Dondoo za soka & michezo

Dondoo za soka & michezo

Share

Habari za Ligi mbalimbali,Matokeo ya Mechi mbalimbali Ndani n.a. Njee ya Tanzania,Habari za usajili wa wachezaji n.a. Habari za Michezo mengine

kwa habari mbalimbali za michezo na burudani ulimwenguni

Photos 12/06/2020

Jonas Mkude atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata majeruhi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.

Akiwa nje ya uwanja Mkude ataendelea na mazoezi mepesi pamoja na matibabu.

Photos 12/06/2020

EYMAEL Kumekucha Jangwani.
June 12,2020.

Akizungumza na BINGWA jana kutoka Shinyanga, Meneja wa timu hiyo, Abeid Mziba, alisema wamefanya mazoezi chini ya Charles Mkwasa, kwani kocha mkuu anatarajia kuungana na kikosi leo.

Alisema kati ya wachezaji waliokuwa wamebaki Dar es Salaam, kipa Metacha Mnata, amefika jana asubuhi na Bernald Morrison anaweza kufika leo.

“Tupo mazoezini jioni hii (jana) katika uwanja wa Fresho, kocha mkuu atakuwepo katika mazoezi ya kesho, Metacha amekuja na ndege ya asubuhi amewahi lakini pia Morrison atakuja asubuhi (leo),” alisema.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Msafara Dominic Albinus ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji alitaja sababu ya timu hiyo kufika alfajiri kuwa imetokana na changamoto walizopata njiani.

Albinus amezungumza na tofutti ya klabu hiyo, kuwa msafara wa timu hiyo ulichelewa baada ya gari yao kupata hitilafu ya kupasuka tairi ya mbele eneo la Manyoni mkoani Singida.

“Tumechelewa sana, lakini tunawashukuru sana wanachama na mashabiki wa Shinyanga ambao wametusubiri hadi alfajiri kutupokea, hii imetupa faraja kubwa na kwa wachezaji imewatia moyo,” alisema.

Photos 14/08/2019

Kocha Mkuu wa Klabu ya Chelsea, Frank Lampard amethibitisha kuwa kiungo wake N'Golo Kanté atakosekana kwenye mchezo wa leo wa UEFA Super Cup dhidi ya Liverpool utakaochezwa saa 4 usiku
-
Aidha, Lampard amesema atandelea kuwatumia zaidi wachezaji chipukizi ambao ni Mason Mount na Tammy Abraham kwenye kikosi chake

Photos 13/08/2019

MICHEZO: Mkurugenzi wa Klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesafiri kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Klabu ya Paris Saint-Germain ili kumrudisha Camp Nou Mbrazil, Neymar

> Mchezaji huyo aliondoka Barcelona kwenda PSG kwa usajili uliyoweka rekodi wa Euro milioni 200 mwaka 2017

Photos from Dondoo za soka & michezo's post 01/08/2019

NICOLAS PEPE ASAJILIWA RASMI ARSENAL‬

‪- Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast (24) amesaini kandarasi ya miaka mitano kwa dau la Paundi Milioni 72‬

‪- Anakuwa mchezaji ghali kusajiliwa Arsenal‬

‪Unadhani Pepe, Lacazette na Aubameyang watafunga magoli mangapi jumla msimu ujao?‬

Photos 01/08/2019

Guardiola, Klopp washikana mashati tuzo ya Kocha Bora FIFA
Unafikiri ni nani anafaa kuwa kucho bora wa FIFA kwa msimu uliopita

Photos 01/08/2019

Kiungo wa klabu ya Manchester United Paul Pogba amesema kwamba alikua akivutiwa sana kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania ila kutokana na muendo wa klabu hiyo hivi sasa anaweza kuwa hana ndoto za kujiunga na klabu hiyo

Photos from Dondoo za soka & michezo's post 01/08/2019

Hizi ndio Jezi mpya za SIMBA SC kwa msimu mpya wa 2019/2020

Photos 01/08/2019

Mancheater united Pia wamewakilisha ada ya paun 80 milion kwa harry maguire na baada ya zile ofa za awali kukataliwa UNITED wanataka kumfanya beeki huyo wa kingereza kuwa beki ghali zaid duniani

Photos from Dondoo za soka & michezo's post 01/08/2019

Uhamisho wa mabadilishano kati ya paul dyabala na Lukaku sasa umebakia hatua chache kati ya manchester united na mchezaji klabu na klabu zimeshakubaliana

Photos 28/12/2018

Jana baraza la wadhamini la klabu ya Yanga lilithibitisha kupokea barua rasmi kutoka kwa Yusuf Manji akithibitisha kurejea katika nafasi yake ya Mwenyekiti katika klabu hiyo.
:
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF Malangwe Mchungahela amesema hajapokea barua yoyote kutoka Yanga kuhusu kurejea kwa Manji: "Sijaletewa barua yoyote, hiyo barua wamesomeana wenyewe hukohuko, sijaiona nasikia tu kupitia vyombo vya hababari."
:
"Utaratibu tumetangaza, anayetaka kugombea aende TFF akachukue fomu, tayari fomu zinachukuliwa. Uchaguzi unaendelea vilevile na nafasi ya mwenyekiti ipo wazi. Uchaguzi umepangwa January 13, 2019 utafanyika."
:
"Siku zote alikuwa wapi hadi uchaguzi umetangazwa ndio anaandika barua? amehoji Mchungahela baada ya kuambiwa Manji amerejea kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti kwenye klabu ya Yanga. (chanzo-UFM)

Photos 28/12/2018

SAMIRI NASIR IS BACK
:
:
Unakumbuka Samir Nasri lakini? Nauliza mnamkumbuka vizuri? Kule Ufaransa anakumbukwa sana na kashfa yake ya kugoma kumpisha siti Thierry Henry kwenye basi la timu ya taifa. Inasemekana Henry alikuwa na siti yake maalum lakini Nasri alikaidi utaratibu huo kiasi cha kuitwa mtukutu ndani ya timu ya taifa.
:
Sasa anarudi tena EPL. Awamu hii anaeleka West Ham sasa. Taarifa zinasema anakamilisha vipimo vya afya.
:
:
Ni baada ya safari ndefu ya maisha ya kusuasua ya kisoka tokea alipoanza kutemwa timu ya taifa na Bwana Didier Deschamps. :
:
Amekumbwa na dhoruba nyingi ingiwemo adhabu ya kufungiwa miezi 18 ya kutokujihusisha na soka baada ya kusadikika kutumia madawa ya kusisimua misuli. :
:
Kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada ya kuvunja mkataba wa klabu kutoka Uturuki ya Antalyaspor.
Nasri mwenye miaka 31 anatarajia kupokea kiasi ya £80,000.
Hebu fikiria hii West Ham:
🇨🇱 Manuel Pellegrini kocha
🇦🇷 Pablo Zabaleta
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Andy Carroll
🇲🇽 Javier Hernandez
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Jack Wilshere
🇫🇷 Samir Nasri

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Msimbazi Sentsr
Dar Es Salaam