22/02/2021
Nashukuru kwa wote mliokuwa pamoja na mimi wakati wote tangu nilipoanza kazi hii hadi imefika tamati
Hakika Mungu ni mwema sana kwangu hatimaye imekwisha
MUNGU WETU SOTE
pata habari za michezo mbalimbali soka ,ngumi ,gofu , mpira wa pete
22/02/2021
Nashukuru kwa wote mliokuwa pamoja na mimi wakati wote tangu nilipoanza kazi hii hadi imefika tamati
Hakika Mungu ni mwema sana kwangu hatimaye imekwisha
MUNGU WETU SOTE
19/02/2021
Mama told me Martin tell them about the dream
final the dream come true thank you Mama
12/02/2021
Guns n Roses
TARISHI
11/02/2021
Tizama sasa ya kale yamepita na yamekuwa mapya
09/02/2021
NUNDA MZEE
NA MARTIN MAZUGWA
Kitu kilichowastaajabisha si kwasababu vilikataliwa na kila mtu la hasha bali ni jinsi vilivyokuwa vimefungwa kwa ustadi mkubwa na mmiliki wake ambaye hadi wakati huo alikuwa hajajulikana.
Kilichowashtua wengi ni jinsi viroba hivyo vivyokuwa na muonekano k**a maiti iliyoviringishwa ndani ya sanda na tayari kwa kuzikwa.
Jambo hilo liliwagutusha wavuvi hao ambao baadhi wakakata shauri na kutaka kuvifungua viroba hivyo kujionea kilichomo ndani, lakini Mzee Masanja Bundala, ambaye ni mkongwe katika kazi ya uvuvi akawaonya vijana hao ambao tayari walianza kutafuta kisu ilikukata kamba.
Mzee Bundala ambaye ni mzaliwa wa Shinyanga, katika Wilaya ya Kahama ambaye aliondoka huko kuukimbia ukata alikuja jijini Dar es Salaam, kutafuta maisha kutokana na magumu aliyokutana nayo huko alikotoka.
Baada ya kutafuta kazi katika viwanda na taasisi mbalimbali za kiserikali na zile za watu binafsi bila mafanikio ndipo akaangukia katika kazi ya uvuvi ambayo alianza kuifanya tangu miaka ya 1980.
Kwa miaka yote hiyo mzee alikuwa mtu wa kutwa kucha baharini akisaka samaki kwaajili ya kitoweo cha yeye na familia yake ambayo ilikuwa na watoto wawili wa k**e na kiume ambao alibaki nao baada ya mkewe kufariki.
Hivyo aliijua vyema bahari na tabia zake kutokana na kupitia maswahibu mengi ndio maana aliwaonya vijana kuacha haraka kukurupukia jambo ambalo wamepata kuliona kwa mara ya kwanza.
Baada ya kuwasihi kuacha papara katika jambo geni vijana hao wanaamua kutulia na kufuata busara za mzee huyo ambaye alikuwa akiheshimika sana kutokana na busara zake.
***
IKIWA ndio kwanza asubuhi purukushani zilikuwa zikiendelea katika kituo kidogo cha Polisi cha Kawe kilichopo Ukwamani, askari waliokuwa wakiingia kazini wengine walianza kutoka baada ya kumaliza lindo la usiku.
09/02/2021
Hii ni zawadi tunakupa ukale utukumbuke
Waogope sana watu wenye kauli hii
05/02/2021
Ni upendo huvumilia yote
Hauna kisasi na husamehe yote
Haijalishi utapungukiwa na kupoteza vyote
Tumeagizwa upendo tuusambaze dunia yote
Mapendo daima
TARISHI
MUNGU WETU SOTE
03/02/2021
Tumeagizwa upendo
Mapendo daima
If i die don't cry look at the sky and say goodbye
MUNGU WETU SOTE
02/02/2021
Asante sana kwa wale wote ambao wamekuwa wakiniombea na kunisapoti bila kuchoka asante kwa upendo wenu kwangu
Baada kuishi na mzigo mzito kwa zaidi ya miaka nane Leo nimeutua mzigo huo asante mwenyezi Mungu kwa kuniweka huru.
Free at last
free at last
free at last
Thank you almighty God am free at last
25/01/2021
Mwaka 2o17 nilianza kuwa karibu yake Galacha...
Mwaka huo akaniamini na kunipa nafasi ya kuandika kitabu cha maisha yake...
2021 kazi uliyonipa imefika ukingoni sio kwamba Mimi ni bora sana la hasha ni imani yako kwangu
Asante kwa heshima hii RASHID MATUMLA ' SNAKE BOY
GODABOVEALL
12/01/2021
Wakati mwingine tunatumia nguvu kubwa kujikosea wenyewe ili kuwaridhisha wale wanaotuzunguka ...
K**a hiyo haitoshi tunapambana kuwapa tabasamu wengine ili hali ndani ya mioyo yetu tunavuja damu...
Kumbuka huwezi kuwa mwema kwa kila mtu kulazimisha kuwafurahisha watu wengi ni sawa na kumwaga sukari baharini na kusubiri chai iliyokolea sukari....
08/01/2021
Nilipokua kijana mdogo Wazazi wangu waliwahi kuniambia kuwa ipo siku nitasafiri nilicheka sana...
Lakini wao walicheka mara mbili kisha wakacheka tena mara ya tatu kwa nguvu...
Laiti k**a ningejua maana ya kicheko chao ningeudhihirishia umma kuwa ridhiki ni k**a ajali hautambui siku ya kuja..
NATAMANI KUWA MTOTO