Sport analysis

Sport analysis

Share

uchambuzi na habari

Photos from Sport analysis's post 25/09/2023
Photos from Sport analysis's post 25/09/2023

FIGHT for life leo ningependa kuzungumzia uharibifu wa uvamizi wa wanyama pori.Nikwa k**a mkazi wa kibutuka wilayani LIWALE mkoa wa LINDI moja ya sehemu tunao patikana wahanga wa uvamizi wa wanyama pori katika makazi ya watu hivyo basi tunaiomba serikali itilie mkazo kwenye kuzuia uvamizi huu k**a sisi raia tunavyokatazwa na kuchukuliwa hatua kali pale tunapoingia hifadhi za wanyama pia waangalie kwenye fidia maana tumechoka kupewa fidia za matusi yaani unaaribiwa mali zenye thamani kubwa k**a vile mashamba ya mikorosho,mbaazi ila tunajikuta tunalipwa fidia ndogo k**a sh 50000 ambayo aikidhi ata gharama ya kuendesha maisha ndani ya mwezi mmoja hali inayosababisha maisha ya wananchi kuzidi kudidimia na kushindwa kuendesha familia zetu pia inadumaza fikra za upambanaji kwa sisi vijana maana hatuioni kesho yetu pia uvamizi huu upelekea vifo kwa ndugu zetu na kuacha familia nyingi bila nguzo za kuegemea maana fidia wanazopata nik**a vile zinawaongeza uchungu maana hazikizi pia ni dharau kwetu

05/06/2020

R.I.P GEORGE FLOYD leo dunia inatufunza jinsi gani binadamu wote tuko Sawa kwanini tubaguane
Kaka umetuachia majonzi sisi watu weusi wenzako.Ata fundi wa mpira wa kiingereza sancho alihitaji haki kupitia kifo chako akituwakilisha sisi wanamchezo wenzako.
Uaga nasikitika kila siku nikiona wanamichezo wenye rangi nyeusi wakibaguliwa.
Natumai familia yako itaweza kupambana katika kipindi hiki kigumu.
JUSTICE FOR GEORGE FLOYD

11/02/2020

Ahsante manula kwa kuonyesha kwamba wewe bado ni Tanzania one wale walio kubeza wamemeza maneno thanks broh AISHI MANULA CLEEN SHEET

Photos from Sport analysis's post 16/07/2019

Author or sport analyser:
Manchile Junior
Contact:0757956403

Nianze kwa kumshukuru Ettiene Ndayiragije kwa kutukumbusha uyu kiumbe ambae watanzania wengi kwa makusudi tuliamua kumpoteza kwenye ramani ya soka kwa kujiaminisha kwamba kachoka na kazeeka.
Anaitwa JUMA KASEJA ni mwanaume wa shoka au mpambanaji aliezaliwa mwaka 1985.Nani hamjui uyu mwana ambae amecheza katika timu kubwa za Tanzania kwamuda mrefu.
Alianza maisha yake ya soka katika shule ya sekondari makongo iliyokuwa ikisimamiwa na kanari Iddi kipingu na baadae akasajiliwa na moro united mwaka 2000.
Katika zama za mwanzoni mwa miaka ya 2000 Simba ulikuwa ina hangaika kumpata kipa ataeweza kuziba nafasi ya mlinda mlango mahiri na maharufu Mohamed Mwameja ambaye Wana Simba wengi na watanzania kwa ujumla walikua wanaujua ubora wa Mwameja akiwa langoni .
Ndipo macho ya Simba yakaangukia kwa kipa chipukizi wa moro united kwa kipindi icho ambae ndio JUMA KASEJA kuanzia apo umaharufu wake ukawa mkubwa na watu wakaanza kuona ubora wake, umaharufu ukazidi pale ambapo Simba wakiitoza zamalek kwa mikwaji ya penalty mjini Cairo nchini Misri yeye akiwa golikipa na alifanikiwa kucheza mkwaji wa penalty, pia miaka michache baadae akafanya hivyo tena safari hii Simba wakiitoa Santos ya nchini Africa kusini. Baadae ikapelekea mahasimu wa wao yanga ikiongozwa na bwenyenye au bosi wao wenye hela Yusuf Manji mwaka 2008 kumsajili mlinda mlango uyu mahiri.
Ambae miaka miwili baadae akarudi tena Simba na kuitumikia mpaka mwaka 2014. Na apo ndipo sinema ya mkuchoka ndio ilianza lakini mwenye akukubali ikapelekea kutafuta ulaji kwenye timu nyingine K**a vile mbeya city, kagera sugar na sasa kmc
Ndio sisi watanzania ambao mpaka leo tuka Gigi Buffon aendelee kudaka wakati yeye amezaliwa mwaka 1975 na alianza kucheza mechi za kimashindano mwaka 1995 akiwa na parma ya Italy au tunamshangilia golikipa wa Misri Essam El Hadary katika kombe la dunia mwaka 2018 akiwa amezaliwa miaka 46 iliyopita na kuanza mwaka soka la kiushindani mwaka 1993 akiwa na Al ahal na bado mpaka sasa anadaka katika timu ya Nagoom nchini Misri au tuna mshangilua Denis Onyango ambae amezaliwa sawa na shujaa wetu JUMA KASEJA Ila tumemwacha Onyango akitamba kwa kuchukua kipa bora wa Africa mara mbili na sisi tukiamini shujaa wetu muda wake umeisha.
Kwangu mm JUMA KASEJA ndio Tanzania one wa muda wote akiwa ameanza kuitwa timu ya taifa kuanzia mwaka 2001, pia ametumikia Serengeti boys.
Ahsante shujaa wangu JUMA KASEJA kwa kuwaonesha watanzania kwamba bado ujachoka. Najua unaweza usicheze mbele ya Aishi Manula Ila kuwa kwako kwenye kamba naamini timu ya taifa imepata kiongozi wa kuwaongoza wachezaji wenzake na mwamasishaji.
Pia napenda kumpongeza tena kocha Ettiene Ndayiragije pamoja na jopo lote la makocha wa muda ndugu Juma Mgunda na Selemani Matora
THANKS MY BROTHER JUMA KASEJA

Photos from Sport analysis's post 15/07/2019

Author or sport analyser:
Manchile Junior
Contact:0757956403

Karibia pazia la ligi kuu nchini uingereza lina funguliwa leo nataka niwape historia fupi ya ligi ya uingereza.
Ilianzishwa mnamo mwaka 1888 ikiwa inajulikana K**a ligi daraja la kwanza kabla ya kubadilishwa 20 February 1992, nakujulikana K**a English premier league.Ambapo inajumuisha timu 20.
Timu nne za juu maarufu K**a top four zinacheza uefa, pia timu zinashika namba 5 na 6 pamoja na bingwa wa FA cup wanacheza ueropa na timu 3 za mwisho kutoka chini zinashika daraja na kupanda zingine 3.
Pia imefanikiwa kushirikisha timu mbili kutoka Wales ambazo ni Swansea city pamoja na Cardiff city .
Zifuatazo ni baadhi za takwimu;
1: Manchester United ndio timu iliyo chukua ubingwa Mara nyingi(20)
2;Alan Shearer ndio kinara wa ufungaji mabao (260)
3;Gareth Barry ndio mchezaji aliecheza mechi nyingi (653)
4; Peter Cech ndio kipa aliecheza mechi nyingi bila kuruhusu goli (162)
5; John Terry ndio anaoza aliebaba makombe mengi (5)
Wafuatao ni washirika wa television katika kurusha matangazo;
1:sky sports
2:BT sports
3:BBC
4: Amazon (live matches)
5:Dstv
Na website ya epl ni Premierligue.com
WELCOME THE NEW SEASON

14/07/2019

Author or sport analyser:
Manchile Junior
Contact:0757956403

Leo tunaweletea Ibrahim Ajibu Migomba amezaliwa September 12 mwaka 1996 katika wilaya ya singida na Ana urefu wa 1.8 m.
Uwanja anatumia zaidi mguu wa kulia, zifuatazo ni nafasi anazomudu kucheza:
1:winga ya kulia
2:winga ya kushoto
3:mshambuliaji wa pili
4: mshambuliaji wa kati
5:kiungo mshambuliaji
Ajbu alianza maisha yake ya soka katika kituo cha bom bom na baadae kutimkia Simba ya watoto mwaka 2009 akiwa na miaka 13.
Timu ambazo amewai kutumikia
1:mwaka 2012 Simba sc
2:mwaka 2013 mwadui fc(mkopo)
3:mwaka 2013_2017 Simba sc
4:mwaka 2017_2019 yanga sc
Na sasa amerejea tena katika timu yake ya zamani Simba sc pia amewai kutumikia timu ya taifa ya Tanzania katika vipindi tofauti.
KARIBU NYUMBANI IBRAHIM AJIBU MIGOMBA miguu ya zahabu au MR ASSIST

Photos from Sport analysis's post 13/07/2019

Author or sport analyser:
Manchile Junior
Contact :0757956403

Leo tunaweletea tena mchezaji mwingine anaitwa Francis kahata nyambura.
Amezaliwa may 4 mwaka 1992, katika mji wa Ruira, Kenya na Ana urefu wa ft5 na nchi 10.
Nimchezaji wa eneo la kiungo ameanza maisha yake ya soka katika kituo cha Ravenna mwaka 2006 na baadaye kituo cha thika united mwaka 2008.zifuatazo ni timu ambazo amewai kuzichezea;
1:mwaka 2008 Thika United
2:mwaka2014 Kf trana
3:mwaka 2015 Gormahia
Pia anacheza timu ya taifa ya Kenya toka mwaka: 2011 na amefanikiwa kuchezea mechi :31 na kufunga mabo 2.
Kwasasa amesajiliwa na Simba sc ya Tanzania kwa mkataba wa miwili.
KARIBU TANZANIA FRANCIS KAHATA NYAMBURA ambae wa Kenya wanapenda kukuita MESSI WA KENYA

Photos from Sport analysis's post 11/07/2019

Author or sport analyser Manchile Junior
Simu no 0757956403
Temeke wailes

Leo ningependa kewaletea historia fupi ya beki mpya wa Simba anaitwa:
Gerson Fraga Vieira
Ambae amezaliwa mnamo October 14 mwaka1992, katika mji wa Porto alegere.
Ana urefu wa futi 5 na nchi 11,anacheza katika nafasi ya ulinzi wakati.
Amezaliwa mji mmoja na gwiji wa mpira duniani Ronaldinho.
Alinza maisha yake ya mpira katika kituo cha kukuzia vipaji kwa watoto cha gremio fc mwaka 2000 mpk 2012, zifuatazo ni timu ambazo amezitumikia katika maisha yake ya soka:
1.mwaka 2012 gremio
2.mwaka2012 oeste (mkopo)
3.mwaka 2014 atenas (mkopo)
4.2015 red bull Brasil (mkopo)
5.mwaka 2016 Mumbai City
6.mwaka 2017atletico tabarao
7.mwaka 2018 Mumbai City
8.mwaka2018 ATK
9.mwaka2019 Simba sc
Pia katika maisha yake ya soka amewai kuchzea timu ya taifa ya Brazil ngazi za vijana.
Mwaka 2007 U15
Mwaka 2010 U17
Ambae amecheza na wachezaji maarufu K**a neymerjr,coutinho,casemiro na Alson Becker na kufanikiwa kuchukua kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 yeye akiwa K**a naodha wa timu.
Kifupi tunasema ni beki katili mwenye sura nzuri

10/07/2019

Leo ni siku tulivu ya jumatano napenda kuwakumbusha na kuwaomba saport zenu mashabiki wangu

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 08:00 - 17:00