13/08/2026
Kutoka kwenye hiki kikosi cha kwanza cha FC Porto kilichoanza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tarehe 26 Mei 2004 dhidi ya AS Monaco, ambapo Porto walishinda mabao 3-0 chini ya JosΓ© Mourinho.
Unaweza kutaja wachezaji wangapi hapoπ€
13/08/2026
Kinachoniuma sio West Ham kucheza Championship, kinachoniuma ni hii mbavu ya kushoto kutoka taifa la Senegal El Hadji Malick Diouf miaka 21 kucheza kule Championship.
Hii mbavu ilisajiliwa mwaka jana tu mwezi July kutoka SK Slavia Praha,ila msimu wake mmoja tu wameshuka daraja.
Nilichokuwa nakiona mimi kwa Diouf hasa ulikuwa wakati wake wa kujitangaza zaidi akiwa EPL ligi inayofuatiliwa zaidi.
Sina maana Championship hakufuatiliwi ila angebaki EPL ingekuwa rahisi zaidi jina lake kuimbwa na vigogo wengi wangepigana vikumbo.
βοΈHaya ni maoni yangu hata na wewe ndugu unayo ya kwako.
13/08/2026
Camera zilimnasa vizuri huyu shabiki wa Aston Villa huko Salzburg jana usiku alipoamua kujiamulia mambo na bado kikawalamba.
13/08/2026
Kuna kipindi ilikuwa ukilitaja jina la PSG, watu walikuwa wanabeza wengi walikuwa wanasema, Ligi ya Ufaransa ni laini,hakuna ushindani wa maana ndiyo maana hata PSG ikifika Champions League haifiki kokote sawa.
Lakini mambo yamebadilika sana kwa mabingwa hawa wa UCL mara 2 tena mfululizo.
Leo hii PSG si timu ambayo vilabu vikubwa vinaitazama kwa uwoga mkubwa sana, mafanikio yao ya miaka ya hivi karibuni yamewafanya wapinzani wengi kuingia uwanjani wakiwa na heshima kubwa na hofu pia.
Kutoka kuwa timu iliyokuwa ikichukuliwa ya kawaida tu kwa sababu ya ligi yake, hadi kuwa miongoni mwa timu zinazohofiwa zaidi barani Ulaya kwa sasa.
PSG wamebadilika kabisa tofauti na namna watu walivyokuwa wanaitazama miaka kadhaa ya nyuma hapo.
βοΈNeves
13/08/2026
Unai Emery amepoteza fainali zote 4 za UEFA Super Cup alizocheza.
β 2014: Alifungwa 2-0 na Real Madrid
β 2015: Alifungwa 5-4 na Barcelona
β 2021: Alipoteza kwa penalti 6-5 dhidi ya Chelsea
β 2026: Alifungwa 2-1 na PSG
Michezo 4, vipigo 4. Emery bado hajawahi kushinda UEFA Super Cup alafu anacheka.
13/08/2026
Lionel Messi na klabu yake wameondolewa kwenye hatua ya makundi ya mashindano rasmi kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya maisha yake ya soka huko Marekani.
Inter Miami imeondolewa kwenye Leagues Cup baada ya kufungwa na Club LeΓ³n leo.
12/08/2026
Tangu Liverpool walipobeba Premier League Mei 2025, kikosi chao kimepoteza wachezaji wengi wenye uzoefu na viongozi muhimu.
Trent Alexander-Arnold aliyekuwa nahodha msaidizi na mwenye zaidi ya mechi 350, aliondoka kwenda Real Madrid.
Andy Robertson aliyekuwa nahodha msaidizi wa Virgil van Dijk akaondoka k**a mchezaji huru baada ya miaka 9 na mechi 378, huku Mohamed Salah mmoja wa viongozi muhimu zaidi ndani ya chumba cha kubadilishia nguo nae akaondoka.
Ibrahima KonatΓ© beki wa kimataifa wa Ufaransa aliyefikisha miaka 27 mwezi May tu hapo nae akiondoka.
Kuondoka kwa wachezaji hao ndani ya miezi 12 kumeiacha Liverpool ikiwa na maswali kuhusu ukosefu wa viongozi ndani ya kikosi, hasa baada ya msimu mbaya uliowafanya kumaliza nafasi ya 5 kwa tabu sana.
Usajili wa Ronald AraΓΊjo unaweza kusaidia kuziba pengo hilo kwani mbali na uwezo wake wa uwanjani, akiwa nahodha wa Barcelona, anatarajiwa pia kuleta uzoefu, uongozi na utulivu kwenye kikosi cha Liverpool.
12/08/2026
Alikuwa na umri wa miaka 23 tu na alivaa jezi namba 10 pale Real Madrid kwenye kikosi kilichokuwa na nyota k**a Benzema, Casemiro, Kroos, Cristiano Ronaldo na Bale.
Alifunga mabao 17, akatoa assists 18, na kushinda UEFA Super Cup pamoja na Club World Cup.
Na yote haya aliyafanya katika msimu wake wa kwanza tu akitokea Monaco ya Ufaransa.
Jina lake ni James RodrΓguez.
12/08/2026
Achana na kina Nunez CR7 mwenyewe aliwahi kukosa kufunga bao hapo k**a anavyoonekana kwenye picha.
Tarehe 18 Novemba 2006, Cristiano Ronaldo alikosa nafasi ya wazi kabisa mbele ya goli tupu katika mchezo dhidi ya Sheffield United kwenye uwanja wa Bramall Lane.
Baada ya kipa Paddy Kenny kutoka upande wa wake wa kushoto, Ryan Giggs alimpatia Ronaldo pasi safi ya mwisho, lakini Ronaldo alipiga mpira juu licha ya goli kuwa wazi kabisa.
Pamoja na hayo bado Manchester United ilishinda 2-1, huku Wayne Rooney akifunga mabao yote mawili.
Tukio hili limeendelea kutajwa k**a moja ya worst misses kubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye maisha ya soka ya Ronaldo.
12/08/2026
Baada ya kutocheza hata dakika moja kwenye Kombe la Dunia, NβGolo KantΓ© alirejea moja kwa moja hadi Uturuki kwenda kuipambania klabu yake ya FenerbahΓ§e.
Alirejea, akacheza mechi zote mbili za raundi ya tatu ya kufuzu Ligi ya Mabingwa, na sasa amebakiza mechi 2 tu kurejea kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka la klabu (UCL)
Baada ya miaka 3, KantΓ© yuko karibu sana kucheza tena Champions League.
Licha ya kutocheza hata dakika moja kwenye Kombe lake la Dunia la pili, KantΓ© hakuwahi kumzungumzia vibaya kocha Didier Deschamps.
Aliheshimu uamuzi wa kocha wake, akarudi klabuni na kuanza kazi mara moja kuhakikisha FenerbahΓ§e inarudi Champions League.
Haijalishi unaishabikia timu gani au wewe ni nani ila shabiki wa kweli hawezi kamwe kumsema vibaya NβGolo KantΓ©.πͺ