29/04/2024
๐ดโช ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Siyo Rahisi kihivyo kuachia silaha ikatumike na Adui.
Hapo Mwanzo nilitoa Taarifa Chama kuwa kasaini mkataba wa awali Yanga.Kitu ambacho nataka kuwafungua Akili hapa ni kwamba mkataba wa awali kwa wachezaji huwa Ni njia yakujihami endapo ataachwa basi Mchezaji asikose Timu ya kwenda kucheza
Rasmi nawakikishia kuwa Cloutus Chama atasaini Simba mkataba wa Miaka miwili kwadau la milioni 300, Cloutus Chamab alipigiwa simu na Moe Dewji na kumomba wakutane Ofisini kwake, Huko walifanya mazungumzo kuhusu Kusaini Mkataba mpya, Cloutus Chama alikubali kusani mkataba Huo.Hivi Karibuni Mwamba wa Lusaka Atasaini mkataba kuendelea kusalia Msimbazi..
าแดสสแดแดก Soka leo kwa habari zaidi
29/04/2024
๐พ๐๐๐๐๐ผ ๐๐๐๐
Kevin De Bruyne sasa ana Asists nyingi zaidi za Premier League mwaka 2024 kuliko Bruno Fernandes na James Maddison wamepata msimu mzima.
---->Ameanza mechi 11 pekee๐ฅ๐ฅ
15/04/2024
Rasmi sasa Bayern Leverkusen mabingwa wa bundes league kwa mara ya kwanza katika ligi kuu ujeruman
15/04/2024
Manchester city sasa wanaongoza ligi ya uingereza EPL baada ya Arsenal na Liverpool kupoteza
02/04/2024
ALIYEWAHI KUWA KOCHA WA UTIMAMU WA VIUNGO SIMBA ADEL ZRANE AFARIKI DUNIA
Habari za Tanzia zilizotufikia mezani hivi punde zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa kocha wa utimamu wa viungo wa Simba SC Adel Zrane amefariki Dunia ambapo kwa sasa alikuwa anatumikia klabu ya APR ya nchini Rwanda ambao wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho taarifa yao ikisema
"Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunatangaza kufariki kwa Kocha wetu wa Fitness, Dk. Adel Zirane, chini ya hali ambazo bado hazijaamuliwa. Roho yake ipumzike kwa Amani ya Milele."
Aidha Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za mchezaji Thadeo Lwanga aliyewahi kuwa naye Simba na sasa walikuwa pamoja APR na Meddie Kagere wametoa taarifa hiyo ya kumpoteza mpendwa wao Adel Zrane.
Taarifa zaidi zitakujia endelea kuwa nasi.
29/03/2024
MAMELODI WANATAKA USHINDI KWA MKAPA ..!!๐
๐ฃ๏ธ โMalengo yetu ni kushinda mchezo wa kesho, hatuna malengo tofauti na hayo, tuna lengo moja tu na hilo ni kushinda.โ
- Kocha wa Mamelodi, Rulani Mokwena.
29/03/2024
UPDATES ๐
๐ฃ"Azizi Ki na Djigui Diara bado sijawaona kambini maana walitarajiwa kurudi leo kutoka kwenye majukumu ya timu zao za taifa, Lakini pia kesho nitawakosa zaidi ya wachezaji 4 hadi 5 kwasababu ya majeraha, wachezaji k**a Aucho,Yao Yao, Pacome na kibwana ni majeruhi."- Miguel Gamondi.
29/03/2024
Kikosi cha Timu ya Mamelodi Sundowns ya South Africa kimewasili Dar es salaam kwa ajili ya kucheza mechi yao ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mamelod wamewasili Tanzania wakiwa na vyakula na vinywaji vyao ambavyo kutokana na kuonekana kutoenea kwenye sehemu ya mizigo ya Basi lililowapokea, imebidi vibebwe kwenye gari la mizigo aina ya canter.
28/03/2024
Klabu ya Simba imepata pigo baada ya mlinda mlango Aishi Manula kuripotiwa kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu k**a ambayo yalimuweka nje mwanzoni mwa Msimu huu.
Manula anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kati ya miezi 10 hadi miezi 12.
Kukosekana kwa nyanda huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ni pigo kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC
28/03/2024
Baadhi ya Wachezaji wa Mamelodi Sundowns waliokuwa Algeria kwenye majukumu ya Timu ya Taifa ya Afrika Kusini wakiwa tayari kuanza safari ya kuja nchini kuungana na kikosi cha klabu hiyo ambacho kinatarajia kuingia leo Dar es Salaam.
Picha ya kwanza ni Mlindalango, Ronwen Williams na mwingine ni Themba Zwane ambaye ni kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho.
Mechi ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns itachezwa Jumamosi saa 3:00 usiku