15/09/2025
Alphonce Simbu: MWANARIADHA ALIYEAMUA KUZUNGUMZA KUPITIA MIGUU YAKE"
Alphonce Simbu, shujaa wa Tanzania, amejijengea jina kwa kuonyesha nguvu, uvumilivu na juhudi zisizo na kifani kwenye mbio za masafa marefu. Anajulikana k**a “mwanariadha asiyeimbwa”, ambaye badala ya maneno, anazungumza kupitia miguu yake yenye nguvu.
Ushindi wa Tokyo 2025
Jana, Tokyo, Simbu aliibuka mshindi wa Mashindano ya Dunia, akithibitisha kuwa bidii, nidhamu, na moyo thabiti huzaa matunda. Mbio hizo zilimshuhudia akipigana hadi mwisho, akivunja mipaka na kushinda washindani wakali kutoka kote duniani.
Mafanikio na Mataji
Dunia, Tokyo 2025 – Shindi
Silver Medal – World Half Marathon Championships
Medali kadhaa – African Championships
Simbu ni kielelezo halisi cha kupambana bila kusita. Anaonyesha uthabiti, ari, na juhudi zisizo na kifani, akichochea vijana wa Tanzania kuona kuwa ndoto zinatimia kwa bidii na moyo thabiti. Miguu yake inazungumza zaidi ya maneno, ikitoa funzo kwa kizazi kipya cha wanariadha na mashabiki wote: ushindi unapatikana kwa matendo, si maneno tu!
14/09/2025
"KIBURI KINAVYOMGHARIMU RUBEN AMORIM MANCHESTER UNITED"
Kitaaluma, ili Manchester United iwe na ushindani mkubwa katika Premier League, Amorim anapaswa kurekebisha mbinu zake kwa namna ifuatayo:
1. Mabadiliko ya Mfumo – Kubadilisha kutoka 3-4-3 kwenda 3-5-2 au 3-4-1-2 kutaongeza wachezaji katikati ya uwanja, kutoa udhibiti zaidi wa mpira, na kupunguza mapengo nyuma ya wingbacks.
2. Matumizi Sahihi ya Wachezaji – Bruno Fernandes apewe nafasi ya namba 10 kwa uhuru wa ubunifu, wakati Ugarte na Mainoo wafanye kazi ya “double pivot” kudhibiti kasi na nguvu za wapinzani. Šeško, badala ya kuachwa peke yake, apewe mshirika wa karibu ili kuongeza tishio la mashambulizi.
3. Ubunifu Katikati – United inahitaji kuondoa utegemezi mkubwa wa mashambulizi ya pembeni kwa kuunganisha winga wanaoingia ndani (k**a Mbeumo au Amad) na viungo wa kati, ili kuvunja safu za “low block” zinazotumiwa na wapinzani.
4. Uwepo wa Mpango B – EPL ni ligi yenye ushindani mkubwa, hivyo United inapaswa kuwa na mfumo mbadala (mfano 4-2-3-1) ili kukabiliana na timu tofauti badala ya kushikilia mfumo mmoja unaotabirika.
5. Press ya Pamoja – Badala ya kuachia nafasi nyingi nyuma, Amorim aandae kikosi chake kufanya pressing ya haraka na kwa pamoja mara baada ya kupoteza mpira, kupunguza uwezekano wa wapinzani kutumia counter-attack.
Kwa jumla, mafanikio ya Amorim katika EPL hayatahitaji tu kushikilia falsafa yake, bali pia kubadilisha mbinu kwa kuendana na sifa za ligi na wachezaji alionao.
07/09/2025
Imearifiwa kuwa klabu ya Yanga Kwa Sasa imna thamani ya shilingi Bilioni 100 za Kitanzania. Hayo yamesenwa na Mwenyekiti anayesimamia mchakato wa mabadiliko katika klabu ya Yanga ndugu Alex Mgongolwa.
Yqpi maoni Yako? Je Yanga wanawazidi Al Ahly Kwa kuwa klabu yenye thamani kubwa barani Afrika? Au ni muendelezo wa kiki ?
11/05/2016
KAIZER CHIEFS WAGOMA KUMPOKEA AJIB IBRAHIMU! | JIPE RAHA5 http://jiperaha5.blogspot.com/2016/05/kaizer-chiefs-wagoma-kumpokea-ajib.html?m=1 #.VzLTbIFHh1s.whatsapp
KAIZER CHIEFS WAGOMA KUMPOKEA AJIB IBRAHIMU! | JIPE RAHA5
Viongozi wa Kaizer Chiefs timu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini wamegoma kuthibitisha ikiwa mshambuliaji hatari wa Simba sports ya Dar es salaam Ibrahim Ajibu anayetarajia kufanya majaribio klabuni hapo. Haya yanakuja siku chache baada ya Ajibu kuitoroka klabu yake ya Simba. Msemaji wa Klabu h...
10/05/2016
MABASI YA MWENDO KASI YAANZA KWA KISHINDO DAR... | JIPE RAHA5 http://jiperaha5.blogspot.com/2016/05/mabasi-ya-mwendo-kasi-yaanza-kwa.html?m=1 #.VzH7ZSaUlfk.whatsapp
MABASI YA MWENDO KASI YAANZA KWA KISHINDO DAR... | JIPE RAHA5
Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT nchini Tanzania imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
28/03/2016
Sauti ya Kariakoo
Jumba Maalumu la Spoti