10/05/2018
Simba bingwa
LIKE PAGE YETU ili kuweza kupata habari mbalimbali za michezo hususani soka la BONGO., KARIBUNI
10/05/2018
Simba bingwa
10/05/2018
Burudani safi na salama
30/10/2017
...
Singida United imedhamilia kufungua uwanja wa Namfua kwa kupata ushindi dhidi ya Yanga wiki hii.
Mashabiki wa soka mkoa wa Singida wanahamu kubwa ya kuiona Singida United ikicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Namfua tangu msimu wa 2000/2001.
Joto la mechi kati ya Singida United na Yanga halipo katika manispaa ya Singida pekee, ila kila kona ya mkoa huu unaosifika kwa kuwa na vijana wengi wanariadha.
Mkuu huyo wa wilaya, pamoja na kuwashukru wakazi wa manispaa ya baadhi kutoka nje ya manispaa, kwa michago yao ya hali na mali iliyofanikisha ukarabati huo.
“Nitumie nafasi hii kuwaalika wapenzi wa michezo wa mkoa wa Singida na mikoa jirani ya Manyara, Simiyu, Dodoma na Tabora.
“Matarajio yangu ni Uwanja wa Namfua kuwa machinjo kwa timu zote za mikoa mingine kila zinapocheza hapa,” alisema kwa kujiamini.
Aidha, Tarimo alisema wamefanya maandalizi ya hali ya juu kwa ajili ya kuipokea Singida United katika maeneo ya kijiji cha Kisaki.
“Tutahamasisha ndugu zetu wa bodaboda, wenye magari binafsi hasa mabasi, wajitolee kusafirisha mashabiki wa Singida United kwenda kuipokea timu yao ambayo, sasa inahamishia mechi zake nyumbani," alisema.
Naye mstahiki meya manispaa ya Singida, Chima Mbua Gwae, wakati akifunga kikao cha baraza la madiwani leo, aliwaalika madiwani na wananchi wote wa manispaa ya Singida kuhudhuria kushudia mechi kati ya Singida United na Yanga.
“Sisi wakazi wa manispaa ya Singida, hii ni bahati yetu kubwa ya kunufaika kiuchumi kupitia michezo ya Ligi Kuu itakayofanyika Namfua. Sote siku hiyo tuwe upande moja na Singida United. Mapenzi kwa Yanga yaje baada ya mechi,” alisema meya Gwae na kuwavunja mbavu waheshimiwa madiwani.
Mkazi wa kijiji cha Ihanja aliyejitambulisha kwa jina moja, Mchungaji alisema kijiji hicho huenda Novemba nne mwaka huu, kikabakiwa na wakazi wachache, tena ni wale watakaokuwa wagonjwa siku hiyo,au wazee na vikongwe.
13/10/2017
..
MITAANI kuna kelele nyingi kuhusu kiungo, Jonas Mkude, kutoanzishwa kikosi cha kwanza pale Simba, huku wengine wakiona poa kwa vile Mghana James Kotei anafanya vizuri kwenye eneo la kati.
Lakini huko mazoezini wameliamsha. Kinachoendelea katika mazoezi ya Mnyama kuelekea mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar ni mpambano usio wa kawaida kati ya wachezaji hao wawili.
Viungo hao wamekuwa wakipambanishwa na kocha Joseph Omog, huku kila mmoja akionyesha vitu adimu ambavyo vimekuwa vikiwachanganya hadi wadau wa klabu hiyo kushindwa kujua nani mkali.
Katika tizi linalopigwa Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, kocha amekuwa akiwapa kazi viungo hao kuonyesha umahiri wao hasa kutokana na ugumu wa mechi hiyo ambayo Mtibwa wameonekana kuipania.
Katika mazoezi ya juzi Jumatano jioni, Omog aliamua kugawa timu yake katika vikosi viwili; cha kwanza kikiundwa na Aishi Manula, Ally Shomary, Jamal Mwambeleko, Yusuf Mlipili, Salim Mbonde, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Juma Liuzio, Nicholas Gyan na Haruna Niyonzima.
Huku kikosi kingine kikiwa na akina Emmanuel Mseja, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Method Mwanjali, Juuko Murshid, James Kotei, Jamal Mnyate, Mzamiru Yassin, John Bocco, Mohammed Ibrahim na Mwinyi Kazimoto.
Baada ya hapo akavipambanisha kwa muda wa dakika 40 na kazi kubwa ilionekana eneo la katikati kwa Mkude na Kotei kuonyeshana ushindani wa hali ya juu kila mmoja akitaka kumfunika mwenzake.
Wawili hao kila wakati walikuwa wakishindana katika kugombania mpira, kukaba na katika kuoneshana ufundi wa kupiga pasi ndefu na fupi jambo ambalo limeacha mtihani kwa kocha kwamba nani aanze.
Baada ya tizi hilo la nguvu.
12/10/2017
WINGA machachari wa Simba, Shiza Kichuya amefichua kuwa uwepo wa Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima katika klabu hiyo umemgusa kwa namna moja ama nyingine na kubadilisha mtazamo wake kwa namna alivyokuwa akichukulia mambo.
Ameeleza kuwa mastaa hao wana kiwango cha kimataifa kutokana na uzoefu wao na walikopitia jambo ambalo linampa changamoto ya kutathimini kazi yake ili ajue kitu gani anatakiwa kukiboresha.
"Ndani ya mechi tano ambazo tayari tumecheza nimejifunza vitu vingi hasa kwa mastaa hao. Kwanza uzoefu wao unawabeba, wanajua kitu cha kufanya kwa kila mechi, hilo linafanya mazoezi yangu yawe zaidi kuliko wao," alisema.
"Mimi nimetoka Mtibwa Sugar, na kujiunga na Simba, lakini wao wamepitia klabu tofauti zenye ujuzi tofauti, naamini nikitulia na kujua siri iliyowafanya wafike hapo, nitafika mbali zaidi kuliko kujifanya mjuaji," alisema.