Liverpoolfc kopites Tanzania

Liverpoolfc kopites Tanzania

Share

Karibu kwenye ukurasa wa mashabiki wa Liverpool FC Tanzania. Tufollow usikose taarifa muhimu za liverpool....YNWA ❤️ | #KopitesTanzania

Unaokuletea habari za usajili, mechi, matokeo, taarifa rasmi, mijadala na matukio mbalimbali yanayohusu Liverpool FC. Ukurasa huu ni kwamahususi kwa habari/mijadala/mada/ kutoka Timu ya liverpoolfc, Page hii inasimamia na kijana mtanzania shabiki wa Liverpoolfc, Page hii itatumia lugha ya kiswahili 99% ilikufikisha ujumbe kwa mashabiki wa Liverpoolfc wa hapa nyumbani na nje ya Tanzania zaidi ...

08/08/2026

Mundo Deportivo inareport kwamba chaguo la kumnunua limewekwa kuwa €55M kwa Ronald Araujo, Liverpool inaripotiwa kufidia 100% ya mshahara wake.

05/08/2026

Kwa mujibu wa ripoti ya DaveOCKOP, ikinukuu mwandishi wa L'Équipe, Loïc Tanzi, Bradley Barcola ameripotiwa kukubaliana masharti binafsi ya mkataba na Liverpool. Hata hivyo, makubaliano kati ya Liverpool na PSG kuhusu ada ya uhamisho bado hayajakamilika, na ndiyo hatua muhimu iliyobaki kabla ya dili kukamilika.

24/07/2026

BREAKING 🚨

Real Madrid wameingia rasmi kwenye mbio za kuwania kumsajili Yan Diomande kutoka RB Leipzig, kwa mujibu wa David Ornstein. Hii inaongeza ushindani mkubwa kwenye dili ambalo Liverpool wamekuwa wakilihusishwa nalo kwa kipindi chote cha dirisha hili la usajili, huku PSG ikitajwa kuwa ilikuwa inaongoza mbio hizo katika wiki za hivi karibuni.

Kwa sasa, mbio za Diomande zinahusisha vilabu vikubwa vya Ulaya, na hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa. Liverpool bado wanatajwa kuwa miongoni mwa wanaomfuatilia kwa karibu, lakini sasa Real Madrid wameongeza presha kwenye vita ya usajili wake.

24/07/2026

🚨 TAARIFA ZA DHARURA: Liverpool yahamia kwa Bradley Barcola! 🔴

Liverpool inaendelea na juhudi za kumsajili winga wa PSG mwenye umri wa miaka 23, Bradley Barcola. Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo wa Ufaransa kwa sasa hana mpango wa kusaini mkataba mpya na PSG na anatamani kuhamia Ligi Kuu England. Arsenal pia wanamfuatilia, huku Bayern Munich wakiendelea kufuatilia kwa karibu.

Hata hivyo, dili hili halitakuwa rahisi. PSG wanatajwa kumthamini Barcola kwa kiwango kikubwa sana, hivyo Liverpool italazimika kuvunja benki ikiwa itataka kumleta Anfield.

Je, ungemkubali Bradley Barcola kuwa mrithi wa Mohamed Salah pale Anfield? 🔥👇

23/07/2026

Liverpool wanatarajiwa kupokea takribani dola milioni 2.2 za Marekani (sawa na pauni milioni 1.66) kutoka FIFA k**a fidia ya wachezaji wao walioshiriki Kombe la Dunia la 2026, jambo linalowaweka katika nafasi ya 15 kati ya klabu zote zitakazolipwa.

Kwa ujumla, klabu za Ligi Kuu England (Premier League) zilichangia takribani asilimia 13 ya wachezaji wote 1,248 walioshiriki kwenye michuano hiyo—idadi kubwa zaidi kuliko ligi yoyote duniani. Kutokana na mchango huo mkubwa, klabu za Premier League zinatarajiwa kupokea sehemu kubwa zaidi ya fedha za fidia zinazotolewa na FIFA.

21/07/2026

🚨🔴 BREAKING: Liverpool imeonyesha nia ya kumsajili Ferran Torres, nyota wa Uhispania na mshindi wa Kombe la Dunia. 🏆🇪🇸

Kwa mujibu wa Loïc Tanzi wa L'Équipe, The Reds wameanza kuangalia uwezekano wa kumnasa Torres

Ferran Torres, sasa ameibuka kwenye orodha ya Liverpool huku PSG nayo ikionyesha nia hiyo ya kuhitaji hutuma yake ..

Kwenye kikosi cha Liverpoolfc anafaa ..?

19/07/2026

🚨 Taarifa Mpya: Liverpool yakaribia kukamilisha usajili wa kiungo chipukizi Samuel Martinez. 🔴🇨🇴

Liverpool inatarajiwa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Colombia, Samuel Martinez, kwa ada ya takribani Pauni 750,000.

Baada ya usajili kukamilika, Martinez ataendelea kuichezea Atletico Nacional kwa msimu ujao ili kuendelea kupata uzoefu, kabla ya kujiunga rasmi na Liverpool majira ya kiangazi mwaka ujao.

Katika kipindi hicho cha miezi 12, Liverpool itakuwa na mchango katika kufuatilia na kuelekeza maendeleo yake ili kuhakikisha anajiandaa vyema kwa hatua inayofuata ya maisha yake ya soka.

Aidha, picha zinaonyesha Martinez akiwa njiani kuelekea Uingereza kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya kabla ya usajili kutangazwa rasmi. 🇨🇴✅

🗞️ Chanzo: James Pearce
📸

17/07/2026

🚨 RASMI: Dominik Szoboszlai amesaini mkataba mpya na Liverpool utakaodumu hadi Juni 2031. 🔴✍🏼

Kiungo huyo raia wa Hungary sasa amejiunga na kundi la wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi ndani ya klabu, jambo linaloonyesha jinsi Liverpool inavyomthamini k**a nguzo muhimu ya timu ya sasa na ya baadaye.

Taarifa rasmi kutoka klabuni inatarajiwa kutolewa hivi karibuni.

SZOBO HABAGUIKI. 🔐🇭🇺❤️

16/07/2026

🎉 Facebook recognized me as a consistent post creator this week!

16/07/2026

🚨 Taarifa Kubwa: Dominik Szoboszlai amefikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na Liverpool utakaodumu hadi Juni 2031. ❤️🇭🇺

Makubaliano ya awali tayari yamekamilika, huku Szoboszlai akionekana kuwa mchezaji muhimu kwa mafanikio ya sasa na ya baadaye ya klabu.

Pande zote zimekubaliana kuhusu muundo wa mkataba mpya, na kinachosalia ni kukamilisha baadhi ya taratibu kabla ya tangazo rasmi. Hakuna shaka kuhusu dili hili—kila kitu kiko tayari.

SZOBOSZLAI ANABAKI ANFIELD! 🔥🔴
HERE WE GO! 💣

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Kunduchi
Dar Es Salaam