Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page

Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page

Share

Hii ni Page ambayo tunaitumia kuomba misaada kwa wadau pamoja na shughuli za kituo.karibu utusapoti na kuwawezesha watoto kutimiza ndoto zao.

Photos from Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page's post 03/01/2023

Nawashukuru sana wote mlioshiriki kuhakikisha Ivomapunda Sports&Daycare Centre inaendelea.Nawasihi muendee kuisaidia hata Kwa kushare na wengine waijue shule yetu pendwa.
TUPO KITUNDA MWANAGATI NA TUNAPOKEA WATOTO KUANZIA MWAKA MMOJA MPAKA MITANO(1-5)Tunazingatia ELIMU NZURI NA MALEZI BORA KWA WATOTO (quality Education and Better care) UJI lishe ulio bora na Lunch kwa toto,usafiri Upo bila mashaka..Tumeshaanza kupokea watoto.
0785919363

21/11/2022

Ball To All Ball to All
Thankyou for making our kids happy all the time..

20/11/2022

.sports.center ..
Jamani samahani nimem-tag
MUNGU pekee nyie wengine mtulie kidogo..
Kumbe life style inaweza kukufanya uonekane mzee ama kijana Ndio nimegundua sasa..
Asante Mungu wangu kwa hii NUSU KARNE..Endelea kunipa afya njema kila siku kila saa kila dakika..Wewe ndiye MUNGU pekee ninaekuabudu..wengine watasema naigiza maigizo ila Mungu wangu endelea kunifanya kijana kwa miaka mingine 50 ijayo..Amen..

Pia shikamoo zenu sizitaki maana zitanizeesha😝😝 tuendelee na salamu yetu ile ile ya “kaka mambo?”

Photos from Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page's post 18/11/2022

.sports.center .gro.faidamarambili .
Nawashukuruni wote mnaoendelea kunitumia salamu za siku yangu ya kuzaliwa..Mungu awabariki..
Lakini kwanza nimtangulize “MUNGU” muumba wa vyote anae endelea kunipa uhai na afya bora siku zote na kunifanya niwe kijana miaka yote🙏🙏..
Nawashukuru jamii nzima ya wanasoka,wapenda soka, waandishi wa habari,ndugu na jamaa wote mnaonizunguka ambao mnanifanya niitwe “IVO MAPUNDA”,bila kuwasahau familia yangu woteee..
Hakika nyie wotee mko na thamani kubwa sana kwangu..
Cha muhimu Tuendelee kumtegemea “YEHOVA,ALLAH,”kwa kila jambo letu na tutafanikiwa..
msisahau kwamba tarh 17/12/2022 ni siku ya maafali shuleni kwetu &DaycareCenter wote nawakaribisha..Shule yetu ipo Kitunda Mwanagati-Kichangani unaweza nicheki kwa 0785919363 nikupe maelekezo..

Photos from Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page's post 25/09/2022

.sports.center

KAKA ALLY MAYAI TEMBELE:NAOMBA SISI MARAFIKI ZAKO WOTE TUPIGE CHINI..
Nina kaujumbe kidogo kwako kaka:
Kwanza hongera sana kwa kupewa jukumu zito la kuongoza michezo nchini.Asilimia kubwa ya wanamichezo wanaimani na wewe kaka..
KAKA mpaka umefika hapo haikuwa rahisi sana ila kutokana na juhudi uthubutu ndio kilichokufanya uwe Ally Mayai.
KAKA tabia yako hakuna asiyefahamu kwamba wewe ni mpole,mtu wa watu,una roho ya huruma na kupenda kusaidia,,hicho Mungu amekupendelea sana na huna budi kumshukuru..
KAKA kwa jinsi ulivyo umejitengenezea marafiki wengi sana WAZURI NA WABAYA..
hivyo unapaswa kujua rafiki yako mwema ni yupi kwa sasa..na mbaya ni yupi..
KAKA wapo watakosema kwamba Ally Mayai nimecheza nae mpira na kusota kwenye maisha hiyo
najua tu atanibeba kwenye shida na raha japo hana ujuzi wala taaluma aliyosomea kisa tu ni rafiki yako ..
Wapo watakao kuletea umbea ili mradi wapate kile wanachokusudia na waonekane eti ni WEMA kwako..
Wapo watakao jifanya MACHAWA WAKO ili tu wapate nafasi..
Wapo watakao kuja na kujifanya wanaujua sana kuuongelea mpira japo hata hajawahi kucheza…
Kaka naomba sana sisi wote TUPIGE CHINI maana tutakuwa chanzo cha wewe kushindwa kutimiza wajibu wako..
Ili uweze kuwa huru na salama hawa watu wote hawapaswi kukuzunguka kwani watakufanya uonekane si chochote si lolote kwa waliokuamini..Baadae haohao ndio watakuwa mbelembele kukuzodoa pale unapokwama..
Kaka ulikiri mwenyewe kwamba “huwezi ijua kesho yako” na kesho yako ndio hii..nenda kawatumikie wananchi achana na “MASAMJOSAMJO” wa mpira..
Wanaojua mpira unawajua na wasiojua mpira unawajua pia…
Kaka Mimi niishie hapa ntakuja tena siku nyingine…Asante!!
.96

Photos from Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page's post 24/09/2022

.sports.center

ALLY MAYAI SISI MARAFIKI ZAKO WA KARIBU TUPIGE CHINI WOTE ILI UFANYE KAZI YAKO VIZURI KAKA.. ujumbe wangu kwako ni mfupi sana kaka…
Kwanza hongera sana kwa kuaminiwa na serikali kuongoza taasisi nyeti..
Lakini pia mshukuru Mumgu kwakuwa huwezi jua kesho yako na hilo pia umekiri kwa kinywa chako..
Umetutoa kimasomaso wana soka hasa ambao tulikuwa tuna ndoto kuona wakongwe *marijendari* tunapata nafasi kuongoza mchezo huu…Naamini mnapokuwa wengi ktk hizi nafasi basi maendeleo ya kukua kwa mchezo huu yanakuwa mepesi..Kwa kushirikiana na wakongwe wengine ambao wamecheza mpira mfano akina na wengine wengi.
KAKA..kwa tabia yako ambayo Mungu amekujaalia, wewe ni mpole sana na mtu wa watu na marafiki lukuki hakuna ambae atabisha juu ya hilo..Na kwatabia yako umejijengea uaminifu na nafasi kubwa kwa watu na hatimae kukuamini kwa kiasi kikubwa sana..Kwa tabia yako kaka umejitengenezea marafiki WEMA na WABAYA..ambao huenda usiwajue haraka sana..
Lakini Mimi wacha nikutonye na marafiki wabaya..Ni wale ambao tutakuja kwako na maneno mengi,kukusifia kukukumbusha mambo ya zamani ambayo tumefanya wote tuki haso mtaani hata maofisini k**a ambavyo nimekuja mimi na picha za zamani tukiwa kwenye kutafuta..Watakuja wengine wakikupa ushauri juu ya majukumu yako unayoenda kufanya..Wengine watakuja na maneno ya umbea ili waonekane wanakupa siri na baadae wachukue nafasi@ojawapo..Wapo wengine wengiii ambao watajisifia kwamba umecheza nao mpira na watakapo kushauri wanaamini utawasikiliza..Muda wa wale ‘MACHAWA’ kujisogeza ndio huu..Wale “MASAMJOSAMJO”ambao wanajifanya wanajua kuusemea mpira na hawajacheza kumbe wanayasemea matumbo watakuja lakini PIGA CHINI..
KAKA naomba sisi wote tupige CHINI maana hatukutakii mema kwenye majukumu yako..tunatakuharibia kibarua chako..Na kibarua kikiharibika tutakuja tena na maneno ya kukukejeri …Umefanya kazi kubwa sana kutengeneza jina sasa fanya juu chini kuwapiga chini watakao haribu jina lako..Wapo tunaodhani kwamba wewe kuwepo hapo ndio urahisi wetu kupata tunachokitaka hata k**a hatujapitia au kusomea taaluma hii kisa tu kwamba wewe nakujua ama tu kwamba tumecheza wote mpira..
KAKA sisi watu wa namna hii TUPIGE CHINI..
KAKA Mimi niko na mambo mengi sana ya kukutonya ila wacha niishie hapa..
Nenda katatue shida za wapenda soka ili uendelee kuacha “LEGACY”
Hili ni # .96

Photos from Ivomapunda.Sports.Centre Fun’s Page's post 21/09/2022

.sports.center BREAKING NEWS: Naomba niwape hii taarifa:Nikwamba tuna vitu viwili tofauti yaani IVOMAPUNDA.SPORTS.CENTER ambacho ni kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji.Tunapokea watoto chini ya miaka 14 wa kike/kiume..Kituo chetu kipo Mwanagati-Kwamfipa
Lakini pia tuna shule ya awali ambayo inaitwa IVOMAPUNDA SPORTS&DAYCARE CENTER.Tunapokea watoto kuanzia mwaka 1.5 - 5 na shule yetu ipo Mwanagati-Kichangani huduma zetu ni mzuri.. Jamani tupende vya kwetu waleteni watoto kwenye taasisi yetu..
.96 @

25/08/2022

.sports.center .light.31508076
TAFAKULI:Huwa najiuliza sana…🤔 Kwa nini nakuwa mwepesi wa kutoa michango ya harusi/sendoff kuliko kutoa sadaka kanisani?..Kwa nini nakuwa mwepesi wa kuhudhulia vikao vya harusi/tamasha la muziki/arobaini n.k? Lakini nakuwa siwezi kuhudhulia mikutano/makongamano ya kanisani?..Nakuwa wa kwanza kutoka ktk lbada kabla ya kiongozi wa ibada..Lakini nakuwa wa mwisho na mwenye kuichungulia pesa wakati wa kutoa sadaka?
…Nimegundua kumbe maisha yangu yanahitaji sana nguvu ya Mungu zaidi ndani yangu ili niweze kuepuka majaribu yote haya..
JE WEWE UMESHAWAHI KUWAZA LOLOTE JUU YA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU WETU..Au na wewe ni ili mradi kunakucha?
.Tafakari🤔

12/07/2022

.sports.center

USIPANGE KUIKOSA HII...
Mimi nitakwepo je wewe🤷‍♂️🤷‍♂️
Asante Baba yangu wa kiroho...
Tukutane Matembele ya pili Kivule kwa Baba Chief

11/06/2022





Timu ya Taifa ya walemavu TEMBO WARRIORS Tupo Poland kwa ajili ya mechi za kirafiki na leo ndio ufunguzi nchi sita washiriki wa Mashindano hapa mji wa Warsaw.Dua zenu waTanzania kwa vijana hawa wanaopeperusha bendera hapa Poland.Mechi Hizi ni maadalizi ya kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu yatakayofanyika Uturuki mwezi wa kumi mwaka huu.


29/05/2022

.sports.center
Mtwara Mtwara Mtwara Mtwara
Kumekuchaaaa!!!!Nabii Suguye anakuja huko….Je Tupo tayari??? Ni wakati wako sasa ambapo unaenda kupata uponyaji wako wa kiroho,shida mbalimbali zina enda kuisha kupitia mtumishi wa Mungu Prophet Nicolaus Suguye. atakuwa Mtwara viwanja vya sabasaba kuanzia tarehe 15-19-June-2022 saa 8:00 mchana.Mkutano utapanbwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za lnjili na wengine weeeeengiii…
Baba, Mama Njoo na familia yako yote,Mimi Pia nitakwepo katika kumtukuza Mungu wetu kwa mambo mengi aliyonitendea Njoo tuungane katika mkutano huu mkubwa wa aina yake na wamaajabu….

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Mwanagati
Dar Es Salaam