in boxing you create a strategy to beat each new opponent, it's just like chess
Kilindo Boxing Club
Mchezo wa ngumi (Boxing) ni aina ya michezo ya mapigano ambapo mabondia wawili wanapigana kwa kutumi
Ngumi Ulingoni, Punguzeni Mbwembwe..
23/06/2022
15/06/2022
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Afrika ( WBF) limesema kuwa Bondia kutoka Tanzania Twaha Kiduku ni Bondia namba nne kwa Ubora Afrika uzani wa Super Middleweight
1. RYNO LIEBENBERG (38) πΏπ¦
2. ISAAC CHILEMBA (35) π²πΌ
3. SENA AGBEKO (30) π¬π
4. TWAHA KIDUKU (30) πΉπΏ
Ikumbukwe tu Twaha Kiduku mpaka sasa ana jumla ya mapambano 28 na ana nyota mbili huku akiwa anashika nafasi ya 96 kidunia kati ya mabondia 1,373
09/06/2022
Bondia Hassan Mwakinyo ameporomoka kwa nafasi 16 kwenye viwango vya ngumi za kulipwa vya dunia sanjari na kupoteza nusu nyota.
Bondia huyo namba moja nchini ametajwa kuwa wa 33 duniani kwenye uzani wa super welter.
Awali Mwakinyo ambaye sasa anaishi Marekani alikuwa nafasi ya 17 mwenye nyota nne, akihitaji nyota moja kuingia kwenye orodha ya magwiji wa ndondi wa dunia wenye nyota tano wakitofautiana pointi.
Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa duniani (Boxrec), Mwakinyo sasa ana nyota tatu na nusu.
Baada ya video iliyosambaa ikimuonyesha bondia wa Afrika Kusini aliyefahamika kwa jina la Simiso Buthelezi, kumuacha mpinzani wake na kupigana na hewa, bondia huyo amefariki dunia kwa kilichothibitishwa kuwa ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipambana na mwenzake Siphesihle Mntungwa kuwania taji la WBF All Africa uzani mwepesi siku ya Jumapili mjini Durban, lakini pambano hilo la raundi 10 lilisitishwa na mwamuzi baada ya Buthelezi kuonekana kupigana na kivuli cha mpinzani asiyeonekana.
Picha za pambano hilo zilimuonyesha Mntungwa akianguka kupitia kamba na kisha, baada ya pambano hilo kuanza tena, Buthelezi alisonga mbele kuelekea kwenye kona tupu ambapo aliendelea kurusha ngumi.
Mntungwa alitangazwa mshindi na baadaye Buthelezi alianguka na kukimbizwa hospitalini. Aliwekwa katika hali ya kukosa fahamu baada ya kugundulika alikuwa anavuja damu kwenye ubongo.
Shirikisho la mchezo wa ndondi Afrika Kusini (BSA) lilithibitisha kuwa Buthelezi alifariki Jumanne jioni katika taarifa iliyotolewa kwa pamoja na familia ya bondia huyo.
Piga Nikupige π€π€
Maajabu katika Ring
Funny Coacher π
Usiige Mwanangu Utaumia kwa Makocha wa Kibongo..
Sparring π€Ό
Ngumi Moja Haina Ushindi, Combination Muhimu kwa Boxer katika Fight βπ€
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Website
Address
Dar Es Salaam