Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imeendelea kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote wa mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ili kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyowekwa.
Profesa Mbarawa amesema hayo leo Mei 13, 2026 wakati akihitimisha hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi Bungeni jijini Dodoma.
Amesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeendelea kufuatilia utekelezaji wa mradi huo katika vipande vyote kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na ya uhakika ya usafiri wa reli.
“Kuhusu kasi ya ujenzi wa SGR, Serikali kupitia TRC imeendelea kuwasimamia wakandarasi wote wa mradi huo kwa karibu ili kuhakikisha miradi inatekelezwa na kukamilika kwa mujibu wa mikataba iliyosainiwa pamoja na kuzingatia viwango vya ubora,” amesema Profesa Mbarawa.
Aidha, Waziri huyo amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kimkakati ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unaenda kwa kasi inayokusudiwa.
Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora na kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka, Profesa Mbarawa amesema mkandarasi wa vipande hivyo ameendelea kusisitizwa kuongeza kasi ya utekelezaji ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati.
Amesema Serikali pia imeielekeza kampuni ya Yapi Merkezi kushirikiana na wakandarasi na wazabuni wengine kwa kuwapatia baadhi ya maeneo ya kazi ili kuongeza nguvu ya utekelezaji wa mradi huo.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, hatua hiyo tayari imeanza kuonyesha mafanikio katika vipande vya Makutupora hadi Tabora pamoja na Tabora hadi Isaka.
Profesa Mbarawa amesema hadi kufikia Machi 2026, ujenzi wa reli ya SGR katika kipande cha Makutupora hadi Tabora chenye urefu wa kilomita 368 na kipande cha Tabora hadi Isaka chenye kilomita 165 ulikuwa ukiendelea, licha ya kuwepo kwa changamoto zilizokuwa zikisababisha kasi ndogo ya utekelezaji kwa muda mrefu.
Hata hivyo, amesema Serikali tayari imepata suluhisho la kukamilisha ujenzi huo baada ya kupata mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya do
Kasimpya Digital
Ukurasa huu ni Kwa ajili Habari,Michezo na matukio mbalimbali Utapata Habari zote za Ndani na Nje ya Nchi
Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar, Mariam Said Khamis ameipongeza Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuendelea kuboresha huduma za usafiri wa reli ya kisasa ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi bungeni, Mariam amesema TRC imefanya kazi kubwa katika kurahisisha usafiri wa wananchi, akibainisha kuwa kuanzia Julai hadi Machi mwaka huu zaidi ya abiria milioni 2.5 wametumia huduma hiyo.
Amesema mafanikio hayo yanatokana na dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mradi wa SGR unakamilika na kuwahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.
“Haya yote ni mapenzi makubwa ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha amekamilisha mradi huu wa kuturahisishia wananchi usafiri wa haraka. Zamani sisi kutoka Zanzibar tulikuwa tunatumia siku mbili kufika Dodoma, lakini sasa tunafika kwa siku moja,” amesema Mariam.
Aidha, amempongeza Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Naibu Waziri pamoja na watendaji wa wizara hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika sekta ya uchukuzi.
Mbunge huyo pia amesema hatua ya TRC kuanza kujitegemea katika kugharamia mishahara, matumizi ya kawaida pamoja na uendeshaji wa huduma ni mafanikio makubwa kwa shirika hilo.
Katika mchango wake, Mariam ameiomba Serikali kuboresha zaidi muda wa safari za SGR kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili safari hiyo ichukue takribani saa tatu, sawa na muda unaotumika kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
“Tunatoka Dar es Salaam saa tatu na kufika Dodoma saa nane, hivyo naiomba Serikali kuboresha safari za kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili nazo ziwe za muda mfupi zaidi,” amesema
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kupata sehemu ya kichwa cha marehemu James Rogers Temba, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha IFM, kilichokuwa hakijapatikana tangu kutokea kwa mauaji yake mwishoni mwa Aprili mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 13, 2026 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, sehemu hiyo ya kichwa ilikutwa ikiwa imefukiwa ardhini katika eneo la Kitunda Kibeberu, wilayani Ilala baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na jeshi hilo.
Polisi wameeleza kuwa jumla ya watuhumiwa watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo, akiwemo Said Ally maarufu k**a “Side”, mwenye umri wa miaka 31, anayedaiwa kuwa mganga wa kienyeji na mkazi wa Kitunda Kibeberu. Taratibu za kisheria zinaendelea kukamilishwa ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi yao.
Aidha, Jeshi la Polisi limewashukuru wananchi pamoja na mamlaka nyingine za uchunguzi wa kisayansi kwa ushirikiano walioutoa ambao umeendelea kusaidia kufanikisha uchunguzi wa tukio hilo.
Polisi pia wametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya dola vifanye kazi zake kwa weledi, huku wakionya dhidi ya kusambaza taarifa za upotoshaji zinazoweza kuchelewesha uchunguzi au kuzua taharuki katika jamii.
Kamanda wa Polisi amesema jeshi hilo linaendelea kulaani tukio hilo baya na la kusikitisha, na kwamba linafuatilia kwa karibu shauri hilo ili kuhakikisha haki inatendeka dhidi ya watuhumiwa wote.
Mwigizaji maarufu wa Nollywood, Alex Ekubo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 40 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Saratani.
Alex alikuwa miongoni mwa waigizaji waliotikisa tasnia ya filamu nchini Nigeria kupitia filamu mbalimbali zilizompatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Afrika.
Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Aboubakar Asenga amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya M. Shiwa kwa usimamizi mzuri wa mradi wa reli ya kisasa ya SGR, akisema mafanikio yaliyopatikana yanaonekana wazi kwa wananchi kupitia huduma bora ya usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Asenga amesema hayo leo Jumatano Mei 13, 2026 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi Bungeni jijini Dodoma.
Katika mchango wake, Asenga amesema Mhandisi Machibya ni miongoni mwa vijana waliobobea katika taaluma ya reli na kwamba amepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uwezo wake wa kusimamia sekta hiyo muhimu ya uchukuzi.
“Huko Shirika la Reli Tanzania yupo kijana anaitwa Mhandisi Masanja Machibya, ni mhandisi ambaye amesomea reli, ameaminiwa na Rais Samia na pia Watanzania wamemuamini. Anafanya kazi kubwa na mafanikio tumepata,” alisema Asenga.
Amesema Watanzania wengi wanakiri kuwa huduma ya treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma imeleta mapinduzi makubwa katika usafiri kwa kuimarisha usalama, kasi na ufanisi wa safari.
Mbunge huyo ameitaka Serikali kuhakikisha inatafuta fedha kwa wakati ili kukamilisha ujenzi wa reli hiyo kuelekea mikoa ya Mwanza na Kigoma, hatua aliyosema itasaidia kuongeza mapato ya nchi pamoja na kufungua fursa za kiuchumi ikiwemo usafirishaji wa makaa ya mawe na bidhaa nyingine.
Asenga pia amewataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono Wizara ya Uchukuzi pamoja na TRC ili kuhakikisha miradi ya kimkakati ya reli inakamilika kwa manufaa ya taifa.
Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa amesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) inaendelea kwa kasi na utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR), huku vipande mbalimbali vya ujenzi vikionesha mafanikio makubwa.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Mei 13, 2026, Profesa Mbarawa amesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, ujenzi wa kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro pamoja na kipande cha pili kutoka Morogoro hadi Makutupora umekamilika kwa kiwango kikubwa.
Amesema sambamba na utekelezaji wa mradi huo, TRC inaendelea kutoa huduma za usafiri katika vipande vilivyokamilika, hatua inayowezesha wananchi kuanza kunufaika na maboresho ya sekta ya reli nchini.
Kwa upande wa kipande cha Mwanza hadi Isaka, Waziri huyo amesema ujenzi umefikia asilimia 68.77 na kazi zinaendelea vizuri.
Aidha amesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, ujenzi wa kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora na kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka unaendelea huku shughuli mbalimbali za utekelezaji zikiendelea katika maeneo hayo.
Profesa Mbarawa amesema baadhi ya vipande vya mradi huo vilikuwa na changamoto zilizochukua muda mrefu kutatuliwa na kusababisha kasi ya utekelezaji kupungua katika hatua za awali.
Hata hivyo amesema Serikali imefanikiwa kupata suluhisho la kukamilisha mradi huo baada ya kupata mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.277, sawa na takribani Shilingi trilioni 3.32.
Hatua hiyo inaendelea kuonesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha miundombinu ya reli nchini kwa lengo la kuongeza ufanisi wa usafiri na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa amesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania imeendelea kuimarisha huduma za usafiri wa reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) kati ya Dar es Salaam na Dodoma, hatua iliyochangia ongezeko kubwa la idadi ya abiria wanaotumia huduma hiyo.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi bungeni, Profesa Mbarawa amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026, jumla ya abiria milioni 2.51 walisafirishwa kupitia reli hiyo ikilinganishwa na abiria milioni 2.05 waliosafirishwa katika kipindi k**a hicho kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Amesema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 22.4, jambo linaloonesha kuendelea kuimarika kwa huduma za usafiri wa SGR pamoja na kuongezeka kwa imani ya wananchi katika matumizi ya reli hiyo ya kisasa.
Aidha, Profesa Mbarawa amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026, TRC ilisafirisha jumla ya tani 102,452 za mizigo kupitia reli ya SGR ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya kuanza rasmi huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa kutumia reli hiyo.
Amesema mafanikio hayo yanaendelea kuonesha mchango wa mradi wa SGR katika kuboresha sekta ya usafiri na usafirishaji nchini pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali haitatoa tena ruzuku ya mishahara kwa Shirika la Reli Tanzania kuanzia mwaka wa fedha 2026/2027 baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa ndani ya shirika hilo tangu mwaka 2017.
Profesa Mbarawa amesema hayo leo Jumatano Mei 13, 2026 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi bungeni jijini Dodoma.
Amesema Wizara inaishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa kuboresha TRC, zoezi ambalo lilianza rasmi mwaka 2017 kwa lengo la kuimarisha huduma za usafiri wa reli nchini pamoja na kuongeza ufanisi wa shirika hilo.
“Tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya mishahara. Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 TRC haitatengewa tena ruzuku kwa ajili ya mishahara kutoka Serikalini,” amesema Profesa Mbarawa.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni ishara ya kuimarika kwa uwezo wa kifedha wa TRC kufuatia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya reli, ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) pamoja na maboresho ya miundombinu ya reli nchini.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia (CHAUMMA) Devota Minja ameishauri Serikali kupunguza gharama za Bima ya Afya kwa wote kwa sababu zipo kaya maskini ambao hawawezi kumudu gharama.
Ametoa ushauri huo leo Mei 12, 2026 wakati akichangia Bungeni mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi, Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Amesema baadhi ya watanzania kiasi cha shilingi laki moja na hamsini ni kiwango kikubwa kwao, hivyo Serikali iangalie namna ya kuwarahisishia.
Bank ya CRDB Leo 12 May 2026 imekabidhi zawadi Kwa washindi mbalimbali,mahindi Wa pili akabidhiwa zawadi ya Inch 85
ndo mpango mzima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere, Mei, 12; 2026 amekuwa miongoni mwa washindi watatu waliopatikana katika droo ya ya awamu ya pili kwa watumiaji wa kwenda nchini Canad kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam