29/08/2026
Klabu ya Simba SC imethibitisha rasmi kuachana na kiungo wao wa kati, Allasane Kante, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji waliotamba na kikosi hicho katika msimu uliopita.
Kante amehitimisha maisha yake ya Msimbazi baada ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja tu.
Weka comment hapa chini...
29/08/2026
Kikosi cha Yanga kimewasili Arusha tayari kuwavaa Fountain Gate kwenye mchezo wa tano wa ligi kuu ya NBC .
Yanga wametoka kushinda mchezo wao wamwisho dhidi ya Pambi Jiji ,wakati wa Fountain Gate ametoka kupoteza mchezo wao wamwisho dhidi ya Mbeya City.
29/08/2026
Baada ya Cristiano Ronaldo kufanikiwa kufunga bao (1) kwenye ushindi wa mabao (2-1) ambao Al Nassr wameupata dhidi ya Al Taawoun bao hilo limemfanya CR7 kufikisha idadi ya mabao (978) hivyo anadaiwa mabao (22) pekee ili kufikisha jumla ya mabao (1,000).
Aidha, tangu atue ndani ya Ligi ya Saudi Pro League Ronaldo ameitumikia Al Nassr kwenye michezo (109) huku akihusika kwenye jumla ya mabao (122) akifunga mabao (104) na kutoa Assisti (18).
NB.Baada ya Cristiano Ronaldo kufunga goli mchezaji Sadio Mane pamoja na wenzake likiwemo benchi la ufundi, walibidi wamkumbushe kuwa wamesahau kushangilia kwa mtindo wake wa "Siuuuu".
Yapi maoni yako....?
29/08/2026
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, amesema bado hajaridhishwa na idadi ya mabao ambayo timu yake imefunga katika michezo minne ya mwanzo.
Manqoba amesema Yanga imefunga mabao 13 katika michezo minne, lakini anaamini kiwango hicho hakitoshelezi kulingana na matarajio yake.
“Ninafuraha tu kwasababu najua ipo siku kuna mtu tutamfunga goli nyingi na itakuwa sio sawa kwake, lakini ndio mpira.”
-Haya ni maneno ya Kocha ya klabu ya Yanga Manqoba baada ya mchezo wa jana dhidi ya Pamba Jiji .
Nani unaona ??
29/08/2026
Nyota wa zamani wa klabu ya Man city ambaye yupo ndani ya klabu ya Napoli, Kevin De Bruyne . Alitoa kauli mmoja baada ya timu yake ya Napoli kuwe kwenye kundi mmoja na klabu yake zamani Manchester City kwenye michuano ya Uefa Champions league.
Kevin De Bruyne alieleza kuwa "hapendi kucheza dhidi ya Manchester City kwani klabu hiyo itasalia kuwa yake ya asili kutokana na miaka kumi aliyodumu huko na mataji waliyoshinda pamoja"
-Alisema Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester City Kevin De Bruyne.
29/08/2026
Beki wa kushoto wa klabu ya Simba SC, Nickson Kibabage, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua mwezi mmoja kutokana na majeraha.
Taarifa zinaeleza kuwa Kibabage alipata majeraha wakati wa mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo dhidi ya Pamba Jiji, hali iliyomfanya akose mchezo huo.
Kibabage sasa anaingia kwenye orodha ya wachezaji wa Simba wanaosumbuliwa na majeraha, huku akitarajiwa kutumia kipindi hicho kwa ajili ya matibabu na kurejea katika hali nzuri ya ushindani.
Uwenda hili ni pego kwa Simba .... Yapi maoni yako?