FANS of SIMBA SC

FANS of SIMBA SC

Share

PATA HABARI ZOTE KUHUSU KLABU YA SIMBA SC HAPA. KWA MAONI ZAIDI NITUMIE SMS. INBOX NAMI NTAKUJIBU ASANTE.

13/04/2025

TETESI
Kutoka kwa Micky Jr amesema Kuna uwezekano mechi ya nusu fainali ya kombe la shirikisho la CAF kupigwa Amani complex Zanzibar

12/04/2025

KUTOKA SIMBA SC WAMEPOST HILO GARI
sijui wanamaana gani,Mimi sijui K**a kuna mtu anajua atuambie

12/04/2025

MWAMBA BADO YUKO SANA SIMBA SC
Leo katika mazoezi ya Simba sc pale kmc complex alionekana golikipa wa zamani wa Simba sc Ayoub Rakrad.
Kumbuka kuwa Ayoub alisitishiwa mkataba wake na Simba sc katika dirisha dogo na nafasi yake kuchukuliwa na ELIE MPANZU.
Haijafahamika Mara moja juu ya uwepo wake pale Simba kuwa anafanya mazoezi ili kuweka mwili sawa au walipo mwacha hakupata timu kutokana na majeraha aliyokuwa nayo na Sasa yuko fiti na anasubili msimu ujao?
TUTAWAAMBIA LET'S WAIT AND SEE

12/04/2025

SIMBA SC TO AMANI COMPLEX?

Wakati zimebaki siku nane kabla ya Simba sc kuwavaa Stellenbosch ya afrika kusini,mpaka Leo hakuna tamko lolote la klabu ya Simba sc kuhusu mechi hii itachezwa wapi!

Aidha itachezwa Benjamin mkapa au amani Zanzibar,kumbuka kuwa wenye uwanja wao wa Benjamin mkapa wameshatoa tamko kuwa wameufungia uwanja huo.
Kwa hiyo K**a mechi itachezwa nje ya dar es salaam ni wakati mzuri kwa viongozi wa Simba sc nao kutoa tamko kuwa mechi yetu itachezwa wapi aidha dar au Zanzibar ili walio mbali waanze kujipanga mapema

Kumbuka mda haumwachi mtu
Hayo ni yangu maoni.

10/04/2025

SERGIO BUSQUETS WA BONGO

Uimara wa Mpanzu kufunga magoli na kutoa assists?,Jean Charles Ahoua na magoli ya free kicks? , Ateba na magoli ya penalty? Mukwala kucheza dakika chache na kufunga magoli mengi? Yes ndio kitu kikubwa kinachoonekana kwa urahisi kwa watu wengi.

Sio mbaya kwasababu Dunia ya mpira inaamini zaidi ubora wa mchezaji ni kufunga magoli na kutengeneza magoli.

Ila kabla ya magoli kufungwa ama baada ya kufungwa nani anapaswa kuzuia vizuri kuipa faida timu?

Hapa ndio eneo nyeti zaidi kwasababu ukuta mgumu utakupa mataji,ukuta mwepesi utawapa washambuliaji kazi kubwa kufunga magoli mawili wao kuruhusu matatu haina maana.

Kwenye kitovu cha timu pale Simba Sc, kabla hujawafikia wale walinzi wanne basi juu yao kuna chuma Yusuph Kagoma,mkata umeme wa maana sana kitovuni,kazi kubwa ni kuua moves za mpinzani, kufanya interceptions, kufanya blocking, kushinda mipira ya juu na chini, kufanya clean tackling, kufanya faulo za kiufundi kuipa timu faida kutoruhusu wavu wao kuguswa.

Ametibu kwa kiwango kikubwa na kufanya wachezaji wengine kufanya majukumu yao kirahisi, Fabrice Ngoma anaonekana kuwa bora zaidi msimu huu lakini siri ya hayo ni Yusuph Kagoma.

Vitu vya kuboresha kwake ambavyo nimevin'gamua ni FIRST TOUCH ZAKE,kuna mazingira anakua na poor first touch inayotoa faida kwa opponent kuiba mpira

Kingine ni acheze though game na sio faulo amabazo wazi wazi zinaonekana na kwa waamuzi Smart moja kwa moja ataigharimu timu.

Mtu sana huyu, kinachohitajika ni muendelezo mzuri wa kiwango mechi baada ya mechi

10/04/2025

TUNAHITAJI NAMBA 10 BORA ZAIDI - FADLU
Kocha wa klabu ya ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟSimba Fadlu Davies amewataka mashabiki wa Simba kutosherehekea mafanikio ambayo wanayapata kwasasa na zaidi waendelee kumpa imani kwenye ujenzi wa timu yake kwani msimu ujao anahitaji kumsajili kiungo namba 10 bora Tanzania.

โ€œTusishekerekee sana kwa sababu bado kuna mambo ya kutimiza zaidi,.Huu ni msingi tu, tunaendelea kujiimarisha na tumeshakaa kikao cha usajili ujao tayari na sasa tunamtafuta kiungo namba 10 bora zaidi wa Tanzania na natumaini tutainasa saini yake.โ€

- Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa klabu ya Simba.

N.B Mie nikiandika kuwa namba 10 aliyekuwepo kwa sasa hatoshi ninaonekana nina Nongwa๐Ÿ˜‚ Alhamdulillahโ€ฆ! Kocha amerudi kudunda nyundo mule mule๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ

Mengine ni ubishi tu wa kutokujua mpira๐Ÿ˜‚


Cc,

08/01/2025

K**A KUNA SHABIKI WA SIMBA SC ANAHITAJI KUWA NA PAGE YA SIMBA SC HII NAIUZA NJOO INBOX ILI AWEZE KUIRUN KWA WAKATI

08/01/2025

Watu mnashindwa kuelewa kanuni ya CAF inasemaje!
Kanuni inasema hivi:
Iwapo timu zitafungana Kwa pweint kinachoangaliwa ni HEAD2HEAD
Kwa maana hiyo SASA Simba sc akitoa sare na bravos atakuwa amepita kotokana jinsi walivyokutana
Simba sc atakuwa na alama 10
Wakati bravos anabaki na alama 7
Na iwapo Simba sc akifungwa atakuja dar kumsubiri constine na Simba sc akimfunga anakuwa na point 12
Kumbuka Simba sc anahitaji japo goli Moja TU Kwa constantin il afuvu
SIJUI MMEELEWA?

17/02/2024

Inawezekana naona tofauti na wengi lakini naona kuwa lazima kuna mambo kadhaa ambayo Simba wanapaswa kubadilisha katika kikosi chao ili kukifanya kuwa bora...

Mechi iliyopita Vs JKT kunaweza kuwa na sababu ya kiwanja lakini unaona suala la kikosi kinachopambana linabaki kwa baadhi ya wachezaji na wengine wanaonekana kuwa slow au k**a wamechoka hivi...

Kuna vitu vinabadilika lakini yanapaswa kuwa mabadiliko ya pamoja na kwa kuwa Simba sasa inarejea kimataifa na fainali yao ni Vs Asec ugenini, lazima FIGHTING SPIRIT iwe ya KIWANGO CHA JUU ili kupata majibu sahihi.

Uwezo bila juhudi na maarifa navyo vinaweza visiwe na faida....UKITULIA...UTANIELEWA. cc salehjembe๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

16/02/2024

MKAZUZU ANASEMA
TATIZO LA SIMBA BADO NI LILELILE.

Tangu timu ipo chini ya kocha mkuu aliyepita Robertinho hawakuwa vizuri technically hasa kwenye kuzuia kitu ambacho kilikuwa kinawafanya wafikike kirahisi na wapinzani wao haijalishi walikuwa wanacheza na wapinzani wa aina gani.

Ahueni ya Simba wamecheza na timu nyingi ambazo hazina wastani mzuri wa kutumia nafasi ndio maana kuna mechi Simba imeshinda lakini hawajatengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wao sometimes we called it lucky.

Mpaka sasa chini ya Benchika bado tatizo lile la Simba linaendelea kuwasumbua, mechi ambazo Simba wamecheza chini ya Benchika licha ya kupata matokeo lakini bado hawajatibu tatizo lao hasa kwenye defense yao hasa kwenye (turn over)

Simba ikipoteza mpira ikiwa inashambulia ni rahisi kwa wapinzani wao kuwafikia kirahisi mwanzo ilisemekana ni kukosekana DM kwenye eneo la kiungo lakini amekuja Babacar Sarr bado tatizo lipo, Nahisi kuna namna kocha inabidi aangalie namna ya kulidhibiti.

K**a Simba ikikutana na timu ambayo inauwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na kuzitumia vizuri basi yatakuwa yale ambayo walikutana nayo dhidi ya Yanga chini ya Robertinho.

NB;Che Malone anafanya kazi kubwa kwenye eneo la ulinzi kutokana na kutokuwa bora kwenye eneo la kiungo.

15/02/2024

Here we go,
kunako majila ya saa kumi za jioni ya leo katika dimba la meja general isamuhyo mbweni dar es ssalaam chama la wana lunyasi simba sc tutacheza dhidi ya mwenyeji wetu Jkt tanzamnia.

Msemaji wa wana lunyasi ahmed ally amesema katika mchezo huo mashabiki wengi tunatakiwa tuwe sisi wana simba sc haijalishi uwanja uko katika hali gani.

Kumbuka kuwa uwanja unaingiiza watazamaji 5000 tu kwa hiyo kuwahi kwako kutasaidia wewe kukaka mbele zaidi kwani uwanja hauna viti watazammaji watasimama mwanzo mwisho.

NB: PICHA KUTOKA MAKTABA

14/02/2024

Repost ahmedally_ MUONGOZO KWA WANASIMBA

Mechi yetu kesho ni saa 10:00 Jioni katika Uwanja wa Meja Genaral Isamhuyo Mbweni

Tiketi ni Sh Elfu 10 tuu hakuna chini ya hapo wala juu ya hapo

Tiketi zitauzwa maeneo ya karibu na Uwanja

Sisi hatuna ugeni hivyo tunapawa kuja kwa wingi Uwanjani na kuutawala Uwanja

Tujiandae kisaikolojia Uwanja hauna viti tutasimama mwanzo mwisho k**a tunaswalia maiti

Tunaoenda Uwanjani tununune tiketi mapema kwani Uwanja unaingiza watu 4000 tu.

Kwa ukubwa wetu, Mashabiki 3900 Wanatakiwa kuwa wa Simba na 100 ni hao wengine

๐Š๐š๐ซ๐ข๐›๐ฎ๐ง๐ข ๐ˆ๐ฌ๐š๐ฆ๐ก๐ฎ๐ฒ๐จ, ๐ค๐š๐ฆ๐š ๐ฎ๐ง๐š ๐ฆ๐ค๐ž๐ค๐š ๐ง๐ฃ๐จ๐จ ๐ง๐š๐จ

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


BUGULUNI MALAPA
Dar Es Salaam