TANGAZO FURSA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KATIKA TEKNOLOJIA YA UHIFADHI WA MAZAO BAADA YA MAVUNO KATIKA VYUO VYA VETA KUPITIA MRADIWA YEFFA
VETA
This is an official account for the Vocational Education and Training Authority (VETA).
12/05/2026
10/05/2026
Matukio mbalimbali katika picha ni wakufunzi 25 wa VETA wakiambatana na Watumishi wa VETA Makao Makuu kutoka Kitengo cha Mafunzo, leo tarehe 10 Mei, 2026 wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es salam,tayari kwa safari ya Kwenda nchi Finland kujifunza ujuzi wa teknolojia zinazohitajika katika uchimbaji na ukuzaji mnyororo wa thamani wa madini.
UHITIMISHAJI WA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, 2026/2027
Mwaka huu 2025/2026, Serikali imepata kibali cha kuajiri walimu/wakufundi 760.
UFUNDI STADI, FURSA K**A ZOTE KWA WATU WOTE.
UHITIMISHAJI WA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, 2026/2027
VETA imeingia makubaliano na viwanda takribani 87 kwa ajili ya kushirikiana katika utoaji mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi.
UFUNDI STADI, FURSA K**A ZOTE KWA WATU WOTE.
UHITIMISHAJI WA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, 2026/2027
Kupitia mradi wa ESPJ II, Serikali imetenga Shilingi Bil 150.3 kwa nunuzi wa vifaa kwa ajili ya vyuo vya VETA.
UFUNDI STADI, FURSA K**A ZOTE KWA WATU WOTE.
09/05/2026
UFUNDI STADI WATAWALA MJADALA WA BAJETI WA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA 2026/2027.
Suala la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi limepewa umuhimu na mtazamo wa kipekee wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 2026/2027 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliohitimishwa leo, tarehe 8 Mei 2026.
Akizungumza kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Wanu Hafidh Ameir hali hiyo imejidhihirisha kwa wabunge kutoa michango mingi na kuuliza maswali mengi zaidi kuhusiana na VETA, ambapo asilimia 62.96 ya maswali yaliyoulizwa yalihusiana na VETA.
“Kati ya maswali 27 yaliyoulizwa na waheshimiwa wabunge, 17 yalielekezwa VETA,” amesema.
Akifafanua kuhusu baadhi ya maeneo, Mheshimiwa Wanu Ameir amesema ujenzi wa awamu ya kwanza wa vyuo 65 vya VETA unatarajiwa kukamilika Septemba 2026 na kwamba fedha ya kumalizia ujenzi huo imeshapatikana.
Kuhusu rasilimali watu kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya ufundi stadi, Mheshimiwa Wanu Ameir amesema mwaka huu Serikali imepata kibali cha kuajiri wakufunzi 770 wa vyuo vya ufundi stadi.
Vilevile, Mheshimiwa Wanu Ameir amebainisha kuwa Shilingi Bil 150.3 zimetengwa kupitia mradi wa ESPJ II kutumika katika nunuzi wa vifaa kwa ajili ya vyuo vya VETA.
Sambamba na hayo, amebainisha kuwa VETA imeingia makubaliano na viwanda takribani 87 kwa ajili ya kushirikiana katika utoaji mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi.
Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yenye jumla ya Shilingi trilioni 2.3.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Contact the business
Telephone
Website
Address
VETA Head Office, 12 VETA Road, 41104 Tambukareli, P.O. Box 802, Dodoma Tanzania, Email: [email protected] Telephone: +255 26 2963661 Fax: +255 22 2863408 Url: Www.veta.go.tz
Dodoma
PLOT NO. 18
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 21:30 |
| Tuesday | 08:00 - 21:30 |
| Wednesday | 07:30 - 21:30 |
| Thursday | 07:30 - 21:30 |
| Friday | 07:30 - 21:30 |