Freestyle Football Tanzania

Freestyle Football Tanzania

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Freestyle Football Tanzania, Jaribu Street Magomeni, Dar es Salaam.

Photos from Freestyle Football Tanzania's post 05/04/2023

WANAHITAJIKA WAJUMBE WA KAMATI ZA MCHEZO WA UCHEZEAJI MPIRA WA MIGUU ZA MIKOA NA WILAYA TANZANIA BARA. Piga 0786955825 kupata nafasi ya kuwa Mjumbe wa Kamati na mtaarifu na mwenzio.

15/11/2020

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS WA TFFA ATOA PONGEZI KWA MABINGWA WA DUNIA NA WASHINDI WA KINYANG’NYIRO CHA ‘TRICK’ BORA YA DUNIA, KUMSHUKURU CESC FABRIGAS KWA UTATHIMINI WAKE PAMOJA NA RAIS MAGUFULI

Jumapili, Novemba 15, 2020. Dar es Salaam.

Rais wa chama cha mchezo wa Uchezeaji wa Mpira wa miguu Tanzania ndg. Chief, Morison Mosses Jumanne Mzee amewapongeza mabingwa, washindi na mtathimini wa shindano la Ubingwa wa Dunia la Uchezeaji wa mpira miguu (WORLD FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP 2020 - REDBULL STREET STYLE IG: ) lililofanyika jana kwa njia ya mtandao.

Salaam za kwanza za pongezi ni kwa mabingwa ambapo bingwa wa kiume wa Dunia ni mchezeaji mpira wa Taifa la Norway Bw. ERLEND FAGERLI (IG:) na bingwa wa k**e wa Dunia ni mchezeaji mpira wa Taifa la Ufaransa Bi. MELODY DONCHET (IG:).

Salaam za pili za pongezi ni kwa washindi wa kinyang’anyiro cha ‘Trick’ bora cha Tuzo za Uchezeaji wa Mpira wa miguu ambapo mshindi wa kiume wa Dunia ni mchezeaji mpira wa Taifa la Norway Bw. BRYNJAR FAGERLI (IG:) na mshindi wa k**e wa Dunia ni mchezeaji mpira wa Taifa la Hungary Bi. KITTI SZASZ (IG:).

Vilevile, amemshukuru sana mchezaji mpira wa Taifa la Spain Bw. Cesc Fabrigas kuwa mmoja wa wahudhuriaji akiwa ndiye mtathimini mkuu wa shindano hili.

Aidha, anawapongeza waandaaji wa shindano hili washirika wetu REDBULL kwa kuzidi kuwa wadau wakubwa wa kudhamini shindano hili la Dunia kwa miaka yote likifanyika, pia katika mataifa kwa ujumla.
Kipekee, amempongeza sana sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Tanzania na kwa hotuba yake nzuri sana aliyoitoa juzi Ijumaa 13 Novemba, 2020 wakati akifungua Bunge la 12 katika Mkutano wa kwanza, kikao cha Nne na kumuomba na kumkumbusha Mhe. Rais na Serikali yake kwa ujumla kwamba watuangalie na sisi TFFA pindi watengapo fedha kwa ajili ya kuziandaa Timu za Taifa za michezo yote pamoja na kupatiwa eneo la kujenga uwanja wa Taifa wa mchezo wetu wa Uchezeaji wa mpira wa mguu nchini.

“UCHEZEAJI WA MPIRA WA MIGUU – YOTE UNAHITAJI NI MPIRA"

Imetolewa na:

KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO CHA TFFA

26/05/2020
Photos 17/05/2017
Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Jaribu Street Magomeni
Dar Es Salaam