13/10/2020
*Tunatoka kweny familia za kimaskini zenye makazi yaliochakaa,Huku vifuani mwetu tumebeba majonzi na huzuni Mkubwa*
*Tunapambana lengo si kujionyesha kwa watu na wala sio kwa kushindana na watu*
*Bali Nia yetu kutaka kubadili ile hali iliyopo katika familia zetu,Usikubali mtu akukatishe tamaa kila mmoja wetu ana malengo yake na majukumu yake kweny familia yake*
* *
* *
* *
12/10/2020
Ningelipenda kukuliza swali hili "
JE, WEWE NI DARAJA AU UKUTA KWA WATU WENGINE"
😢Hivi na wewe ni miongoni mwa wale wanaokwazika wengine wakifanikiwa.
🥺Wakipata mchumba unakasirika, wakinunua gari una nuna?
🥶Umo kwenye wale ambao hawapendi kuwaona wenzao wakiwazidi fedha, Uchumi, ujuzi.
😤Hupendi kuwaona wengine wakiwa na furaha?
Natumaini hauko hivyo.
Sote katika ulimwengu huu, tumeletwa kwa kusudi na k**a tukilitumikia shauri letu vizuri basi tunaweza kuishi maisha yenye furaha.
Tunapaswa kufanyika baraka kwa wengine na sio balaa. Kuwa madaraja na sio ukuta.
✍🏿 kuna watu wanaotusubiri tupige hatua katika maisha ili tufanyike daraja kwao, kufikia ndoto zao.
✍🏿 Ukilala ama kukata tamaa kuna maelfu ya watu nyuma wanakusubiri ufanyike daraja, ili na wao wafanyike daraja kwa wengine.
📒 Furaha yako na iwe katika kuijenga furaha ya watu wengine, tusimame kwa pamoja kuyafuta machozi ya wanaolia sasa, maana kesho watakapocheka watatukumbuka tulipokuwa pamoja nao taabuni.
Mabadiliko huanza na Fikra, Chukua hatua
Mafanikio yanaitaji subra na uvumilivu
10/10/2020
TAMBUA MIFUMO MITATU YA BIASHARA INAYOTAMBULIKA DUNIANI KOTE;
1-Mfumo wa kawaida wa maduka (jumla na rejareja). Asilimia 90% dunian kote wanatumia MFUMO hii
2-FRANCHISE mfumo huu unamilikiwa na watu wachache sana na wenye mitaji mikubwa sanaa (matajiri)
✍️Biashara izi wanatumia NEMBO ya makampuni mama ambayo imeshafanikiwa sana na bidhaa zake kutambulika na kukubalika duniani kote
Mfano,,cocacola,Pepsi,Sonny Samsung* etc
3-NETWORK MARKETING(Biashara za mtandao)
✍️Ni mfumo wa kibiashra ambao mteja alielizika kumshirikisha mtu mwingine kwa njia ya maneno ya mdomo(word of mouth marketing)
✍️Kuwashirikisha wengine kunaweza kufnyika mahali popote k**a Nyumbani,Maofisini,saloon,Chuo,Migahawani na kwenye mitandao ya kijamiii
*Internet*
*Facebook*
*Istagram*
*Linked in*
*WhatsApp*
*Twitter*
*YouTube*
Inaendelea......✍✍
10/10/2020
HAIJALISHI UPO KATIKA HALI GANI!!
Mafanikio ni kitu ambacho kila mtu anakihitaji katika maisha. Lakini tunasahau kwamba mafanikio ni mchakato ambao hutumia hatua za mtoto, ndio maana ilimchukua miaka 18 kwa Jack Ma kuwa na Alibaba ya Sasa.
Unapaswa kuenjoy process ( Mchakato) na sio hatma. Kila mmoja hutazama mwisho wa changamoto bila kujifunza faida yake ili utakapohitimu uwe na kitu cha kujipongeza kwa kushinda.
Ukweli ni kwamba itakuchukua siku nyingi kuweza kufanikisha jambo unalolihitaji.
Utakutana na upinzani mwingi wa kutosha lakini hupaswi kuiacha njia unayoiamini na kujikatia tamaa.
Ipo hivi,
Humchukua miezi 9 mama mjamzito kuipokea furaha yake mikononi mwake.
Lakini, humchukua miaka 2 Mama Tembo kumpata mtoto tembo.
Pia, humchukua kuku siku 21 kuweza kupata vifaranga vyake.
Kila jambo lina muda wa utimilifu wake kwa kuzingatia uthamani na umuhimu wake katika maisha.
Najua unapitia wakati mugumu, lakini usiwe na shaka wala wasiwasi, endelea kupika hatua.
Tambaa》Tembea》Kimbia》Ruka.
Mabadiliko Huanza na Fikra, Chukua Hatua.
08/10/2020
Kuna watu mtaanza wote CHINI ila wakipanda juu HAUTAKUWA nao.
Hili lazima ulikubali na ulizoee.
Ni kweli, mlihangaika wote, ila baada ya yeye kupanda juu amekusahau.
Ni kweli mlisoma darasa moja ila leo yeye ni mkurugenzi na wewe unatafuta kazi na ameshindwa kukusaidia.
Ni kweli, mlikua mnaishi mtaa mmoja na yeye sasa ni milionea na wewe unatafuta mtaji, ameshindwa kukusaidia.
KUNA MAMBO NATAKA NIKUKUMBUSHE :
1. Kuna watu ambao wewe unawachukulia k**a ni watu wako wa karibu sana ila wao hawakuoni hivyo, hauna nafasi kwao k**a nafasi uliyowapa wewe.
2. Kuna watu huwa wanaamini kilichowafikisha hapo ni juhudi zao.
Wakikuangalia wanakuona wewe ni mzembe haujafanya juhudi k**a wao.
3. Kuna watu ni kawaida yao wakipanda juu huwa wanatupa marafiki wote walioanza nao na wanatafuta wapya.
Huwa wanakumbuka marafiki wa zamani wakianza kupata shida tena.
4. Kuna watu Mungu hatakuja kuwaruhusu wakusaidie wasije wakakuingiza kwenye mambo yatakayokuharibu.
5. Usiwalaani WALIOKUSAHAU, bali UMSHUKURU MUNGU ambaye bado ANAKUKUMBUKA.
6. SIKU YAKO INAKUJA !