Jioni iwe poa kwenu washkaji zetu.
Part of Pain Jogging Sports Club
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Part of Pain Jogging Sports Club, Sports, Dar es salaam, Dar es Salaam.
25/01/2019
Mlamkaze?
Habari zenu wadau?
Waswahili wanasema kimya kingi kinamshindo je unataka kujuwa tunakuja na mshindo gani?
Endelea kuwa nasi.
17/12/2017
Uongozi wa part of pain jogging sports club pamoja na wanachama wote kwa ujumla tunakupongeza sana mwanachama mwenzetu ndugu Issa Ismail kwa kuhitimu masomo yako.
Tunakutakia maisha mema na yenye mafanikio.
All the best wadogo zetu wa form four mnaofanya mtihani leo mungu awe nanyi.
Habari zenu?
Habari za leo wadau wetu?
Mipango ya maboresho ya club yetu PART OF PAIN JOGGING yanaendelea kuanzia ngazi ya uongozi mpaka kwa wanachama wote kwa ujumla.
Moja ya maboresho hayo ni kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya lakini vile vile kila mwanachama atapewa mkataba utakaomlinda yeye juu ya kupata haki zake stahiki.
Tunakaribisha wadhamini popote walipo waje kuwekeza kwetu.
Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu mtongani au piga simu kupitia 0677 278 979.
"MAZOEZI NI AFYA MICHEZO NI AJIRA"
Siku ya tano ya mwezi wa kwanza mwaka 2017.
Tuna tarajia kufanya mambo mazuri ndani ya mwaka huu ila kikubwa tunaomba sapoti kutoka kwenu wadau wetu ili tuweze kutimiza malengo yetu.
PART OF PAIN JOGGING SPORTS CLUB
+255 677 278 979 MTONGANI DAR ES SALAAM.
YAH:MUHARIKO WA USAFI UTAKAOFANYIKA TAREHE 31/12/2016
Vijana wa PART OF PAIN JOGGING SPORTS CLUB wenye maskani yetu mtaa wa MTONGANI kata ya AZIMIO wilaya ya TEMEKE mkoa wa DAR ES SALAAM tutauaga mwaka 2016 kwa kufanya usafi katika maeneo ya mtaa wetu.
Hivyo basi kutokana na umuhimu wako/wenu kwetu tumeamua tuwaharike/tukuharike ili uweze/muweze kushirikiana nasi katika siku hii muhimu kwetu.
Uwepo wenu/wako utatufariji na kutupa nguvu katika kutimiza agizo la muheshimiwa rais wa nchi yetu ndugu JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI la kufanya usafi kila jumaamosi ya mwisho wa mwezi.
Tunaomba uje/muje na vifaa vya usafi ili kuongezea nguvu ya vifaa vilivyopo.
Tunatanguliza shukrani za dhati kwenu/kwako pia tunamuomba mwenyezi mungu awajaalie/akujaalie afya njema ili uweze/muweze kuungana nasi siku ya tarehe 31/12/2016 kwa pamoja tufanye usafi.
"KWA PAMOJA TUIJENGE TANZANIA SAFI"
Imetolewa na
MUBARAK H LUSONZO
Msemaji wa kundi.
Weekend njema kwenu wadau wetu.
Dhumuni letu ni kuwajenga vijana katika imani ya kiundugu na kuwatoa katika fikra mbaya za uharifu, uvunjifu wa amani na utumiaji wa mihadarati (madawa ya kulevya)
Tunahamini mazoezi ni afya na michezo inatujenga kuwa raia wema.
Tunahitaji mchango wa mawazo kutoka kwenu wanajamii wenzetu ili kwa pamoja tuijenge tanzania njema.
Msisite kuwasiliana nasi kupitia kwenye akaunti zetu za mitandao ya kijamii kwa maoni na ushauri zaidi.
Tupo instagram, facebook na twitter vilevile tunapatikana whatsaap kwa namba 0623 052 246.
Tushirikiane kuwajenga vijana ili tuijenge tanzania.
17/12/2016
Michezo ni afya.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Address
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam