22/04/2024
Hekaya za Kombo
Kibu Anaufanya Mpira Uonekane Mchezo Mgumu.
Playing football is very simple, but playing simple football is the hardest thing there is.Johan Cruyff
Johan Cruyff aliamini sana kwenye nadharia yake ya kucheza mpira ni rahisi sana lakini kucheza mpira rahisi ni kitu kigumu kwasababu
1.Alitaka kuona wachezaji ambao wanafanya vitu rahisi kuurahisisha mchezo bila kutumia nguvu nyingi hasa kipindi wana mpira.
2.Alitaka kuona ubongo unafanya kazi kuliko fuvu la kichwa yaani akili kwanza akili mwisho.
Uenda kaburi la Johan Cruyff likawa linatingisha kwasababu ya kile anachokifanya Kibu Dennis akiwa na mpira mguuni kwasababu kuna muda Kibu anafanya vitu ambavyo havina maana
1.Kibu akiwa na mpira anataka kukimbia nao Kila muda kitu ambacho kinawafanya wapinzani kuendelea kujiimarisha kwenye muundo wao kuzuia.
2.Kibu ubongo wake kuna muda unashindwa kujua kwamba mpira unatakiwa kutembea kuliko yeye kipindi timu ina mpira (in possession).
3.Kibu kuna muda anashindwa kutafuta nafasi kwenye maeneo muhimu kwa ajili ya kupasia mpira kirahisi kabisa.
Kibu Denis mchezaji wa kisasa kabisa lakini changamoto kubwa hafahamu muda wa kukimbia na mpira na muda wa kupamiana na wachezaji wa timu mpinzani,kukimbia sana na mpira katika tafsiri ya soka la kisasa ni kuvifanya vitu vizuri kwa njia ngumu.
Binafsi nafikiri wachambuzi wala rushwa na mashabiki wavivu wa kufikiri sahihi kuna sehemu wanashindwa kumsafisha Kibu Denis matongotongo vizuri wanampa sifa za kijinga eti anakaba sana na kuwasumbua mabeki wameshindwa kabisa kumwambia Kibu kuna upande wa shillingi wa kucheza mpira rahisi kabisa kwenye njia rahisi.
Nendeni kwenye kaburi la Johan Cruyff mkachukue ubongo wake kisha muuweke kwenye kichwa Cha Kibu.
If truth shall kill them let them die.
21/04/2024
Hekaya za Kombo
Inonga sio kidonge Cha Maumivu
Kuna vichaka viwili kichaka cha ubora na kichaka cha ubovu,nafikiria Simba wanapaswa kukubali kujificha kwenye kichaka cha ubovu kwasababu watakuwa wanajiambia ukweli wao wenyewe kuwa kwasasa sio kwamba timu yao haina wachezaji wazuri lakini lazima wakubali Simba inacheza mithili ya watoto wa kindergarten yaani Simba haina makali kwenye kuzuia hatari za mpinzani na kuwa makatili mbele ya goli.
Kwenye mechi ya jana kundi la mashabiki wavivu wa kufikiri wameacha kujificha kwenye kichaka cha ubovu wa timu kiuchezaji wameamua kutengeneza kichaka kipya cha kumnyonya damu beki kisiki mahiri Enock Inonga eti alijifanya kaumia ili timu ifungwe,Hawa mashabiki wameamu kuutukuza ujinga hawataki kukubali kwamba kulwa kwa misimu kadha amekuwa bora mbaya zaidi hawana kukumbuku tamu kwamba Inonga aliyekuwepo kwenye goli 5 za derbi iliyopita ni yule yule aliyekuwepo jana pale kwa mkapa akishuhudia ubora ukiamua mechi.
Kwasasa mashabiki wa Simba wanapaswa kukubali kwa ubora wa Yanga hata Simba wangekuwa 22 kiwanjani wangefungwa tu jana kwasababu Simba ipoteza nguvu yake kuu ya ushindani kiwanjani,sasa hivi kila timu inaamini inacheza na Simba yenye haiba ya swala.Siku zote watu wenye busara ukubali kulamba kinyesi ukubali kwamba matapishi ya zamani ni muhimu kwenye kujenga matapishi mapya,Simba inapaswa kujengwa upya kuliko kutaka kumjenga Inonga.
Inoga hawezi kuwa kidonge kwenye ubora wa Yanga.
If truth shall kill them let them die
31/03/2024
Gamondilism Ilikuwa Zaidi ya Nadharia.
Miguel Gamondi kabla ya mechi alifanya kazi vizuri kwenye uchambuzi wa Mamelods (Swot Analysis).
Garmondi alifahamu ubora wa Mamelods kwenye maeneo haya
1.Mamelods ni wazuri kwenye kutafuta sana nafasi kwenye maeneo mbalimbali ya uwanja kwa ajili ya kupasiana mpira wakiwa huru.
2.Mamelods wakiwa wanajenga mashambulizi watu hatari ni
I.Williams kwenye build up
II.Marcelo Allende na Mokoena wako dynamic sana kwenye kucheza k**a namba 6 & 8 wawili iwe kwenye build up au kwenye ku develop plays za Mamelods kwenye phase zote.
3.Lucas Ribeiro pale kwenye zone ya 14 ndio kiini Cha Peter Shalulile na Lorch kufanya vizuri mbele ya goli la mpinzani kwasababu ya uwezo wake mzuri kwenye kutembea na mpira na kuupasia kwenye maeneo yote ya juu.
Kwa hiyo Mamelods wakiwa na mpira
I.Kwenye phase 1 & 2 watu hatari ni Williams,Mokoena na Allende.
II.Kwenye phase ya 2 na 3 Lucas Ribeiro ni mtu hatari kwenye kuendelea kuitembeza timu mbele ya Lorch na Shalulile.
Kwa hiyo hili kuwazuia Mamelods Miguel Gamond alifanya hivi.
1.Hakuna kuwapa nafasi ya kucheza wakiwa huru kwenye maeneo nyeti hasa mstari wa katika na mstari wa kwanza wa ulinzi yaani Yanga walikuwa wanapress sana kwenye low- mid block.
2.Kuwanyima Allende na Mokoena nafasi nyingi huru za kupasia mpira kwenye njia za katikati ya uwanja ndio maana kazi kubwa ya Mkude,Muda na Max ilikuwa ni kupress katikati ya uwanja bila ya kupoteza muundo wao (pressing structure).
3.Bila mpira Yanga walitakiwa kukimbia sana na ku react kwa haraka sana kwenye matendo ya kuzuia (defensive actions).
4.Mkude alikuwa mchezaji muhimu kwa ajili kutopoteza muundo wa kuzuia mbele ya mstari wa mabeki wa Yanga,alikuwa mithili ya msumari uliopigiliwa chini kwa ajili kucheza pale pale katikati kwa ajili ya ku maintain shape ya kupress mbele ya mabeki.
5.Hakuna kupress kwenye mstari wa juu na idadi na kubwa ya wachezaji kwasababu ikitokea pressing imeshindwa kufanya kazi Mamelods wangefaidika.
28/02/2024
Hekaya za Kombo
Heshima ya Chama,Kipaji cha Pacome
Kuna kundi la watu wenye utapiamlo wa kiakili watu ambao kila kukicha wanasaga mawe wanapiga zumari wanapiga filimbi kutaka kuipoka heshima ya Clotus Chota Chama kwasababu ya kipaji kikubwa kilicholala kwenye miguu ya Pacome,Wanajaribu kutumia mtambo wa gongo kupima heshima ya Chama wakati akili zao zikiwa zimeviringishwa na sigara bwege,mtanange,ulanzi,Skadi,chimpumu.Hawa watu hawataki kabisa kusikia heshima ya Chama eti ina uzito mkubwa kuliko kipaji cha Pacome.
Hawa watu wenye utapiamlo wa kiakili waliwahi kuuchukua ujinga wakauweka kwenye vita ya Aziz na Chama waliwahi kuichukua miguu ya John Bocco wakaimwagia pombe mbele ya Mayele ,wanachanganya sana tofauti kati ya kipaji na heshima na mbaya zaidi walianza kupenda aina fulani za pombe kabla ya kuipenda pombe yenyewe, ndio maana wale wanafalsafa wa mpira wa zamani walichagua heshima ya Chama kuliko kipaji cha Pacome sio kwasababu vichwa vyao vimejaa ugoro isipokuwa akili zao zimefika chini ya maji kabisa baharini.
K**a tutaacha vibuyu kupima ukweli,k**a tutaacha taarabu na kisha tukachagua kutumia kioo cha mpira na hip hop kuwa mziki ambao ndio kipimo halisi cha kipaji cha Pacome na heshima ya Chama basi taswira ya ukweli itaakisi mbele ya kioo cha mjinga na mwerevu.Najua wale watu wenye utapiamlo wa kiakili mtakuwa mmeelewa kwamba huu sio ushindani wa Chama na Pacome ni uhusiano kati ya heshima na kipaji.
If truth shall kill them,let them die.
27/02/2024
Hekaya za Kombo
Mboga ya Jirani ni Sumu
Ahmed Ally mbele ya jicho la camera amekaa na suti yake muda mwingi ana kazi ya kuzungumzia matatizo ya jirani anasahau kuwa familia yake ina matatizo lukuki nafikiri baba mjinga ndio anaweza kufanya hili yaani anajidili mboga ya jirani iliyochacha kuliko kutafuta dawa ya mboga yake iliyooza.Huu utamaduni wa Ahmed Ally wa kujadili matatizo ya Yanga kwenye press ya Simba ni ishara mpira wetu umekubali kuwakumbatia wapiga ngoma sebuleni.
Ally Kamwe amechagua kuwa Ahmed Ally aliyepaka bleach kwasababu ameendelea pale alipoishia ndugu yake yaani kwenye press ya Yanga kaamua kuleta ngojera kibao za Simba,Ally Kamwe anaamini hawezi kuifanya biashara Yanga pasipo mkono wa Simba anaamini hawezi kufika mjini bila ya kutengeneza maudhui yenye sura ya Simba ndani yake.Wale wachache wanaofahamu kuhusu nguvu ya chapa tunaona Ally Kamwe ana tumia nguvu nyingi kupika chakula cha Simba wakati Yanga Kuna njaa kali.
Ukifuatilia hizi press mbili za hawa wakuu wa idara ya habari ya Simba na Yanga utangudua mpira wetu bila taarabu hauwezi kwenda utangundua kwamba ili biashara ya Ally Kamwe iweze kwenda lazima biashara ya Ahmed Ally ipewe jina la mbwa mbaya.
Relative Truth.
K**a ukweli utawaua acha wafe tu.
24/02/2024
Kombo Tactical Analysis
Malaika na Mashetani Wamefurahi Sana
Cr Belouzidad walikuwa wanapress kwenye 5-4-1,CR Belouzidad wakiwa kwenye 5-4-1 ndani ya dakika 40 za kwanza walifanya hivi
1.Walizuia kwa idadi kubwa kwenye phase 1 & 2 ya uwanja.
2.Walikuwa wanajitahidi kuubana uwanja (condensing)
3.Walitengea mazingira ya kutaka kuishambulia Yanga wakiwa wazuia kwa idadi (rest attack)
Cr Belouzidad baada ya kufungwa ilibidi wanabadilishe njia za kucheza na
1.Waliamua kuondoka kwenye kuwa defensive minded.
2.Kwenye kushambulia walijitahidi kuweka presha ya kushambulia kwa namba kubwa.
Kitendo Cha CR Belouzidad kutaka kucheza kwa kuwa na matendo Cha kushambulia (offensive actions) kilisababisha
1.Kutokuwa na rest defensive nzuri
2.Kuacha nafasi ( space) kubwa kwenye upande wa kulia kushoto na katikati hasa kuanzia mbele ya safu ya ulinzi.
Pacome kwenye 2/3 na 3/3 alikuwa mithili ya jini
1.Uwezo wa kuama kutoka zone moja ya uwanja kwenda nyingine ulikuwa mkubwa sana sana
2.Kutengeneza vibanda kwa ajili ya kupokea mpira
3.Uwezo wa kushindana kwenye mazingira ya 1v1 1v2 1v3
4.Kutengeneza nafasi.
Yanga wakiwa na mpira shape yao ya 2-4-4 walikuwa na uwezo mkubwa sana
1.Kuweka presha kwenye sanduku la kwanza la CR Belouzidad
2.Bila mpira walijitahidi kuwa na muundo mzuri wa pressing 4-5-1
3.Walicheza kitimu sana (Collective play)
NB
Pacome ni Chama mtupu.
Full-time
Yanga 4- 0 CR Belouzidad
20/02/2024
Kombo Tactical Analysis
Mwananchi Hampiga Polisi
✍️Polisi Tanzania walikuwa na madhaifu makubwa haya
✍️1.Walishindwa kuizuia vizuri Yanga kwenye mapama ya uwanja hasa ufanisi wa miguu ya Augustin Okrah.
✍️2.Kila Pasi au krosi iliyokuwa inapigwa kutoka pembeni mwa uwanja ilikuwa inaitawanya safu ya ulinzi na kuacha space kubwa ambayo Guede alikuwa vyema kwenye kuishambulia hasa yale magoli 2.
✍️3.Agustin Okrah alikuwa na mechi kasi, uwezo wa kutengeneza nafasi, kushinda matukio ya 1v1. 🔥
✍️4.Joseph Guede yale magoli ya leo ni muhimu kwenye kumaliza mikosi yake,yataleta confidence yake.
Full-time
Yanga 5-0 Polisi
19/02/2024
Kombo Tactical Analysis
Azam Kasimamishwa Pale Tabora.
✍️Tabora United walikuwa bora sana kwenye kutengeneza nafasi leo hasa baada ya kushinda mpira wakiwa wanazuia kwenye 4-4-2.
✍️Tabora walikuwa vyema kwenye kutengeneza nafasi kupitia mapana ya uwanja yaani walikuwa na runners wazuri hasa yule
✍️Tatizo kubwa la Tabora United lilikuwa kwenye matumizi ya nafasi hawakuwa makatili kabisa mbele ya goli.
✍️Azam leo walikuwa chini hawakuwa na sharpness kabisa hasa eneo la mwisho (offensively they not good ).
Tabora Leo walicheza vizuri sana.Azam wamepoteza alama muhimu kabisa kwenye mbio za ubingwa.
Msimamo wa Ligi Kuu
1.Yanga Alama 43
2.Azam Alama 36
3.Simba Alama 36
NB.Simba ana mchezo mmoja mkononi.
19/02/2024
Hekaya za Kombo
Tamko la Mwenyekiti wa Mtaa
Mwenyekiti wa mtaa mzee Kamwe Kindoki ametoa tamko kwamba siku 24/02/2024 kila raia wa jamhuri ya jangwani lazima kichwa chake kikatwe nakupandikizwa kichwa kingine,kichwa ambacho kitakuwa na akili na rangi za zidane kwenye pacome day,hili sio tu tamko ni kauli ya kimamlaka ya serikali ya jangwani ni lazima izingatiwe.
Tamko la mwenyekiti wa mtaa Mzee Kamwe Kindoki linasisitiza sana kuhusu mwaraabu kuzikwa pale lupaso sio kaburini isipokuwa juu ya kichwa kilichojaa rangi cha zidane wa Ivory Coast,tamko halijaacha pia kusisitiza kuhusu moyo wa kila mwanachi kusukuma damu katika mtindo wa Kipacome Pacome siku ya 24/02/2024 pale nyumbani lupaso.
Mwenyekiti wa mtaa Mzee Kamwe Kindoki pia kichwa chake kitakuwa kimejaa vichwa vidogo vya Zidane moyo wake utakuwa hauna haja na matumizi ya damu hisia za zidane zitatosha tu kufanya kila kitu kiende sawa katika mwili,hili tamko halijamgusa tu raia wa kawaida pale jangwani isipokuwa mpaka mtoa tamko mwenyekiti wa mtaa mzee Kamwe Kindoki.
17/02/2024
Kombo Tactical Analysis
Yanga Yakusanya Kodi Kiurahisi
KMC walikuwa chini sana kwenye mambo haya
1.Hawakuzuia vizuri kwenye 4-4-2
KMC bila mpira walikuwa wanazuia kwenye muundo wa 4-4-2,Yaani Waziri Junior na Awesu walikuwa wanaanza kupress mbele ya Job na Bacca na Kisha wachezaji 8 waliobaki walikuwa wanatengeneza mazingira ya 8v 8 dhidi ya Yanga.
1.1 KMC kwenye mazingira ya kuzuia kwenye 8 vs 8 walishindwa kufanya haya
a. Walishindwa kutengeneza ya mistari inazuia karibu karibu
b.Kuzifunga nafasi vyema
2.Pasi zilikuwa zinapotea kirahisi
KMC Kuna muda walikuwa wanapoteza pasi kirahisi sana hasa kwenye maeneo hatarishi (sanduku la 1 na 2).
Kuna muda pia pasi zote zilizokuwa zinatoka nyuma kwenda kwenye sanduku la mwisho zilikuwa zinaishia kwa Bacca na Job.
3 .Build up yao ilishindwa kuishinda pressing ya Yanga.
KMC walishindwa kabisa kuivunja vunja pressing ya Yanga ambayo ilikuwa inatengenezwa na mzize+Max+Aziz na Pacome (pressing structure).Kwasababu
a.KMC walikuwa wanapiga pasi nyingi zisizokuwa na ulazima wakati wa build up.
b.Kushindwa kupiga pasi chache za haraka haraka hasa nyuma ya migongo ya wachezaji wa Yanga waliokuwa wanaanza kupress (Max,Aziz,Pacome, Mzize.
Yanga wakiwa na mpira Leo watu hatari walikuwa ni
1.Kibabage
Kwasababu ya uhatari wake wa kukimbia hakiwa hana mpira mguuni (off the ball movement),angali goli la Pacome.
2.Pacome
Kwasababu ya uwezo wake kucheza kwa kubadilisha maeneo,uwezo wa kukaa na mpira na kupiga pasi.
3.Mudathir Yahya
Kwasababu ya uwezo wake kucheza nyuma ya safu ya kiungo ya KMC na hasa kufanya mikimbio bila kuelekea mbele ya goli. ( Off the ball movement).
Full -Time
KMC 0-3 Yanga
15/02/2024
Kombo Player Analysis
Kuwa mkweli kati hawa nani kaonesha kiwango kibovu toka asajiliwe.
1.Joseph Guese
2.Fredy Michael
Powdered by
15/02/2024
Kombo Player Analysis
Kwa mujibu wa ndugu huyu mshambuliaji ni Bure kabisa.
Naomba tujadili huu mtazamo.
Powdered