashabiki wa michezo kuendelea kuenzi na kudumisha amani, akisema ni nguzo muhimu inayovutia wawekezaji katika sekta ya uchumi na michezo nchini, hivyo kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mhe. Chalamila pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuipa sapoti timu ya Dar City FC inayoshiriki michuano ya kimataifa ya mpira wa kikapu ya Road to BAL, itakayofanyika kuanzia kesho katika uwanja wa IST.Amesisitiza kuwa mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao wala mali zao wakati wa kufuatilia michezo hiyo, kwani maandalizi yote yamekamilika kwa kuhakikisha hali ya utulivu inatawala kipindi chote cha mashindano.
Baadhi ya wananchi wa Kenya waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuupokea mwili wa Hayati Raila Odinga walijawa na hisia kali za majonzi na upendo kwa kiongozi huyo.Wakiwa wamebeba huzuni isiyoelezeka, baadhi yao walionekana wakifuta vumbi kwenye ndege maalum iliyobeba mwili wa “Baba ”, k**a ishara ya heshima, kuaga na kumtakia safari njema ya mwisho.Wengine walitumia mikono yao, wengine wakikata matawi ya miti na kuyatumia kwa unyenyekevu kuisafisha ndege hiyo, tukio lililozua hisia nzito na kuashiria namna Raila alivyogusa mioyo ya Wakenya wengi.Hali ya ukimya na vilio ilitanda uwanjani, huku umati mkubwa ukishuhudia kwa machozi kumbukumbu ya mwisho ya kiongozi aliyependwa na wengi.
Ila Wakenya 🙌
Gavana wa Kaunti ya Mombasa, Abdulswamad Sharif Nassir, alishindwa kujizuia machozi aliposhuhudia mwili wa Hayati Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, ukishushwa kutoka kwenye ndege maalum katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi.Katika tukio hilo lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi, viongozi wa serikali, na wanasiasa wa vyama mbalimbali, jeneza lililofunikwa kwa bendera ya taifa lilishushwa kwa heshima na maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), huku ukumbi mzima ukitawaliwa na ukimya mzito wa majonzi.Gavana Abdulswamad alionekana akibubujikwa na machozi, akifuta uso wake mara kwa mara huku akishika kifua kana kwamba akihisi uchungu wa kumpoteza mtu aliyemchukulia k**a mlezi na kiongozi wa kizazi chake.Taswira hiyo ya huzuni iliwagusa wengi waliokuwa wamefurika uwanjani, wakitazama kwa majonzi tukio hilo lililojaa heshima na hisia kali. Wengi walitafakari pengo kubwa lililoachwa na Raila Odinga — mwanasiasa ambaye kwa miongo kadhaa alisimama k**a sauti ya haki, demokrasia na matumaini kwa mamilioni ya Wakenya.Tukio hilo lilithibitisha kwa mara nyingine kwamba Raila hakuwa tu mwanasiasa, bali alikuwa alama ya umoja, ujasiri na mapambano yasiyokoma kwa ajili ya taifa la Kenya.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Website
Address
Dar Es Salaam