23/02/2022
Zedekia emmanuel
Kwa update mbalimbali za michezo ndani na nje ya Tanzania
23/02/2022
22/09/2019
TIMU ya Kagera Sugar imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuwachapa wenyeji, Mbao FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo Awesu Awesu aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 38, kikosi cha kocha Mecky Mexime kikishinda mechi ya tatu mfululizo na zote ugenini.
Hiyo ni baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma kabla ya kuwapiga 2-1 Alliance FC Uwanja wa Nyamagana hapo hapo Mwanza kwenye mechi zake mbilo zilizopita.
22/09/2019
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alikuwa Nahodha wa timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KV Oostende katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Mabao ya Genk usiku wa jana yalifungwa na kiungo Mvenezuela Ronald Vargas aliyejifunga dakika ya 18, mshambuliaji Mnigeria Ebere Paul Onuachu dakika ya 44 na kiungo Mnorway, Sander Berge dakika ya 90, wakati bao pekee la lilifungwa na mshambuliaj Mguinea, Idrissa Sylla dakika ya 32.
Ushindi huo katika mchezo wa nane wa msimu, unawafanya KRC Genk, mabingwa watetezi wa ligi hiyo ya Ubelgiji wafikishe pointi 13 sasa wakilingana na AA Gent ambayo hata hivyo imecheza mechi sita na wanaendelea kushika nafasi ya saba.
24/08/2017
Liverpool yarudi rasmi uefa
TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE 22/08/2017.
1.BRADFORD ya Ligi Daraja La Kwanza England, imemsajili Beki wa kulia Luke Hendrie kwa mkopo kutoka Burnley mpaka January. ( ).
2.BARCELONA imekataa tamaa ya kumsajili Kiungo Mshambuliaji wa Liverpool, Phillipe Coutinho baada ya Miamba hao wa Anfield kusisitiza kuwa nyota huyo wa Brazil "hauzwi". ( ).
3.Klabu ya BRIGHTON imethibisha kumsajili Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Ghana, Raphael Dwamena kutoka klabu ya Fc Zurich hivyo atasafiri mpaka UK kwa ajili ya vipimo ili kuungana na klabu hiyo iliyopanda daraja Ligi Kuu England msimu huu. ( ).
4.MSHAMBULIAJI wa Fiorentina, Nikolas Kalinic yupo katika Viunga vya San Siro kwa ajili ya vipimo vya afya ili kujiunga kwa mkopo na wababe hao wa Milan. Nyota huyo wa Croatia anajiunga na Ac Milan kwa mkopo wa mwaka mmoja kwa dau la pauni €5m(£4.6m), na endapo atafanya vizuri atasajiliwa jumla kwa pauni €20m(£18.3). ( ).
5.KIUNGO wa Inter Milan, Geoffrey Kondogbia yupo mbioni kujiunga na Valencia kwa mkopo haijajulikana ni Mkopo wa muda gani. ( ).
6.KLABU ya Millwall ya Ligi daraja la kwanza England, imempeleka beki wake wa kati Kwa mkopo, Sid Nelson katika klabu ya Yeovil ya Daraja la pili nchini humo mpaka January. ( ).
7.KIUNGO kinda wa Kimataifa wa Algeria na Arsenal mwenye umri wa miaka 19, Ismael Benncer yupo mbioni kuondoka Arsenal ili kujiunga na Empoli ya Italia.( ).
8.KLABU ya Leed United ya Championship inataka kumsajili Mshambuliaji wa Middlesbrough, Rudy Gestede.( ).
9.PLYMOUTH ya Ligi Daraja la kwanza England inataka kumsajili Mshambuliaji wa Celtic, Nadir Ciftci kwa mkopo wa muda mrefu.( ).
10.STOKE CITY inamtaka beki wa Tottenham Hotspur, Kevin Wimmer. ( ).
11.KIUNGO wa Stoke City, Moha El Ouriach amekubali kujiunga na klabu ya Espanyol kwa mkataba wa muda mrefu. ( ).
12.MSHAMBULIAJI wa Leeds United, Chris Wood amejiunga na Burnley kwa mkataba wa miaka minne.( ).
13.MSHAMBULIAJI wa Southampton Sam Gallagher amekubali kujiunga na Birmingham City ya Championship kwa mkopo wa muda mrefu.( ).
14.MSHAMBULIAJI wa Everton, Oumar Niasse anafikiria kujiunga na Fenerbahce kwa mujibu wa tovuti ya ya nchini humo. Mshambuliaji huyo wa Senegal alijiunga na Everton January mwaka Jana kutoka Lokomotiv Moscow ya Urusi kwa pauni £13.5m kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Hull City.
15.KOCHA WA ZAMANI wa England, Steve McClaren amepata kibali ya kuifundisha Klabu ya Maccabi Tel Aviv ya Nchini Israel.( ).
16.KIUNGO wa Real Madrid , Mateo Kovacic yupo tayari kujiunga na wababe wa Anfield, Liverpool endapo Phillipe Coutinho atatimkia Barcelona. ( ).
17.CHELSEA imeweka kiasi cha pauni £91m mezani ikitaka kumsajili Mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti.( ).
18.JUVENTUS & MANCHESTER UNITED zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Kiungo Kinda wa Arsenal mwenye umri wa miaka 18, Marcus McGuane.Manchester City pia wapo kwenye vita hiyo.( ).
19.TOTTENHAM imetenga kiasi cha pauni £20m ili kumsajili Kiungo wa Everton, Ross Barkley. ( ).
20.MANCHESTER CITY itajaribu kwa mara ya mwisho kuwasajili mabeki wawili wa Kati, John Evans kutoka West Brom na Ben Gibson kutoka Middlesbrough kabla ya dirisha la usajili halijafungwa jumatano ya wiki ijayo .( ).
21.PARIS SAINT-GERMAIN imetenga kiasi cha pauni £200m ili kuwasajili mastaa wawili kwa mpigo kutoka Monaco, Kylian Mbappe na Fabinho ambapo kwenye pesa hiyo, Mbappe ataigharimu PSG pauni £128m huku Fabinho pauni £78m.Hata hivyo imeelezwa kuwa PSG itamtaka Mbappe kwa mkopo ili kuukwepa mkono wa FIFA katika harakati za kufuja pesa hasa baada ya kumsajili Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar kwa pauni £200m.( ).
22.KIUNGO wa Juventus Claudio Marchisio ameomba kuondoka katika klabu hiyo ya Turin huku ikielezwa kuwa Bosi wa Chelsea, Antonio Conte anamnyatia Kiungo huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 31.( ).
23.GALATASARAY ya Uturuki inamtaka beki wa,Arsenal, Kieran Gibbs.( ).
24.VALENCIA inamtaka Kiungo wa Manchester United, Andreas Perreira kwa mkopo wa muda mrefu.( ).
25.BAYERN MUNINCH inataka kumrudisha Ujerumani Mshambuliaji wa PSG, Julian Draxler huku Man United, Arsenal na Man City zikimtaka.( ).
26.KIUNGO wa OGCE Nice ya Ufaransa, Jean-Michael Seri amekubali mkataba wa miaka minne ili kujiunga na Barcelona. ( ).
27.MANCHESTER CITY, BURNLEY, WEST BROM na WEST HAM zinamgombea Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ghana na Lorient ya Ufaransa, Abdul Majeed.Nyota huyo ana thamani ya pauni £12m.( ).
28.MSHAMBULIAJI kinda wa Arsenal, Chuba Akpom anatakiwa na Vilabu vya Leeds United na Celtic. ( ).
SIKU NJEMA KWA WOTE!!!!
TRANSFER ZONE.....MONDAY 21/8/2017.
1.ARSENAL imempa ofa mpya Kiungo wake, Alex Oxlade-Chamberlain mkataba wa miaka 4 na mshahara wa pauni £125,000 ili kumzuia asiende Chelsea.Nyota huyo wa England anatakiwa na Boss wa Chelsea, Antonio Conte kwa dau la pauni £40m. ( ).
2.MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United aliyemaliza mkataba wake Mwezi June, Zlatan Ibrahimovic anatarajia kusaini mkataba mpya na miamba hiyo ya Old Trafford wiki hii ili kuongeza nguvu katika safu ya Ushambuliaji ya klabu hiyo...Haijajulikani atasaini mkataba wa miaka mingapi. ( ).
3.CHELSEA inajaribu kutaka kumsajili beki wa Tottenham Hotspurs, Toby Alderweired ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. ( ).
4.MANCHESTER CITY ipo tayari kulipa pauni £300m ili kumsajili Kiungo Mshambuluaji wa Barcelona, Lionel Messi.SuperStar huyo wa Argentina amewekewa kipengele hicho kwa klabu yoyote inayomtaka ambayo itakuwa tayari kutoa pauni £300m. ( ).
5.CHELSEA inataka kumchukua Kiungo wa Poland na PSG mwenye umri wa miaka 27, Grzegorz Krychowiak kwa mkopo baada ya jaribio lao la kumtaka Kiungo wa Leicester City, Drinkwater kuonekana kusuasua. ( ).
6.KOCHA wa Newcastle United, Rafa Benitez anataka kumsajili Mshambuliaji wa West Ham, Andy Carroll na Kiungo Mshambuluaji wa Arsenal, Jack Wilshere ili kuimarisha safu yake ya Ushambuliaji ambayo mpaka sasa haijafunga bao lolote katika mechi mbili za Ligi Kuu England. ( ).
7.LEICESTER CITY imesema kuwa Kiungo wake Mshambuliaji Riyard Mahrez atabaki klabuni hapo kwa msimu mwingine.Nyota huyo alihusishwa na tetesi za kutua Arsenal, Barcelona na As Roma.( ).
8.KOCHA wa Stoke City, Mark Hughes Ana amini kuwa kumpata Mshambuliaji wa PSG, Jesse Rodriguez kutamfungulia milango ya kuwasajili mastaa wenye viwango vya dunia.Kocha huyo amemsajili Jesse kwa mkopo kutoka PSG. ( ).
9.WEST HAM inakaribia kumsajili Kiungo Mkabaji wa Sporting Lisbon, William Carvalho kwa dau la pauni £40m. ( ).
10.KIUNGO wa PSG Goncalo Guedes ametua Katika klabu ya Valencia kwa mkopo ili kupisha usajili mpya wa Mshambuliaji mpya wa Monaco, Kylian Mbappe. ( ).
NAWATAKIA JUMATATU NJEMA!!!
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 19.08.2017
Dau la Barcelona la Pauni milioni 119 la kumtaka Philippe Coutinho limekataliwa na Liverpool. Barca walikuwa tayari kutoa pauni milioni 80, na kiasi kilichosalia k**a nyongeza iwapo Coutinho atashinda Ballon d’Or na makombe mengine. (Mirror)
Barcelona watamgeukia Jean Michel Seri iwapo watashindwa kumsajili Philippe Coutinho, 25, kutoka Liverpool. (SPORT)
Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa Paris Saint-Germain Angel Di Maria. (The Sun)
Monaco wamesema bei ya Kylian Mbappe ni euro milioni 200, huku PSG wakiendelea kumnyatia. (Sky Sport)
Paris Saint-Germain watatangaza usajili wa Kylian Mbappe, 19, kutoka Monaco, kwa euro milioni 180 na kuwa mchezaji wa pili aghali zaidi duniani nyuma ya Neymar. (Mundo Deportivo)
Chelsea wanataka pauni milioni 50 kumuuza Diego Costa, 28, lakini Atletico Madrid wako tayari kutoa pauni milioni 30. (Sun)
Dau la pauni milioni 63 la Chelsea kumtaka mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti limekataliwa. (The Sun)
Chelsea wanamtaka winga wa Inter Milan Antonio Candreva, 30, huku Milan wakiwa tayari kumuuza kwa pauni milioni 25. (Mirror)
Real Madrid wanapanga kupanda dau la pauni milioni 46 kumtaka kipa wa Manchester United David de Gea. (The Sun)
Manchester United watamruhusu kipa David de Gea, 26, kujiunga na Real Madrid msimu ujao iwapo wataweza kumsajili kipa wa AC Milan Gianluigi, 18, Donnarumma. (Sun)
West Ham wanaghadhibishwa na jitihada za kutaka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 25, huku timu hizo mbili zikivutana kuhusu tofauti ya pauni milioni 5.5 katika bei ya usajili. (Telegraph)
Manchester City wameambiwa lazima walipe takriban pauni milioni 30 ikiwa wanataka kumsajili beki wa West Brom, Jonny Evans, 29. (Times)
Paris Saint-German wamesema hawatopokea dau lolote msimu huu la kumuuza winga Julian Draxler, 23. (ESPN)
Inter Milan wameonesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo beki wa Arsenal Shkodran Mustafi. ( GianlucaDiMarzi o.com)
Licha ya Arsenal kumnyatia, Marco Asensio, mchezaji huyo anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kubakia Real Madrid hadi mwaka 2023 na pia kusaini kipengele cha uhamisho chenye thamani ya euro milioni 500. (Marca)
Arsenal wapo tayari kupanda dau kumtaka winga wa PSG Julian Draxler msimu huu, huku PSG wakitaka pauni milioni 32. (The Times)
Real Madrid wamekataa dau la fedha nyingi kutoka kwa Juventus kumtaka Mateo Kovacic. (AS)
Tottenham wapo katika mazungumzo ya kina kutaka kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Argentina Juan Foythe, 19, anayechezea Estudiantes, kwa pauni milioni 9. (Guardian)
Kiungo mpya wa Everton Gylfi Sigurdsson, 27, amesema hana majuto yoyote kuhusiana na mtafaruku uliozuka wakati wa mchakati wa uhamisho wake wa pauni milioni 40 kutoka Swansea. (Times)
Niwatakie Wikend Njema wana michezo wenzangu
20/08/2017
Arsenal yapata kpgo cha kwanza kwenye ligi
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Zedekiaokungu@yahoo. Co. Uk
Dar Es Salaam
MWANZA