Elcapitano Maestro

Elcapitano Maestro

Share

1️⃣. Sports Pundit (English & Swahili) 2️⃣. i'm the best football analyst in africa

12/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣Ousmane Dembélé amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu 2025-26 wa Ligue 1

Alianza mechi 9 pekee na mechi 11 akianza kwa kutokea benchi hivyo ameonekana uwanjani kwa jumla ya michezo 20 huku akifunga mabao 10 na kutoa pass za mabao 6 na alikuwa nyota wa mchezo mara 4.

Ousmane Dembélé amecheza mechi 20 na bado ndie mchezaji aliefanya vizuri zaidi kwa Ligue 1 ukiwalinganisha na wachezaji wenzake wa PSG.

💁🏾‍♂️

11/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

JIFUNZE...👇

Elcapitano Maestro 🗣 kuna mambo sita (6) ambayo ni hatari zaidi kwenye ligi ya epl...

na miongoni mwa jambo hatari zaidi kwa Epl ni pale ambapo timu kubwa inapotaka kurejesha makali yake kisha ikamchukua kocha ambae mwenye CV ya kawaida halafu kuweka imani nae kuwa atafanya makubwa.

Ligi ya Epl ligi yenye presha kubwa inahitaji kocha ambae anajua kutafuta alama hata akiwa kwenye presha kubwa.

Liverpool wakati wanatafuta kurudi kwenye ubora walimpata klopp ambae tayari alikuwa na CV nzuri na alishaonekana yeye ni kocha wa aina gani, the reds walimpa muda na akafanya makubwa.

Man United walimpata Mourinho na matumaini ya United kurudi katika ubora yalikuwa makubwa sana na hata hivyo vikombe alibeba.

lakini pale ambapo Mourinho alipotaka nafasi kubwa zaidi ndani ya klabu hilo lilikuwa tatizo nae akatimuliwa.

Chelsea walimpata Thomas Tuchel ambae alikuwa na CV nzuri alifanya makubwa kwa muda wake lakini hakuwa na wasaa wa kuijenga chelsea iliyokuwa bora..

Man City wao ndio funga kazi walijua kabisa namna ambavyo epl ni nini inahitaji, walimchukua Guardiola kisha na kumpa nafasi kubwa ndani ya klabu na hatimae hivi sasa City ni moja ya klabu kubwa zaidi epl.

🗣hivi sasa naiona chelsea ipo katika kitendawili kigumu juu ya nani awe kocha wa chelsea, lakini ikiwa watataka wawe bora kwa msimu ujao ni LAZIMA wahakikishe kwanza wanampata kocha mwenye CV nzuri.

hata kwa man united ikiwa itahitaji kufanya vizuri zaidi kwa msimu ujao bado itahitaji kocha mwenye CV nzuri.

Arsenal waliamua kupita njia tofauti waliamua kuanza na arteta ambae hakuwa na uzoefu wowote walimpa muda sana na sasa uzoefu anao kwenye makombe ya ndani na hata kwa makombe ya nje.

sitoshangaa kuona arteta akirudi man city k**a kocha mkuu kwasababu city ni mabingwa wa kusoma alama za nyakati.

Usisahau kwamba bila ya uwepo wa guardiola, mikel arteta angekuwa tayari ashabeba ubingwa wa epl.

💁🏾‍♂️

Photos from Elcapitano Maestro's post 11/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 msimu huu 2025-26 kuna mechi 7 ambazo Arsenal wameshinda 1-0 kwa kweli David Raya kuna namna ameipambania tuzo yake ya Golden Gloves.

Kuna mechi nyingi uwepo wa Raya langoni umesababisha arsenal kuondoka na alama zote tatu.

Pengine huyu ndie mchezaji bora zaidi kwa Arsenal msimu huu ambae anaweza kuanza timu yoyote ile duniani.

2019...wakati arteta anamsaini kocha wa makipa wa brentford(inak cana pavon) baada ya miaka minne alimuomba arteta aweze kumsaini raya na sasa raya ameshinda tuzo ya golikipa bora mara 3 mfululizo 😀.

💁🏾‍♂️

10/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 kila mtu ashinde mechi zake, na msisahau kwamba wakati ligi inaanza nilisema kwamba bingwa wa msimu huu 2025-26 atakuwa ni Arsenal.

ikiwa arsenal haitashindwa ubingwa msimu huu ndio itakuwa kwa mara ya kwanza nitabiri bingwa halafu asibebe ubingwa.

💁🏾‍♂️

09/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 Manchester United imesitisha uhamisho wa kiungo wa Chelsea Cole Palmer, ikiamini vipaumbele vyao vya uhamisho viko kwingineko msimu huu wa joto.

Chanzo: Mirror Football

🗣 Lavia na Santos bado si viungo ambao wanastahili kuanza kikosi cha kwanza cha chelsea.

vile vile enzo fernandez, caicedo na palmer hawawezi kuifanya safu ya kiungo kuwa imara.

Palmer anakuwa bora ikiwa atatoa mchango mdogo wa ki-ulinzi.

Chelsea wakiwa na uwezo wa kumpata Caicedo mwingine watarahisisha kazi kubwa sana katika safu ya kiungo, hio itakuwa sababu pia ya kurudisha ubora wa palmer akitokea pembeni.

Moja ya namba ngumu zaidi kuicheza uwanjani ni eneo la namba 8 na ndomana kuna timu zinacheza huku zikiwa na namba 8 wawili kiwanjani ili timu iwe na balance na uhakika wa kuanzisha mchakato wa kutengeneza nafasi.

💁🏾‍♂️

09/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Jose Mourinho 🗣 ikiwa Real Madrid itataka kurejea kushinda mataji ya ligi, lazima wawe na nguvu zaidi nyuma.

timu kwa sasa haina usawa katika eneo la ulinzi na ninataka kuwaleta wachezaji wa chaguo lake ili kurejesha utulivu na muundo kwenye safu ya ulinzi.

nb: timu yenye safu imara ya ulinzi ndio inaweza kubeba makombe hata arsenal akitaka ubingwa wa UEFA ni lazima awe bora katika ulinzi dhidi ya PSG.

💁🏾‍♂️

07/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Mwandishi 🗣 Je, unazizungumziaje mbinu zako baada ya kutinga fainali kwa mara ya pili mfululizo...?

Luis Enrique 🗣"Sina nia ya kuelezea mbinu zangu, kwa sababu hutaweza kuzielewa"

💁🏾‍♂️

07/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Mchambuzi wa michezo wa Ufaransa Walid Acherchour 🇫🇷 🗣"Khvicha Kvaratskhelia anastahili Ballon d'Or kwa sasa. Lakini hatastahili kwa sababu yeye ni Mjojia.

Georgia haitashiriki Kombe la Dunia la FIFA mwaka huu, na kutokuwepo kwa Kvaratskhelia ndio mwisho wa bahati mbaya yake 🇬🇪.

💁🏾‍♂️

07/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 Luis Enrique alimtoa Ousmane Dembélé, mmiliki wa Ballon d'Or, dakika ya 66… na hakukuwa na malalamiko hata kidogo baina yao.

Kulikuwa hakuna kuchanganyikiwa, hakuna drama, hakuna mtazamo hasi, bali dembele alimsalimia kocha wake kwa mkono na kukaa kwenye benchi bila kusema neno.

Na hivi ndivyo imani kwa meneja inavyoonekana kubwa sana kwa wachezaji wake, sasa fikiria Vini Jr au Mbappé katika hali hii hii 😀.

nb: wachezaji wote wa PSG wameungana kwa ajiri ya kupambania falsafa za kocha wao na wana muamini kuliko kitu chochote.

hata mikel arteta wachezaji wake wana muamini sana na ndomana tumeweza kuiona arsenal ya tofauti sana.

bahati mbaya...👇

wakati ambao PSG anaisubiri fainali huku arsenal ana kibarua kizito cha kumaliza ligi ambayo aliianza vizuri.

Psg watapata wasaa mzuri sana wa kuisoma arsenal na kujua ni vipi wataicheza mechi yao.

ipo hivi...👇

mechi ya fainali huamuliwa na mbinu pamoja na utimamu wa kimwili kuelekea katika mchezo huo.

ukitaka kujua ni kwa kiasi gani arsenal wanaandaa utimamu wao wa kimwili kuelekea fainali ni pale ambapo arsenal atapata matokeo mapema katika mechi zake tatu zilizosalia za ligi kuu 😀.

💁🏾‍♂️

07/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 Michael Olise ndoto za kushinda ballon dor zimezimika tayari 😒 wakati dunia ilikuwa inasubiri maajabu ya olise lakini Luis Enrique aliamua kuimaliza mechi kwa mbinu kali...

niliwaambia kwamba Vicent Kompany hana mbinu za kumtoa kwenye mashindano Luis Enrique.

ili uwe bingwa wa Uefa inabidi timu yako iwe na uwezo wa kupata matokeo hata ukiwa unacheza kwa presha ya namna gani.

Vicent Kompany timu yake bado haijakamilika kwa mbinu ndomana nilisema mapema sana kuwa bayern munich hatoweza kushinda uefa champions league.

naamini sasa Kompany atakuwa amepata darasa huru katika njia ya kuumiza sana lakini huo ndio mpira 😀.

💁🏾‍♂️

06/05/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

PSG AMETINGA FAINALI BAADA YA KUMTOA BAYERN MUNICH...

Elcapitano Maestro 🗣 pengine huenda baadhi yenu ukawa ni ukweli mchungu zaidi kwenu lakini ukweli ni kwamba mimi ndie mchambuzi bora zaidi wa soka barani afrika...

hizi darasa zilifaa ziende mbali zaidi, japo kuna media zilitaka nifanye nazo kazi lakini niliwaambia wazi I'm more expensive one.

fanyeni promo za kutosha 😀 ili nianze kuchambua mechi kabla k**a zamani maana naamini watu wa mikeka nitaokoa maisha yenu

sasa ipo hivi...👇

niliwaambia Vicent Kompany hana mbinu za kumtoa nje ya mashindano Luis Enrique mbali na hilo nilisema PSG ndie atakuwa bingwa msimu huu 2025-26 nilisema sana juu ya hili, mpaka wengine mkawa mnasema mimi ni team PSG ee ni kweli, napenda kujifunza kutoka Luis Enrique.

nilisema pia Bayern Munich HANA timu ya kuchukua UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwasababu ili uwe bingwa lazima uwe na mbinu sio kuwa na washambuliaji wakali tu usishangae ndomana arsenal unamuona fainali.

wengi wenu mlibisha sana lakini uzuri huwa sifuti post ili vizazi vijavyo vije kuona andika la mchambuzi bora zaidi wa soka barani Afrika.

sasa ni fainali ya PSG dhidi ya Arsenal na ndio fainali ambayo nilikuwa naisubiri na huenda labda ikakuuma lakini hizo ndizo timu bora zaidi kwasasa.

Niwakumbushe tu mechi ya fainali nitaenda kuishuhudia LIVE... usikute mimi Elcapitano Maestro AI nilieamua kutengeza account 😀 kwani unajua mimi ni nani...?

💁🏾‍♂️

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam