Kariakoo Digital

Kariakoo Digital

Share

This website has all the information on shops and businesses in Kariakoo and is available to anyone,anytime using laptops, computers & all Mobile Devices. e.g.

It is a known fact that Kariakoo drives the retail industry in Tanzania supplying everything from clothings, medicine, cosmetics, building materials e.t.c to many small scale
traders all over the country. However, businesses in Kariakoo don’t advertise but rely on walk in customers. This is because it is costly for small shops to advertise in the
media (radio, TV, Press etc). But if they are comb

29/06/2016

MAKINIAPP: Hatua ya Kwanza

Fahamu jinsi ya kutumia MakiniApp kwa ufasaha zaidi kupitia video hii.

Kwa safari salama, usisahau kudownload MakiniApp
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.pro.makini

Kwa maoni, maswali au ushauri tembelea facebook.com/MakiniApp

Abiria ni haki yako kufika salama...!

Photos 21/04/2016

LIJUE BASI LA MWENDO HARAKA

MRADI wa mabasi yatakayo kwenda mwendo wa haraka katika barabara teule mpya jijini Dar es Salaam unaweza kuwa na ufunguo wenye sulushisho dhidi ya foleni na misongamano ya magari jijini humu.
Matarajio ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni kwamba kuzinduliwa kwa mradi huu kutakuwa ndio mwisho wa tatizo sugu la foleni katika barabara zake nyembamba ambazo nyingi mtindo wake ulijengwa na Wakoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.
Pamoja na kuwahi kuwepo aina hii ya mabasi katika miaka ya 1980, sasa mabasi haya yamerudi tena katika ubora wa kipekee na tofauti hasa katika suala zima la uundwaji wake wa kuvutia zaidi na ulio na mapambo mengi k**a vile televisheni, kiyoyozi, kamera za usalama(CCTV Camera) ambazo zitasaidia kuonyesha usalama ndani ya basi, endapo utatokea uhalifu wowote muhusika ataonekana mara moja. Pamoja na kuwepo vyote hivyo pia kuna na viti kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa viungo pamoja na mama wajawazito.

TUANGALIE BAADHI YA SEHEMU KATIKA BASI HILI;

A. STELINGI - STEERING WHEEL
Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani, wenye ubora wa kimataifa na unaozingatia usalama wa basi liendeshwapo barabarani muda wote. Pia kiti cha dereva kina uwezo wa kumpunguzia uchovu wa kukaa kwa muda mrefu ili kumsaidia kuwa makini aendeshapo basi husika ili kuepukana na ajali.

B. TAIRI - TYRE
Matairi bora yaliyothibitishwa na viwango vya kimataifa (ISO) ili kuweza kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi.

C. KIZIMIA MOTO - FIRE EXTINGUISHER
Mitungi maalum ya kuzimishia moto utokanao na vimiminika (mafuta), gasi, hitilafu za umeme n.k

D. INJINI - ENGINE
Aina ya injini ni CUMMINS iliyotengenezwa nchini Marekani (USA) ndio inayotumika katika mabasi yaendayo kwa haraka, injini hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uchafuzi wa mazingira, imedhibiti uchafuzi wa mazingira (air pollution), makelele (noise pollution)

E. KAMERA ZA USALAMA - CCTV CAMERAS
Skrini ndogo yenye ukubwa wa inchi saba inayo dhibiti kamera 16 zilizomo ndani ya basi zinazo onesha yote yanayojiri ndani ya basi na kwa kupitia teknolojia iliyowekwa ndani ya kila basi yenye uwezo wa kutuma picha za matukio yote yanayojiri ndani ya basi liwapo barabarani kwenda kituo kikuu cha udhibiti na uchunguzi na matukio ya kihalifu na uharibifu wa samani.

F. VITI - SEATS
Ndani ya basi haki za walemavu, wazee, wajawazito zimezingatiwa kwa kutengewa viti maalum kulingana na mahitaji husika ikiwemo vikuju vya kushika kwenye bomba kwa abiria wanao simama.

13/04/2016
Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


P. O. Box 78107 NIC Investment House 13th Floor Samora/Mirambo Avenue
Dar Es Salaam
255