02/08/2026
Mapambano yataendelea, hakuna kukata tamaa.
Daniel Sinda Sinda Benjamin Fernandi
The Home : Running, Throwing, Jumping & Walking. News of Best World's Athletes, Events & Competition.
Athletics Tanzania (AT) is the National Governing body responsible for Track and Field, Marathons ,Road Races and Cross Countries. It is affiliated with National Sports Council of Tanzania (NSC) and World Athletics (WA) which is the international governing body of Athletics.
02/08/2026
Mapambano yataendelea, hakuna kukata tamaa.
Daniel Sinda Sinda Benjamin Fernandi
01/08/2026
Workouts Alphonce Felix Simbu🇹🇿 , road to Sydney Marathon Glasgow 2026
All the Best, Champion.
📸 Merit Concept
Hard work pays. Mao Hhando
🎥 Javier Mauricio Leal
30/07/2026
Wawakilishi Wetu 🇹🇿 mashindano ya Jumuiya ya Madola , Glasgow, Scotland Glasgow 2026
Kutoka Kushoto ni; Makenji, Benjamin, Hamida , Kocha Marcelina Gwandu, Sisilia Panga , Sinda Sinda na Joshua Gisemo.
SIMBU APEWA MILIONI 10 ZA MAANDALIZI YA SYDNEY MARATHON
Mwanariadha Alphonce Simbu Alphonce Felix Simbu🇹🇿 aishukuru benki ya NMB NMB Bank Plc kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 10 ;k**a fedha ya kumuwezesha kwenye maandalizi ya mbio za "TCS Sydney Marathon " TCS Sydney Marathon presented by ASICS zitakazofanyika tarehe 30 Agosti 2026, huko Australia.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (MICAS) Baraza la Michezo la Taifa Gerson Msigwa Neema Yotham Msitha 🇹🇿 NMB Bank Plc
MAKENJI AVUNJA REKODI YA TAIFA YA MIAKA 47, AFUZU NUSU FAINALI YA MITA 200 GLASGOW 2026
GLASGOW, Scotland | Julai 29, 2026
Mwanariadha wa Tanzania Winfrida Makenji ameandika historia kwa kuvunja rekodi ya taifa ya mbio za mita 200 wanawake iliyodumu kwa miaka 47, baada ya kutumia sekunde 23.88 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 inayoendelea jijini Glasgow, Scotland.
Muda huo wa sekunde 23.88 umefuta rekodi ya awali ya taifa ya sekunde 23.92, iliyowekwa na mwanariadha Nzaeli Kyomo kwenye Michezo ya Afrika iliyofanyika Agosti 2, 1979 jijini Dakar, Senegal.
Mbali na kuweka rekodi mpya ya taifa, Makenji pia amefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya mbio za mita 200 wanawake, hatua inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kuwania mafanikio makubwa kwenye mashindano hayo.
Makenji anatarajiwa kurejea tena uwanjani kesho kushiriki mbio za nusu fainali, ambapo atakuwa akisaka nafasi ya kutinga fainali na kuwania medali, huku akiendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026.
🎥✍️ Issa Ndokeji Kunduchi ITV TANZANIA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (MICAS) Baraza la Michezo la Taifa Gerson Msigwa Neema Yotham Msitha 🇹🇿
29/07/2026

Glasgow 2026
📌✍️ Issa Ndokeji Kunduchi
28/07/2026
Mwanariadha Alphonce Simbu Alphonce Felix Simbu🇹🇿 akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa benki ya NMB NMB Bank Plc tawi la Arusha ; kwa lengo la kupokea zawadi ya fedha ya kumuwezesha yeye kwenye maandalizi yake ya mbio za "TCS Sydney Marathon " TCS Sydney Marathon presented by ASICS zitakazofanyika tarehe 30 Agosti 2026, huko Australia.
28/07/2026
Mazungumzo yenye Tija kwa Wanariadha. Yajayo Yanafurahisha.
Alphonce Felix Simbu🇹🇿 NMB Bank Plc
MAKENJI AWEKA REKODI YAKE BORA JUMUIYA YA MADOLA 2026 MJINI GLASGOW, SCOTLAND
GLASGOW, Scotland | Julai 27, 2026
Mwanariadha wa Tanzania Winfrida Makenji ameweka rekodi yake bora binafsi ya sekunde 11.65 katika Heat namba 3 ya mbio za mita 100 wanawake kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 inayoendelea jijini Glasgow, Scotland.
Makenji alionyesha kiwango kizuri katika mbio hizo, ambapo muda alioutumia wa sekunde 11.65 umeandika rekodi yake mpya bora binafsi (Personal Best), hatua inayoonyesha maendeleo makubwa katika kiwango chake cha ushindani.
Baada ya kukamilisha mbio za mita 100, Makenji sasa anajiandaa kushiriki tukio lake la mwisho la mashindano hayo, mbio za mita 200 wanawake, zitakazofanyika Julai 29, 2026. Katika mbio hizo ataingia akiwa na rekodi yake bora ya sekunde 24.04, akilenga kuendelea kuboresha muda wake na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (MICAS) Baraza la Michezo la Taifa Gerson Msigwa Neema Yotham Msitha 🇹🇿
✍️ Issa Ndokeji Kunduchi
| Monday | 21:00 - 17:00 |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| Wednesday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| Friday | 09:00 - 17:00 |
| Saturday | 10:00 - 15:00 |