20/04/2023
π¨βͺοΈ | ππππππ: Toni Kroos new deal
Understand Toni Kroos has already signed a new deal with Real Madrid β itβs here we go confirmed ππ©πͺ
β New deal will be valid until June 2024 as expected.
β Kroos never negotiated with any other club as he just wants and hopes to retire at Real Madrid one day.
β Official announcement pending, timing up to Real Madrid β same as for VinΓcius and Karim Benzema.
18/04/2023
Kuna vijana wengi kwenye mihangaiko yetu ya kila siku, wapo ambao tunafahamu wana ndugu wenye mali na pesa nyingi na sio kwamba hawapendi kuomba msaada.
Siku moja huko nyuma nikiwa bado sijaanza utafutaji nakumbuka nilikaa na mzee moja mwenye busara sana (Apumzike kwa amani) akaniambia "Mwanangu kinyume cha msaada ni kusimangwa, penda sana kutafuta chako"
Now days vijana tumeamua kuondoka mbali na familia zetu, kuacha watu tunaowapenda na kwenda sehemu za mbali ambazo hatukuwahi kuwaza huko zamani kwa lengo la utafutaji wa maisha kwa njia halali.
Watu hupenda kutafuta kwa jasho, kula vyao wakiwa na amani moyoni. Let's go kijana mwenzangu huenda leo ni zamu yetu
22/03/2023
Sisi tunatoka Tanzania! Tunatoka vijijini na mjini hatuna tofauti ya kimaisha, tunaishi kawaida wengi kati yetu wamekosa uhakika na kesho! Kuamka na kiporo asubuhi kwetu ni tendo jema mfano wa Simione Petro kutupa nyavu kwa amri ya Yesu kristo, hatuwazi baga na pizza vichwani mwetu, hayo sio maisha yetu.
Tukiumwa hatuitiwi daktari nyumbani, unafunikwa kitambaa chenye maji kwny paji la uso! Pain killer kupooza maumivu na shuka mbili kupunguza baridi sambamba na dua nene unipone haraka kwa uwezo wa Mungu baba.
Nyuma tulipoteza ndugu na jamaa zetu kwa homa kali, Maralia na mimba, kijiji kilikosa hospitali ya karibu na hata walio mjini walikosa hela ya kumuona mtaalamu na kuishia kwenye foleni. Sad story
Mama mjamzito alipaswa aende km 10+ kila wiki kufata kituo cha afya kujua maendeleo ya mtoto tumboni! Huko ndio tulipo ata yule kiongozi aliyetuahidi mabomba ya maji safi na nguzo za umeme hatujamuona toka uchaguzi
Nani abebe shida zao..? Ajitokeze mwenye huruma asaidie wadogo zetu hawaendi shule kisa umbali, mwenyekiti wa kijiji agongi mhuri bila cha juu upigaji ndio jadi yetu hasa kwa mwenye dhamana.
Dc nipeleke wapi vilio vyao..? Njooni mjionee kwa macho vijana hawana ajira licha ya kusoma hadi vyuo na mmesema wajiajiri, kubeti ndio kazi yao na bado wakiwin mikeka mnachukua 18% k**a kodi
By mkwel ally
12/03/2023
Baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Afrika Kusini imeripoti kuwa Rapa kutokea nchini Afrika Kusini Costa Tsobanoglou maarufu Costa Titch, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka jukwaani wakati akitumbuiza.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Costa Titch amefariki dunia usiku wa kuamkia leo alipokuwa akitumbuiza jukwaani Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini baada ya kuanguka ghafla akiwa jukwaani ambapo taarifa hizo zinadai Msanii huyo alikuwa na historia ya ugonjwa wa Kifafa.
Japokuwa taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi na Familia au Mamlaka za Afrika Kusini, Watu maarufu wa Afrika Kusini akiwemo Mwanasiasa maarufu Afrika Kusini na Mbunge kupitia Chama cha EFF nchini humo, Julius Malema bila kutoa maelezo zaidi ameonesha kuwa katika majonzi kupitia ukurasa wake wa Twitter, ukurasa rasmi wa Twitter wa Sound City pia umethibitisha kifo hicho huku nchini Tanzania pia Wasanii Ommy Dimpoz, Nandy, Mbosso na wengine wakionesha masikitiko yao mtandaoni kufuatia kifo hicho.
Costa Titch amewahi kufanya kazi na Wasanii wa Tanzania ambao ni Diamond Platnumz aliyeshirikiana nae kwenye wimbo wa "Superstar" ulioachiwa October 2022, pia ameshirikishwa na Mbosso kwenye wimbo wa Moyo ulioachiwa miezi saba iliyopita.
08/02/2023
Jioni nyingine tena yenye majonzi na uchungu bado riziki ni mtihani upande wetu, Siku ndio tofauti ila bado maumivu ni yale yale ya jana. Waliofanikiwa wanasisitiza tuendelee ku-trust the process licha ya muda kusogea lkn mipango yetu imebaki pale pale.
Pasi ndefu tuliyopiga jana ndio tumepiga na leo hakuna anayejali kuhusu sisi. Kauli iliyojaa ubinafsi "vijana hawapambani" hawakumbuki asubuhi tumewahi kabla ya kufungua ofisi zao amna tulichoambulia zaidi ya secretary kusema "Boss kasafiri" rudi baada ya wiki tatu.
Itazame mitaa tunayotoka, zitazame ndoto tunazoota, tazama mapambano ya vijana wengi usiache kuangalia na changamoto wanazo pitia kila kukicha afadhali ya jana
Walioshika System hawaamini kwenye kusafisha njia watu wapite wanaforce story zetu na zao zifanane ata k**a hakuna ugumu wataweka ugumu
Tuishi vizuri isije tokea siku ukamuomba uliyemnyima
ONE DAY WE WILL MAKE IT
28/01/2023
MABADIRIKO.
"Kuna muda unapambana sana kufikia malengo lakini hufanikiwi, vikwazo na changamoto huzidi nguvu yako ya msukumo na kujikuta ukikata tamaa. Rafiki kuna kitu kidogo naomba nikukumbushe,
ππ½ dakika hubadirika na kufanya masaa yasonge.
ππ½Jua huzunguka dunia na kufanya usiku na mchana.
ππ½ vivyo hivyo hata siku pia hazigandi, ndio maana tarehe hubadirika, wiki hutimia, miezi kusonga na baada miaka kupita.
Kidogo sasa najua utakuwa umetambua namaanisha nini, yaani ukikwama kuyafikia mafanikio haimaanishi ukate tamaa lah! Sha. Jaribu tena na k**a bado kila ujaribupo mbombo inazidi kuwa ng'afu, badirika wewe using'ang'anie kukibadirisha kisichobadirika. Usijari watasema nini, wapuuze wanao amini huwezi. KUMBUKA, kuna njia mbili ndefu na fupi na zote zinaitwa njia. Hivyo chagua njia ya kupita usisimame, kwakuwa utapotea wakati wa kwenda kurudi mwenyeji. Badirika mabadiriko yanavyotaka kukubadirisha ili ufanikiwe".
19/01/2023
Kuna wakati mambo yanaenda vizuri upande wako kila unachogusa ni uhakika mpaka unajihisi ni mbarikiwa k**a Yakobo mwana wa Isaka
Alafu upo ule wakati kila kitu kwako ni mtihani 1 haikai wala 2 haifai! Kazini matatizo, mahusiano hayaeleweki, ndugu wanaleta noma, watu unao amini ni msaada hawapokei simu wala kujibu text mpk unadhani duniani umekuja kuteseka
Ugumu wa maisha ndio kitu pekee kinachofanya watu wengine waishi, yupo ambae hajui atakula nn lkn yupo mtu anakula na kusaza kinabaki anamwanga, maana halisi ya Tuishi
Bahati mbaya sana tunaogopa nyakati ngumu kuliko kitu chochote, tunasahau hiki ni kipimo cha ukomavu, imani ya ushindi ikawe na ww k**a vile Mfalme Daudi dhidi ya Goliathi, Daniel dhidi ya simba wenye njaa kali au Shadraka, Meshaki na Abednego katika tanuru la moto mkali
Believe Yourself, Fanya kazi kwa bidii, usitamani cha mwingine, subiri wakati wako wa baraka ukufikie hayupo ambae Mungu amemsahau kila mmoja wetu anakusudio la kuwepo hapo alipo
We'll overcome more than overcome in him who strengthens us
Mkweli Alcantara noted by
30/12/2022
RIP to the iconic Pele. ποΈ
Football will miss youπ
29/12/2022
Leo nataka niwakumbushe msemo wa mwanafalsafa mmoja unasema "A good man is hard to find because he is working somewhere" Yaani mwanaume bora ni ngumu kumpata kwakuwa yupo mahali anapigania mkate wake.
Mzee mmoja ananikumbusha "Mwanangu maisha hujayajua, naweza kutafuta elfu kumi mwanangu avae na mama ake atamwambia nguo hii nmekununulia, nanyi mnatoka mbele mnasema hakuna k**a mama sisemi hawana thamani ila wasikilizeni kwa akili... Mzee anaondoka na kuniacha nikifikiri kwa kina
Kuna vijana wana mahusiano yao hii leo yameteketea kutokana na harakati zao za maisha, Atabeba zege ili alipe kodi bado mke hatajali
Atabeba mchanga ili familia yake ile na atazibua vyoo ili mkewe avae vizuri k**a wanawake wengine ila bado kuna mtu anatokea anamchukulia mke wake inaumiza sana
Kumbe leo Boxng Day na Premier League inarudi
...Tuishi na Tuwemo