19/02/2026
Iran yajenga ngao ya zege katika eneo la kijeshi huku kukiwa na mvutano mkali wa Marekani
Michezo na burudani
19/02/2026
Iran yajenga ngao ya zege katika eneo la kijeshi huku kukiwa na mvutano mkali wa Marekani
18/02/2026
Premier League imetoa orodha ya wachezaji wote wenye Imani ya Kiislamu ambao watafunga mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani 🌟🌙.
Lengo la kutoa orodha hiyo ni kutambua uwepo wao utakaofanya mechi zisimishwe Kwa muda Ili waweza kufuturu wakati ukifika k**a mechi ikiwa inaendelea,wachezaji hao orodha Yao ni k**a ifuatavyo:
🇫🇷 William Saliba — Arsenal
🇫🇷 Boubacar Kamara — Aston Villa
🇧🇪 Amadou Onana — Aston Villa
🇲🇦 Amine Adli — Bournemouth
🇹🇷 Enes Ünal — Bournemouth
🇧🇫 Dango Ouattara — Brentford
🇹🇷 Yunus Konak — Brentford
🇬🇭 Tariq Lamptey — Brighton
🇹🇷 Ferdi Kadioglu — Brighton
🇸🇪 Yasin Ayari — Brighton
🇬🇲 Yankuba Minteh — Brighton
🇹🇳 Hannibal Mejbri — Burnley
🇨🇭 Zeki Amdouni — Burnley
🇫🇷 Wesley Fofana — Chelsea
🏴 Tosin Adarabioyo — Chelsea
🇫🇷 Naouirou Ahamada — Crystal Palace
🇲🇦 Chadi Riad — Crystal Palace
🇸🇳 Ismaïla Sarr — Crystal Palace
🇲🇱 Cheick Doucouré — Crystal Palace
🇲🇦 Adam Aznou — Everton
🏴 Tyrique George — Everton
🇸🇳 Idrissa Gana Gueye — Everton
🇸🇳 Iliman Ndiaye — Everton
🇫🇷 Thierno Barry — Everton
🇫🇷 Issa Diop — Fulham
🇪🇸 Adama Traoré — Fulham
🇫🇷 Ibrahima Konaté — Liverpool
🇫🇷 Hugo Ekitiké — Liverpool
🇪🇬 Mohamed Salah — Liverpool
🏴 Kieran Morrison — Liverpool
🇺🇿 A. Khusanov — Man City
🇩🇿 Rayan Aït-Nouri — Man City
🇫🇷 Rayan Cherki — Man City
🇪🇬 Omar Marmoush — Man City
🇹🇷 Altay Bayındır — Man United
🇲🇦 Noussair Mazraoui — Man United
🇨🇮 Amad Diallo — Man United
🇨🇲 Bryan Mbeumo — Man United
🇩🇪 Malick Thiaw — Newcastle
🇨🇩 Yoane Wissa — Newcastle
🇨🇮 Ibrahim Sangaré — Nottingham Forest
🇲🇿 Reinildo Mandava — Sunderland
🇨🇬 Arthur Masuaku — Sunderland
🇸🇳 Habib Diarra — Sunderland
🇨🇭 Granit Xhaka — Sunderland
🇫🇷 Abdoulaye Mustapha Ba — Sunderland
18/02/2026
Daktari bingwa auawa vitani:
Daktari ajulikanaye kwa jina la Arouna Louré, aliuawa vitani katika mstari wa mbele wa mapigano huko Burkina Faso.
Baada ya daktari huyo kumkosoa Mheshimiwa na jeshi lake kuwa hawajui kupambana na magaidi na kuongeza kuwa serekali hiyo imeshindwa na ugaidi, hata hivyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa Ibrahim Traore ni dhaifu hana uwezo wa kuongoza nchi kubwa k**a Burkina Faso, baada kauli hizo Daktari Arouna Louré alik**atwa na jeshi la nchi hiyo na kuandikishwa kwa nguvu jeshini, na kupewa mafunzo wa mda mfupi ili akaonyeshe kwa vitendo mbinu za kupambana na magaidi vitani k**a alivyokuwa akikosoa mara kwa mara. Kwa bahati mbaya magaidi wamemuuwa vitani.
10/02/2026
📶TETESI ZA SOKA ZINAZOENDELEA BARANI ULAYA LEO JUMANNE YA FEBRUARY 10,2026.
Cristiano Ronaldo anatarajiwa kusitisha mgomo wake katika klabu ya Al-Nassr na kucheza tena katika klabu hiyo ya Saudi Pro League siku ya Jumamosi.
Fowadi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 41 amekosa mechi mbili kwa sababu hakufurahishwa na jinsi klabu hiyo inavyoendeshwa. (Sky Sports)
Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford Barcelona inategemea uchaguzi wa rais wa klabu hiyo mwezi ujao.
Mkataba wa pauni milioni 26 kwa mshambuliaji huyo wa Manchester United kwa mkopo, 28, ndio kiini cha ombi la Joan Laporta kuchaguliwa tena. (Times - Subscription Required}
Manchester United itamlenga mshambuliaji wa Everton na Senegal Iliman Ndiaye, 25, ikiwa Rashford atahamia Barcelona kwa mkataba wa kudumu. (Caught Offside),
Bournemouth inapanga kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Eli Junior Kroupi, 19, kandarasi mpya yenye unono mwingi kwa nia ya kuzuia kutakiwa na baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya, vikiwemo Chelsea, Liverpool, Real Madrid na Paris St-Germain. (Sun),
Manchester City wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 100 kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Elliot Anderson, 23. (Teamtalks)
Bayern Munich hawatarajii kumsaini fowadi wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, na hivyo kuongeza matumaini ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Christian Falk),
AC Milan wana imani kuwa Fulham watatoa chaguo la pauni milioni 21 kumnunua winga wa Nigeria Samuel Chukwueze, 26, ambaye yuko kwa mkopo Cottagers. (Gazzetta - In Italy)
Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mjerumani Rocco Reitz, 23, ambaye thamani yake ni takriban £35m. (Fichajes - In Spanish)
Mchezaji mwengine anayelengwa na Manchester United, Sandro Tonali wa Newcastle United, huenda akawa na bei ya hadi £100m. Kiungo huyo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 25 pia anavutia klabu za Arsenal, Manchester City na Juventu
05/02/2026
MVUTANO UMERUDI NDANI YA REAL MADRID: 🔥
Kocha Álvaro Arbeloa yuko chini ya shinikizo ndani ya chumba cha kubadilishia nguo:
❎️ Baadhi ya wachezaji wanahisi yeye ni meneja wa muda tu. Kwahiyo hakuna MABADILIKO YOYOTE ambayo yameonekana mpaka sasa.
❎️ Kikosi kilishangaa kwamba Dani Ceballos hakucheza dhidi ya Benfica katika mchezo wa UEFA Champions League.
❎️ Mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi ya Rayo Vallecano ulicheleweshwa kwa sababu ya kutoelewana na wachezaji wake.
Source: [ La Ser ]
03/02/2026
WAZIRI WA MICHEZO UKRAINE AMSHAMBULIA INFANTINO KWA KAULI KUHUSU URUSI
Waziri wa Michezo wa Ukraine amemkosoa vikali rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, akimtaja kuwa “asiye na uwajibikaji” na “mwenye mawazo ya kitoto” kufuatia kauli yake kwamba FIFA itazingatia kuondoa marufuku iliyowekwa dhidi ya Urusi. Timu za taifa za Urusi pamoja na klabu zake zilifungiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa na FIFA pamoja na UEFA mwezi Februari 2022 baada ya uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine.
Licha ya vita kuendelea, Infantino amenukuliwa akisema kuwa marufuku hiyo “haijafanikisha chochote” na badala yake “imeongeza tu hasira na chuki.” Aliongeza kuwa kuruhusu wavulana na wasichana kutoka Urusi kushiriki michezo ya soka katika maeneo mengine ya Ulaya kunaweza kusaidia kupunguza mgawanyiko na kuleta mshik**ano kupitia michezo.
Akijibu kauli hizo kupitia mitandao ya kijamii, Waziri wa Michezo wa Ukraine, Matvii Bidnyi, alisema maneno ya Infantino “hayana uwajibikaji — na hata ni ya kitoto.” Alisisitiza kuwa kauli hizo zinatenganisha soka na uhalisia wa vita ambako watoto wanauawa. Bidnyi alikumbusha kuwa tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi, zaidi ya wanamichezo na makocha 650 wa Ukraine wameuawa, wakiwemo zaidi ya wachezaji wa soka 100.
04/10/2024
Mtangazaji wa Wasafi Media Dida Shaibu amefariki Dunia baada ya kuumwa na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mtangazaji mwenzie Maulidi Kitenge.
30/09/2024
Mahak**a ya Hakimu Mkazi Dodoma (Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki) leo September 30,2024 imewahukumu kifungo cha maisha jela Washtakiwa wanne wakiwamo Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Magereza baada ya kuwakuta na hatia katika makosa yote mawili walioshtakiwa nayo la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti Mkazi wa Yombo Dovya, Jijini Dar es Salaam.
Kesi hii ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 ilikuwa inawakabili Washtakiwa wanne akiwamo MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo ambaye ni Askari wa JWTZ, Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.
Kesi hii maarufu ‘Waliotumwa na Afande’ imesikilizwa faragha katika Mahak**a ya Hakimu Mkazi Dodoma ambapo upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya Washtakiwa.
Washtakiwa walifikishwa Mahak**ani kwa mara ya kwanza August 19, 2024 na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti huyo ambaye Mahak**ani anatambulika kwa jila la XY ambapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule Washtakiwa hao baada ya kusomewa mashataka walikana na kutokana na unyeti wa kesi hiyo hawakupatiwa dhamana ambapo baada ya kesi kusikilizwa kwa siku kadhaa leo wamesomewa hukumu na kukutwa na hatia hivyo kuhukumiwa kifungo cha maisha.
10/09/2024
Guine 1 _ 2 Tanzania
dk" 88
Tanzania Football Federation
22/08/2024
came TZ
22/08/2024
Kesi ya Jinai iliyofunguliwa na Wakili Paul Kisabo dhidi ya Afisa wa Polisi, ASP Fatma Kigondo anayetajwa k**a ‘Afande’, inasubiri wito wa kupangiwa tarehe ya kusikilizwa ambapo tayari imepangwa mbele ya Hakimu Francis Kishenyi
Afisa huyo ameshtakiwa kwa kuwezesha genge la Watu Watano waliomfanyia ukatili wa Kingono ikiwemo Ubakaji wa Kikundi (Gang R**e) na Ulawiti Msichana ambaye jina lake limehifadhiwa, hivyo anatajwa k**a ‘Binti wa Yombo’
✍️