13/01/2026
Ameandika Mchambuzi Alex Ngereza Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram 😁👇
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Michezo Extra, Sports Team, Nangade Sede, Dar es Salaam.
13/01/2026
Ameandika Mchambuzi Alex Ngereza Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram 😁👇
30/12/2025
Klabu ya Simba SC imetambulisha rasmi wataalamu wawili wapya watakaoungana na benchi la ufundi: Davies Phiri k**a kocha wa makipa na Prinil Deen k**a mchambuzi wa video.
Davies Phiri ni golikipa wa zamani wa Zambia ambaye pia amewahi kuwa kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Zambia, huku Prinil Deen akiwa na leseni ya UEFA B na uzoefu wa uchambuzi wa video akiwa ameifanya kazi hiyo katika klabu kadhaa barani Afrika.
Wawili hao wataungana na benchi la ufundi linaloongozwa na Steve Barker kuimarisha kikosi cha Simba katika mashindano yajayo.
30/12/2025
:
Wachezaji wa Yanga SC, M***a Balla Conte na Aziz Andambwile, wanatajwa kuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga na Singida Black Stars kwa mkopo.
Taarifa zinaeleza kuwa jambo hilo tayari limejadiliwa kati ya viongozi wa pande zote mbili, na endapo makubaliano yatakamilika, wawili hao watajiunga na Singida katika dirisha hili dogo la usajili.
30/12/2025
Kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars na timu ya taifa ya Togo, Marouf Tchakei (30), yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Klabu ya Yanga SC.
Taarifa zinaeleza kuwa usiku wa kuamkia leo, uongozi wa Yanga ulimtumia ujumbe maalum wa kumtaka afanye maandalizi ya vipimo vya afya na picha kwa ajili ya utambulisho.
Kocha Mkuu wa Yanga ameripotiwa kuhitaji kiungo namba 10 mwenye uwezo wa kupress na kucheza kwa kasi, ambapo jina la Marouf Tchakei limependekezwa na kupewa kipaumbele.
Muda wowote kutoka sasa, mchakato wa usajili unaweza kukamilika rasmi.
30/12/2025
Muda wowote kuanzia sasa, Klabu ya Yanga inatarajiwa kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa Singida Fountain Gate, raia wa Guinea, Mohamed Damaro Camara (23).
Taarifa zinaeleza kuwa tayari kuna makubaliano kati ya Singida na Yanga kuhusu uhamisho huo, huku mchezaji mwenyewe akiwa amekubali kujiunga na Wananchi.
Kinachosubiriwa kwa sasa ni kusainiwa rasmi kwa mkataba, jambo ambalo linaweza kutokea muda wowote, na kisha Damaro atakuwa rasmi sehemu ya kikosi cha Yanga.
[]
30/12/2025
Klabu ya Young Africans SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Emmanuel Samuel Mwanengo kutoka klabu ya TRA United.
Mwanengo, mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Tanzania, amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Wananchi.
27/12/2025
Tanzania imeendelea kutafuta alama katika Michuano ya AFCON 2025 huku leo wakilazimishwa sare ya 1-1 na Uganda, kwenye mchezo wa pili wa Kundi C. Hii inakuja baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Nigeria.
Je, nini kinaendelea kuikwamisha Taifa Stars?
° Ulinzi wa kusuasua
Japokuwa safu ya ulinzi imeonyesha ukomavu wa kupambana, bado kuna mapungufu kwenye mawasiliano na positioning. Magoli tunayoruhusu ni ya kizembe, hasa katika dakika za maamuzi. Tunaonekana kutojifunza kutokana na makosa ya nyuma.
° Ushambuliaji usio na makali
Tanzania inatengeneza nafasi, lakini inakosa umaliziaji wa uhakika. Hakuna mshambuliaji mwenye “killer instinct”. Tunaleta mashambulizi mazuri, lakini tunashindwa kuyakamilisha.
° Mpango wa kiufundi
Inaonekana tunashindwa kubadilika ndani ya mchezo. Kocha anahitaji kuongeza ujasiri wa kufanya mabadiliko ya kiufundi mapema, hasa pale timu inapokuwa inashindwa kutengeneza presha ya kutosha.
Mchezo dhidi ya Tunisia – Dili la Kufa au Kupona
Kwa hali ya kundi, Tanzania haina namna ila kushinda dhidi ya Tunisia.
Tunisia wana uzoefu mkubwa, lakini wameonekana wakiyumba. Taifa Stars wanahitaji nidhamu ya mchezo, mbinu sahihi na morali kubwa.
Ushindi unaweza kuleta mabadiliko makubwa.
Hitimisho:
Taifa Stars wanahitaji kujitazama kwa jicho la ndani zaidi. Sio tu kujua tunakosea wapi, bali kuchukua hatua sahihi haraka.
Huu ndio wakati wa kuonyesha dhamira halisi ya kwenda mbali katika soka la Afrika.
||
25/12/2025
Leo ni siku ngumu sana kwangu binafsi na kwa familia nzima. 🥺😭💔
Kwa masikitiko makubwa, natangaza kuondokewa na dada yangu mpendwa Cecy Simba.
Cecy alikuwa zaidi ya dada – alikuwa rafiki, mshauri, mtu wa furaha na mwenye upendo wa kweli kwa wote waliomzunguka.
Tumepoteza sauti ya upole, tabasamu la matumaini, na moyo wa kipekee.
Pumzika kwa amani dada yangu Cecy Simba.
Umeacha pengo kubwa, lakini pia kumbukumbu za thamani ambazo hazitafutika.
Tutakuombea, tutakukumbuka.
🕊️💔🕯️ ||
24/12/2025
Ameandika Steve Champion ✍️
Ndiyo, tumepoteza dhidi ya Nigeria — lakini hatukutawaliwa uwanjani. Haibadilishi matokeo, lakini linapotazamwa kwa jicho la kitaalamu, Taifa Stars haikuwa timu ya kubebwa wala ya kubezwa. Tulicheza kwa nidhamu, kwa heshima, na kwa kiwango cha ushindani.
Nigeria ni taifa kubwa kisoka, lina wachezaji waliopo viwango vya juu duniani — akiwemo Victor Osimhen. Lakini dhidi ya Tanzania, hakuwa na nafasi; alikuwa kivuli tu mbele ya ukuta wetu imara ulioongozwa na Bacca na Mwamnyeto. Historia inajirudia — Tanzania daima imebarikiwa kuwa na mabeki thabiti, na kizazi hiki hakijatutoa kwenye mstari huo.
Tunaamini kwenye kundi hili Taifa Stars haitamaliza mikono mitupu. Alama tatu na sare moja ni malengo ya kweli, mengine tumuachie Mungu. Lakini kubwa zaidi, hii AFCON inatufunulia sura mpya ya mpira wetu — Tanzania haiko tena kwenye orodha ya “vibonde”. Tumebadilika. Tunapambana. Na hata tunapopoteza, tunapoteza kwa heshima.
Kwa waliotamani tufungwe au waliosherehekea matokeo mabaya — ni wakati wa kutafakari. Hii timu si ya mtu mmoja. Ni ya taifa. Ni ya Watanzania wote. Kuwabeza wachezaji wetu ni sawa na kulidhalilisha taifa zima. Tunapoteza pamoja, tunashinda pamoja.
Hii si ndoto — dhidi ya Tunisia na Uganda, tutajibu kwa vitendo. Tutarudi tena. Tukiwa thabiti zaidi. Tukiwa wamoja. Na tukiwa na imani kuwa Taifa Stars ni zaidi ya historia ya vipigo — ni sura mpya ya matumaini.
||
22/12/2025
Klabu ya Yanga SC ipo kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo mshambuliaji wa Vipers pamoja na timu ya taifa ya Uganda, Allan Okello (25), kwa ajili ya usajili katika dirisha dogo la mwezi Januari.
Taarifa zinaeleza kuwa Rais wa Yanga tayari amefanya mazungumzo binafsi na mchezaji huyo k**a sehemu ya mpango wa kumvutia kujiunga na Wananchi. Muda wowote kuanzia sasa, chochote kinaweza kutokea iwapo makubaliano yatakamilika.
||
21/12/2025
Sherehe ya Ufunguzi wa AFCON inayoendelea hivi sasa huko Morocco ni ya kupendeza kupindukia. Ni tukio zuri sana kwa soka la Afrika.
Mechi ya kwanza kati ya Morocco na Comoro itaanza rasmi usiku huu saa 4:00 usiku
Kwa sasa, furahia picha hizi kutoka kwenye shamrashamra za ufunguzi.
21/12/2025
Azam Media Group imelaani vikali mfululizo wa matukio yaliyojitokeza leo katika Uwanja wa Dandora jijini Nairobi, Kenya wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya mechi kati ya Nairobi United FC na Gor Mahia FC saa 10:00 jioni, ambapo gari la OB (Outside Broadcast) lilivamiwa na wahuni hivyo vifaa vya Matangazo vilivyokuwepo ndani ya gari hilo kuharibiwa
Wakati Azam Media Group ikiendelea kujitahidi kuinua na kuunga mkono ukuaji wa Ligi Kuu ya Kenya kwa kuhakikisha ligi inaonekana kwa kiwango cha juu kupitia matangazo ya moja kwa moja, matukio k**a haya ya uharibifu si tu kikwazo bali pia yanaonyesha taswira ya kusikitisha ya Ligi Kuu ya Kenya.
Aidha katika uvamizi huo hakuna mfanyakazi wa Azam Media aliyejeruhiwa.
|| Credit Scope Media