13/07/2023
πππ’π‘π ππππ: Klabu ya Yanga imethibitisha kumsajili Winga Maxi Mpia Nzengeli kutoka klabu ya Maniema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Max Mpia Nzengeli (23) raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesaini kandarasi la kuitumikia Young Africans SC mpaka Juni 2025.
Maxi Mpia Nzengeli anamudu kucheza k**a winga wa kulia, winga wa kushoto na kiungo mshambuliaji.
13/07/2023
JONAS MKUDE ATUA YANGA SC
Miaka 13 baada ya kuitumikia Simba SC kiungo mkongwe nchini Jonas Mkude atua Jangwani kwa msimu wa 2023-24.
Nungu nungu mwenye miaka 30 analimudu vyema eneo la kati k**a kiungo mkabaji β¦ sehemu iliyompa sifa kubwa akiwa na wekundu wa Msimbazi na timu ya taifa ya Tanzania πΉπΏ.
Kabla ya kutua jangwani baada ya kumaliza mkataba na Simba SC , alihusishwa na kujiunga na Singida Fountain lakini ni mabingwa wa muda nchini ndio wamefanikiwa kuipata saini ya legendary huyo.
26/05/2022
Unafikiri hii battle itaishaje 28?
04/03/2020
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kuvurumishwa leo Jumatano ya March 4, 2020, ambapo Wana Lambalamba Azam FC, wanawakabili Wekundu wa Msimbazi, Mabingwa wa Nchi, Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 kutokana na ubora wa vikosi vya timu hizo, ambazo zimesheheni nyota kadhaa wakali na wa kigeni.
Azam FC wanasaka ushindi na alama tatu muhimu kwa ajili ya kufuta unyonge wa kufungwa mara kwa mara, vile vile kujiweka sawa katika mbio za kuifukuza Simba katika kuwania taji la VPL.
17/07/2019
Kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara ipi karata yako Kati ya mahasimu wawili ππ
04/06/2017
hongera mabingwa wa uefa champions league
24/05/2017
βNikiwa hapa Brussels kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya nimepata fursa ya kukutana na mwanasoka na kipenzi chetuβ β Jakaya Kikwete.
http://jidakiss.blogspot.com/2017/05/live-rais-mstaafu-jk-akutana-na-samatta.html
LIVE RAIS MSTAAFU JK AKUTANA NA SAMATTA UBELGIJI
udaku michezo pamoja na magazet
04/05/2017
Jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambazo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.
Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa kampuni ya udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.
Akizungumza na gazeti hili jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwepo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.
Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la Makao Makuu haujafanyika.
"Ni kweli kesi iko katika mahak**a ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi", alisema kwa kifupi Mkwasa, Kocha na Mchezaji wa zamani wa timu hiyo.