15/05/2026
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄: Kiungo Emam Ashour (28) 🇪🇬 ataondoka katika klabu ya Al Ahly mwishoni mwa msimu huu kwa mujibu wa wakala wake Adam Watani na ameshatangaza hilo kwa Vyombo vya Habari nchini Misiri! 💔😳
Kulingana kwa kutoelewana kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Al Ahly na Wakala wa Emam Ashour kutokana na matukio ya kufungiwa na kupigwa faini kwa Mteja wake Emam Ashour na yamekuwa mengi na watawala wa Al Ahly hawakatai kuondoka kwa mchezaji yeyote, mradi ofa kubwa ya kifedha itolewe na anatajwa kurudi Zamalek SC kwaajili ya msimu ujao wa 2026-27.⭐️🥵
15/05/2026
Jarida maarufu duniani la TIME limemtaja Rais wa Simba SC, Rais wa makampuni ya MeTL Group na Mwanzilishi wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji katika orodha ya TIME100 Philanthropy 2026, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa kwa jamii kwa kugusa maisha ya mamilioni ya Watanzania kupitia miradi ya elimu, afya, maji safi na kusaidia jamii zisizojiweza.
Rais wa timu yetu anatupa furaha ya uwanjani na nje ya uwanja anagusa maisha ya Watanzania wenzetu
15/05/2026
🚨OFFICIAL Kikosi cha Sweden kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026.
15/05/2026
🚩 𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : La Liga 🇪🇸
REAL MADRID CF 2️⃣➖️0️⃣ REAL OVIEDO
⚽️ 44" Gonzalo
⚽️ 80" Bellingham
15/05/2026
🚨🇫🇷 OFFICIAL Kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya kombe la Dunia.
14/05/2026
🚨 BREAKING
Michael Carrick atabakia kwenye klabu ya Manchester United na dili la mkataba mpya lipo kwenye hatua za mwisho..
Kila mtu kwenye klabu kuanzia viongozi hadi wachezaji wanataka Michael aendelee kuwa kocha mpya ndani ya klabu..
Per :Fabrizio Romano
Wanangu wa United vipi, mmefurahia hili dili au litachoma nafsi yako.
Mimi naona Michael hatoshi ,ila tusimalize maneno..
GAFFER 👊
14/05/2026
🚩 𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : Premier League 🏴
MANCHESTER CITY 3️⃣➖️0️⃣ CRYSTAL PALACE
⚽️ 31" Semenyo
⚽️ 40' Marmoush
⚽️ 84" Savinho
14/05/2026
🚨 Baada ya Ushindi wa mabao 5-3 Usiku wa kuamkia Leo dhidi ya Cincinnati kutoa Asisst moja na kufunga mabao mawili Lionel Messi sasa amefikisha mabao 909 kwenye maisha yake ya soka. 🐐
🏟 Michezo - 1153
⚽️ Mabao - 909
🎯 Asisst - 411
⚽️🎯 Mabao/Asisst - 1320
12/05/2026
Klabu ya soka ya Yanga, imetozwa faini ya shilingi milioni thelathini (30,000,000), kwa kosa la wachezaji wake na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kubadilishia jezi kwenye mchezo wa NBC Premier League dhidi ya Simba SC, katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yanga haikutumia chumba hicho rasmi na badala yake ilitumia nyumba iliyopo jirani na uwanja huo ng’ambo ya pili ya barabara inayopita katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo.
Naye Meneja wa klabu hiyo, Walter Harson amefungiwa michezo mitatu na faini ya Shilingi milion moja (1,000,000) kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba SC, Clatous Chama kwenye mchezo huo uliopigwa Mei 3, 2026 na matokeo kuwa sare ya 2-2.
Mwndishi Katherini Shirima
Mhariri |
12/05/2026
🚨 OFFICIAL Desire Doue ameshinda tuzo ya mchezaji bora Chipukizi wa mwaka kwa Wachezaji wa Ufaransa.🇫🇷❤️💙
Inakuwa tuzo yake ya Pili Mfululizo mwaka 2025 na 2026.✨️
12/05/2026
🚨🇫🇷 OFFICIAL Kikosi bora cha Mwaka Lii kuu ya Ufaransa Ligue 1 tuzo za UNFP.