IJUE AFYA YAKO

IJUE AFYA YAKO

Share

Ijue afya yako inahusika sana na afya zetu katika makundi mawili yaani
1.Afya ya kiroho yaani spiritual matter
2.Afya ya kimwili yani physical matter

18/09/2023

Kitabu chetu Cha MAJUMA 70 ya unabii wakitabu cha danieli kipo tayari Kwa muundo wa hard copy na soft copy
Kukipata wasiliana nasi Kwa namba 0768350550 na 0676086350

18/09/2023
02/05/2023

Kifo ni uponyaji wa kudumu ambao Mungu huwapa watu wake. ni Moja ya maneno ambayo mzee wangu mkoba uliwahi kusema kipindi unatufundisha seminar ya kitabu Cha ufunuo

01/05/2023

JINSI YA KUMALIZA VIZURI
Na Mch: Chambo
Andiko: 2 Timotheo 4: 6-7
2 Timotheo 4:5-8
Dhima kuu: Maagizo ya mwisho ili kumtia moyo Timotheo katika huduma. Paulo alitamani kuona kijana wake Timotheo amalize vizuri

[6]Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.

[7]Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
(8)sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana,mwamizi wa haki, atanitunukia siku ile: wala SI Mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kw shauku kudhihirishwa kwake.

# Mifano ya wa watu walioanza vizuri na wak**aliza vibaya
1. Sauli alianza vizuri na Mungu lakini ak**aliza vibaya, mwanzoni alikubali kuongozwa na Mungu badae anaongozwa na mwanamke Mwenye Pepo la uaguzi na kuanzia hapo akapoteza ushirika na Mungu
2. Yuda Iskarioti alianza vizuri na Yesu lakini badae ak**aliza vibaya Kwa kumsaliti Yesu
3. Dema alianza vizuri na Mungu lakini mwishoni anapenda ulimwengu Kwa kuiacha Imani.

MAMBO MATATU YA KUJIFUNZA JINSI NA NAMNA YA KUMALIZA VIZURI
1. Pigana vita vizuri vya Imani, mkristo anatakiwa KUTAMBUA kuwa Yuko katika vita, biblia inasema vaeni silaha zote za Mungu, inatakiwa kuwa mpambanaji

Waefeso 6:10-11

[10]Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

[11]Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

2 Wakorintho 10:3-5

[3]Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;

[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

A. MAOMBI NI SILAHA INAYOSAIDIA KUMALIZA VIZURI
B. NENO NI SILAHA INAYOSAIDIA KUMALIZA VIZURI

C. KUMTUMIKIA MUNGU KWA UAMINIFU NI SALAHA NZURI YA KUSHINDA VITA.

2. Mwendo , kaza mwendo

Waebrania 12:1-2

[1]Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

[2]tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

DHAMIRIA KWENDA MBINGUNI

3. Linda Imani Yako -ukitaka kumaliza vizuri Linda Imani Yako sana

15/12/2022

Afya ya akili ni Kila unaponunua kifurushi Cha data za Internet ikitumie pia kutengeneza Hela Kwa kujifunza biashara kilimo ufugaji na mengine mengi sio tu insta,fb,TikTok other wise k**a huna maono ya kimaisha. K**a linafaa chukua ni Bure tu.

28/11/2022

Mambo matatu muhimu ili uwe na afya nzari
1.punguza softy drink zote
2.Acha kumwagilia moyo Kwa pombe
3. Jifunze kusamehe na kusahau.
Ukifanya hivyo Niko pale utanishukuru badae😁😁

22/11/2022

Maisha ni rahisi sana na ni afya ukiwa na vifuatavyo
1. Chakula
2.Mavazi
3. Malalo (malazi)
4.Upendo

21/11/2022

Hili wimbi la vijana kulala wanalala na energy kuamka na energy mlo wa mchana energy. nafikiri yanaweza kuleta madhara Kwa badae lakini sasahivi imekuwa k**a mfumo was maisha wakati watengenezaji wameweka tahadhari kuwa huruhusiwi kunywa zaidi ya chupa mbili.sasa najiuliza k**a hivi vinywaji no hatari he no nguvu kazi ya namna Gani tutaipoteza baada ya miaka ijayo? Toa maoni Yako ili elimu hii iwafikie vijana kumbuka comment Yako ni muhimu na iwe ya kujenga na kuelimisha jamii.

07/07/2022

Kanisa ambalo Yesu alisema"Nitalijenga Kanisa langu, Wala milango ya kuzimu haitalishinda" Mathayo 16:18. Ni kanisa ambalo Lina sifa zipi Kibiblia?
A.Kanisa ambalo waamini wake wameokoka na wanaishi Kwa vitendo juu ya wokovu wao.
B. Kanisa ambalo linatunza viwango vya maadili ya kikristo ili kujitofautisha na waigizaji wa mambo ya Mungu.
C. Kanisa ambalo waamini wake wako tayari kuibeba kweli ya injili wanayoiamini bila aibu, Kwa gharama yoyote ili wengine waisikie hiyo injili.
D. Kanisa ambalo linamngojea Bwana Yesu wakati wowote arudi ili Kuja kulichukua na kulipeleka mbinguni Kwa Baba.
E. Kanisa ambalo haliko tayari kuchanganya neno la Mungu na uongo. Kanisa ambalo linazingatia kanunu sahihi za kuyatafsiri maandiko ili kutopotosha maana ya maandiko iliyokuwa imekusudiwa na waandishi walioandika Biblia.
F. Kanisa ambalo linaishughulikia dhambi Kwa waamini wanaotenda dhambi bila kujali hadhi ya mtenda dhambi.
Ndugu yangu hayo ni baadhi tu ya mambo yanayolitambulisha kanisa Hilo. Swali la msingi ni hili Je, wewe ni mmoja wa washirika katika kanisa Hilo? Sifa pekee ya kuwa mshirika wa kanisa Hilo ni kutubu dhambi zako na kuziacha na kumwamini Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako Sasa. K**a Bado hujafanya hivyo, usijute, hujachelewa, nafasi Bado unayo. Amini Leo. Fanya maamuzi sahihi. Barikiwa na Bwana Yesu.

30/06/2022

Tafadhali elewa kuwa tiba haipatikani tu kwenye vituo vya afya;

*Mazoezi* ni tiba.
*Kufunga* ni tiba.
*Kula vyakula vya asili* ni tiba.
*Kucheka* ni tiba.
*Kupata usingizi* wa kutosha ni tiba.
*Mwanga wa jua* ni tiba.
*Kuonesha upendo* na *kuwasaidia watu* ni tiba.
*Kupendwa* na watu ni tiba.
*Kutoa shukrani* ni tiba.
*Kutafakari kwa kina* ni tiba.
*Kusoma na kujifunza Neno la Mungu* ni tiba.
*Kumsifu Mungu* ni tiba
*Kula vizuri na kwa wakati sahihi* ni tiba.
*Kuwa na fikra chanya* ni tiba.
*Kumtegemea na kumwamini Mungu* ni tiba.
*Kuwa na marafiki wema* ni tiba.
*Kusamehe wengine* ni tiba.
*Kukubali kosa na kuomba radhi* ni tiba.
*Kufanya kile ukipendacho bila aibu* ni tiba.
*Kutoa dukuduku na kueleza yanayokusumbua rohoni* ni tiba.

Ukiweka akilini mambo hayo yakawa sehemu ya kawaida katika maisha yako, *utapunguza sana utegemezi wa tiba za hospitalini* na safari za kwenda maduka ya dawa.

28/06/2022

Mungu alikuleta duniani ukiwa original. Wewe sio kopi ni halisi ndio maana alama za vidole hazifanani hata k**a mngekuwa mapacha wa kufanana, Mungu hatoi copy yeye alikuleta ukiwa og. Shetani asikukatishe tamaa wala wewe mwenyewe acha kukata tamaa Mungu yupo kwa ajili yako.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dodoma