01/11/2023
Ijue orodha ya vilabu vitano maarufu kutoka Afrika ndani kwa mwezi Oktoba 2023!
👍😄😍⤴💬
1. 5,48M
2. 4,36M
3. 3,22M
4. 3,11M
5. 2,69M
Credit: Deporfinanzas
📣 Tunakuletea Soka Business! ⚽️
Fuatilia ukurasa unaoelezea masuala ya biashara ndani ya soka
01/11/2023
Ijue orodha ya vilabu vitano maarufu kutoka Afrika ndani kwa mwezi Oktoba 2023!
👍😄😍⤴💬
1. 5,48M
2. 4,36M
3. 3,22M
4. 3,11M
5. 2,69M
Credit: Deporfinanzas
01/11/2023
Sponsorship 📢
Klabu ya Simba Sc imeingia Mkataba wa udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) kupitia kinywaji chake cha Pilsner Lager.
27/10/2023
Orodha ya vilabu kumi vilivyo na thamani kubwa ya udhamini wa mbele kwenye jezi zao.
Thamani ya Mkataba wa Barcelona na kampuni ya kupakua muziki mitandoni ya Sportify 🔥
Imeletwa kwenu na Sports Business Institute Barcelona kinachotoa Masters in Sports Management kwa gharama nafuu kabisa. Jiunge nao sasa kuleta mapinduzi ya Soka duniani.
Football is Branding!
22/10/2023
SB Makala: Florentino Perez 😎
Huenda maana halisi ya Football Business ikawa ni namna Real Madrid inavyofanya vyema katika biashara ya soka duniani.
Na hii ni kutokana na mapato yao kwa msimu uliopita 2022/23 yenye thamani ya £843 Milioni kuwa bora kuliko vilabu vingine vikubwa duniani.
Na hii yote ni kwa usimamizi mkubwa wa raisi wao Florentino Perez, wengi tukimwiita Don Perez kutokana na wasifu wake mkubwa katika utendaji kazi wa mipango na mikakati yake.
Na leo SokaBusiness tunakuletea Makala maalumu kuhusiana na Florentino Perez.
Twende pamoja!
Ni mwezi Machi 8, 1947 alizaliwa jijini Madrid yalipo makao makuu ya Hispania.Kihistoria ni Mwanasiasa wa zamani akishikilia nyadhifa mbalimbali k**a uwaziri wa utalii,mawasiliano na uchukuzi. Pia kukaimu nafasi ya unaibu waziri wa viwanda na kilimo nchini Hispania kabla ya kuhamia katika soka.
Perez ni mfanyabiashara aliye na taaluma ya uhandisi wa ujenzi. Amejihusisha na kampuni ya ujenzi ya Grupo ACS tangu ilipoanzishwa mwaka wa 1997 na sasa ni mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji.
Mwanzoni ndoto ya Perez katika kuiongoza Real Madrid haikutimia kwakuwa alishindwa katika uchaguzi wa urais mnamo 1995 na Ramon Mendoza.
Lakini mnamo mwaka 2000, katika uchaguzi mwingine wa uraisi Perez alitumia fursa ya hali duni ya kifedha ya Real Madrid na kupotea kwa ushindani wao dhidi ya mahasimu wao Barcelona kwa kuahidi kuboresha muundo wa uongozi na akaahidi kusajiliwa kwa wachezaji wa hali ya juu akiwemo Luis Figo wa Barcelona wakati wa kampeni yake.
Na hii ilimsaidia kushinda uchaguzi kwa kupata asilimia 94.2 ya kura na kisha kutimiza ahadi yake kwa kumnunua Figo kutoka kwa mpinzani wao mkuu kwa ada ya rekodi ya dunia wakati huo.
Kuwasili kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kulizua mtindo wa kusajiliwa kwa Galacticos katika uongozi wake ambayo ni pamoja na ununuzi wa nyota wengine hadi sasa k**a Zinedine Zidane, Christiano Ronaldo, David Beckham, Michael Owen ,Gareth Bale, Karim Benzema,Eden Hazard , Luka Modric ,Jude Bellingham na wengineo.
Na hiii imemfanya chini ya utawala wake kuifanya Real Madrid kubeba mataji mengi makubwa k**a mataji sita ya UEFA champions league, sita ya Kombe la dunia la vilabu,matano ya European Super cup, sita ya La liga , matatu ya Copa del Rey na sita ya Spanish super cup.
Na huyo ndiye Don Perez ambaye kulingana na jarida la Forbes 2023 inakadiriwa ana utajiri wenye thamani ya $2.3 Bilioni unaomfanya kuwa bilionea nambari 1434 duniani.
Utajiri wake umepatikana hasa kutokana na maslahi yake ya kibiashara katika sekta ya ujenzi.
BUSINESS IS DON PEREZ!
16/10/2023
Jinsi muundo wa kibiashara ndani ya Bundesliga unavyofanya kazi.
Ni Bundesliga ya Ujerumani,moja kati ya ligi bora sana za kandanda ikiwa ina nyota bora na wenye thamani sana duniani k**a Harry Kane, Jamal Musliara, Sebastian Haller, Manuel Neur na wengineo.
Hii inathibitishwa na CEO wa bodi ya Bundesliga, bwana Christian Seifert anasema “Bundesliga inafanikiwa katika mgawanyiko kati ya utendaji wa kiwango cha juu wa michezo na muundo wa kibiashara.”
Katika uchanganuzi wa sheria za Bundesliga zinaonesha utawala na usimamizi wa fedha husimamiwa zaidi katika namna bora ya vilabu ndani ya Bundesliga kutengeneza miundo sahihi ya kibiashara katika kuwavutia mashabiki.
Kupitia Mtazamo wa kimantiki wa utawala wa soka na fedha ndani ya Bundesliga unaonesha kuwa wanatumia 51% pekee ya mapato yao kwenye mishahara na gharama zingine tofauti na vilabu vya Premier League vinatumia 70% ya mapato yao kwa mishahara na gharama zingine.
Bundesliga ina nia ya kuliweka soka lao katika mazingira ya kisasa Zaidi na ili kuhakikisha jambo hili linawezekana wameweka ubunifu katika mikataba ya kibiashara na ushirika. Mfano katika Uuzaji wa haki miliki za majina ya uwanja wa vilabu k**a Allianz Arena wa Bayern Munich,
Hii ni ngumu kwa baadhi ya ligi ama vilabu vingine kukubali mabadiliko ambayo yanakinzana na mila na historia japo mabadiliko haya yanaleta pesa ndani ya klabu. Mfano Makadirio yanaweka thamani ya haki miliki za chapa ya uwanja wa Manchester United ,Old Trafford kuwa ni zaidi ya £600,000,000, lakini ni ngumu kwa wamiliki wao Familia ya Glazers kusaini ushirika na taasisi zingine katika umiliki wa brand ya uwanja huo kutokana na mila na desturi zao.
Pia Miundo ya kibiashara ndani ya Bundesliga inazingatia kanuni na sheria zinazoweza kuonekana k**a njia rahisi ya kuepuka matatizo ya kifedha. lakini ligi k**a vile Premier Leagua hazina sheria wala vizuizi kuangalia kuhimiza vilabu katika matumizi.
Katika muundo wa kibiashara ndani ya Bundesliga pia kuna sekta ya masoko ya kimataifa. Mfano Bayern Munich ilifungua tawi la ofisi ya Marekani mnamo Aprili 2014 katika jitihada ya kuendeleza masoko yao ya kimataifa na walianza ziara ya nchi hiyo majira ya pre-season.
Pia Borussia Dortmund wamechukua hatua za majaribio katika soko la Marekani kwa kushirikiana na pande mbili; Cincinnati United na La Roca katika masoko yao hata kupata wachezaji kanma Gio Reyna, Givens na wengineo wenye vipaji vya hali ya juu.
Kiukweli Bundesliga imetengeneza muundo mzuri sana wa kibiashara kwa vilabu vyake na hii inaifanya kua moja ya ligi yenye ushawishi duniani. Ikiibua msisimko na ushabiki mkubwa kwa soka la ujerumani lenye kutumia kasi na nguvu nyingi.
FOOTBALL IS BUNDESLIGA!
15/10/2023
Ni nani atawapokonya Glazers umiliki wao ndani ya Manchester United?
Jana Sheikh Jassim alitoa oda mara mbili ya dola bilioni 3.5 kwa familia hiyo ili kukamilisha mchakato.
Wakati huo huo akipanga kutoa dola bilioni 1.5 ili kuweza kufanikisha masuala ya usajili nje ya ununuzi wa klabu, ambapo jumla ingefika dola bilioni 8.5.
Lakini bado ikawa ngumu, na akaamua kujitoa.
Sasa zimebaki jitihada za Sir Jim Ratcliffe kununua asilimia 25 ya hisa za Man United zitapigiwa kura hivi karibuni 🔴
Mpango huo unatazamwa k**a hatua ya kwanza ya uchukuaji wa hatua kwa hatua - utapigiwa kura kwenye mkutano wa bodi siku zijazo
Unajisikiaje kuhusu Ratcliffe kuwa mmiliki mpya? ✨
14/10/2023
Sponsorship 💰⚽🔥
Shirikisho la mpira wa miguu Africa (CAF) limeitangaza rasmi VISIT SAUDI k**a wadhamini wakuu wapya wa michuano mipya ya African Football League ambayo inatarajia kuanza October 20, 2023 na kuisha November 11, 2023.
-Timu shiriki zote nane (Al Ahly, Wydad, Esperance, Mamelodi, Simba, Petro de Luanda, TP Mazembe na Enyimba) zitapewa dola 1,000,000 (zaidi ya bilioni 2.5) k**a timu kushiriki kuanzaia hatua ya robo Fainali.
Iwapo timu itafuzu nusu fainali zitapata ongezeko la dola 700,000 (bilioni 1.75)
Bingwa wa mashindano ya African Football League 2023 atapata ongezeko la dola 2,300,000 (bilioni 5.75) kutoka nusu fainali na kuwa na jumla ya dola 4,000,000 (bilioni 10)
Huku mshindi wa pili atapata ongezeko la dola 1,300,000 (bilioni 3.25) na kuwa na jumla ya dola 3,000,000 (bilioni 7.5).
10/10/2023
Sponsorship 📢
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ("CAF") na kampuni ya michezo ya PUMA wamesaiini makubaliano ya udhamini wa kiufundi kwa Matukio kadhaa ya CAF ikiwemo michuano ya TotalEnergies CAF Africa Cup of Nations Côte d'Ivoire 2023.
Makubaliano hayo yataanza rasmi tarehe 1 Novemba 2023 na PUMA itatoa mpira rasmi wa mechi kwenye mashindano ya CAF, na pia kutoa vifaa kwa waamuzi na kushiriki katika fursa kadhaa za uuzaji, ndani na nje ya uwanja.
CAF na PUMA watazindua mpira rasmi wa mechi ya TotalEnergies CAF Africa Cup of Nations Cote d'Ivoire 2023 kwenye Droo ya Fainali siku ya Alhamisi tarehe 12 Oktoba saa 19H00 GMT.
09/10/2023
Social Media Analytics 📊
Vilabu 5 bora vya kandanda barani Afrika kwenye wakati wa Septemba 2023!
Jumla ya mwingiliano💙💬
1. 13,9M
2. 8,87M
3. 6,39M
4. 6,00M
5. 5,70M
Credit : Deporfinanzas