03/09/2026
Whatsapp channel yetu ipo mahususi kwaajili ya kukusogezea picha kali sana za wachezaji kutoka vilabu mbalimbali ulimwenguni..
Utachagua wewe uchukue picha kwaajili ya ku save k**a wallpaper, dp, nk.
link ya channel hii hapa...>>> https://whatsapp.com/channel/0029VbCzMdnGE56mpL5QDn0I
03/09/2026
NI MAXI NZENGELI AU LIBASSE GUEYE?
Ndani ya mwezi ulioisha, wachezaji kadhaa wamefanya vyema sana wakizisaidia klabu zao kuondoka na alama muhimu...
Lakini kati ya hao, Maxi Nzengeli na Libasse Gueye wamefanya bora zaidi na kuhakikisha timu zao zinaokota kila alama kati kwenye mechi 05 zilizochezwa...
Takwimu zao hizi hapa;
🟢🟡 MAXI NZENGELI — YANGA SC
⚽ Mabao: 3
🎯 Assists: 2
🏆 MOTM: 4/5
🔴⚪ LIBASSE GUEYE — SIMBA SC
⚽ Mabao: 1
🎯 Assists: 5
🏆 MOTM: 3/5
Je, Nani anastahili zaidi kuwa mchezaji bora wa mwezi?!
03/09/2026
Kwa zaidi ya asilimia 70% kinachowafelisha wachezaji wengi hususan kwenye hizi Simba SC Tanzania & Young Africans Sports Club ni pressure...
Kisha asilimia 30 yanaweza kuingia mengineyo k**a mazingira, mifumo ya timu,nk.
Kwa dakika nilizomtizama kinda, Juma Abushiri naona ameamua kujitengenezea pressure mwenyewe...
Abushiri anapaswa kuambiwa kuwa hayupo kwenye umri wa ku prove chochote kile, anapaswa kuuenjoy mpira tu.
Timu haipo kwenye mabega yake, ajaribu kuiga mwenendo wa kina Abdulnassir Casemiro.
play as you train..📌
03/09/2026
Hizi mbili ni 🔥
Hapa designer alituliza kichwa...
Wananchi kimataifa...📌
31/08/2026
Pass maridadi, pass elekezi ya kuvunja ukuta wa Fountain Gate kutoka kwa Maxi Nzengeli.
Kisigino au watoto wa mjini wanaita kisigwato kutoka kwa technician Stephan Aziz Ki..
Finishing ya viwango mno iliyojaa kila aina ya quality na swaga kutoka kwa Peter Shasha Man 🔥
Aloooh!! Na hapo Mangqoba anasema bado timu yake haijafika kwenye ile level anayoitaka yeye. 😃
Yule baba ana roho mbaya sana, ukimsikiliza unaweza usilete timu uwanjani...😁
29/08/2026
Bado ni mapema kusema ila binafsi naona Young Africans Sports Club bado wanahitaji kurudi sokoni dirisha dogo na kutafuta kiungo mkabaji mwenye uwezo mkubwa wa kutimiza jukumu lake 'mama'
Huyu Duval Ngoma kwa dakika nilizomtizama naona ni passer mzuri na ana movement sahihi ndani ya uwanja..
Lakini;
Ngoma sioni k**a ni kiungo wa kukata umeme, sijaridhika na kiwango chake cha kupokonya mipira pia uwezo wa kuipa timu balance.
K**a jana ubora wa Mudathir kipindi cha kwanza ulimbeba sana Ngoma lakini Mudathir alipochoka kipindi cha pili, kiungo chote kikapoteana... Ngoma hakuonekana tena kwenye wakati ambao timu ilihitaji mipango kuanzia kwake...
Labda k**a ata improve, vinginevyo bado Yanga wanahitaji namba 6...
29/08/2026
MMESIKIA HUKO?!!!
Ni suala la muda tu, mashabiki wa Simba SC Tanzania mjiandae tu, msimu huu mtaweka sana vifusi vya mbolea 😁
Doumbia gari litawaka "soon" tu... Anasema Ahmed Ally;
"Coastal Union walifahamu hatari ya Doumbia ndio maana wakaweka mpango maalumu wa kumkaba na kumzuia
Pamoja na yote aliweza kufurukuta na kutengeneza hatari kadhaa zikagonga mwamba na nyingine kupaa
Siku Doumbia akikutana na mabeki wanaotoa assist kwa washambuliaji basi atafunga mpaka refa atachoka kuita kati
Ni muda tuu!!!!"
Ahmed Ally..
27/08/2026
Baada ya kusaini mkataba mpya, kiungo wa Al Ahly, Emam Ashour ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi barani Afrika...
Ashour atakunja kitita sawa na Tsh 270+ kwa mwezi..
Ana bonus nono...
Release clause ya mkataba wake huo (mpaka 2030) ni Tsh 81 Billion...
Mpira pesa.... 💰
27/08/2026
Tunaaanza upyaaaaaa 😁
we're back....📌