20/12/2025
Bado masaa machache tukutane uwanjani.
Hakuna Kiingilio, mkaribishe rafiki amkaribishe rafiki.
Mahali : Jimboni VTC
Muda: 10:00 jioni.
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Geita Basketball league, Sports League, Geita.
20/12/2025
Bado masaa machache tukutane uwanjani.
Hakuna Kiingilio, mkaribishe rafiki amkaribishe rafiki.
Mahali : Jimboni VTC
Muda: 10:00 jioni.
10/03/2025
Familia ya Wanabasketball yazulu nyumbani kwa HASSAN SAI. Ambayo iliyoongozwa Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa kikapu mkoani Geita, Ndg. Eric Rumbagi. Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Ndugu. Deodatus Mnazi, Mratibu wa Ligi ya Mkoa Ndg. Adam Mayeye na baadhi ya wachezaji katika uwakilishi kutoka team ya Mpira wa kikapu ya Mkoa wa Geita ambapo Marehemu alihudumu k**a mchezaji na mwanachama hai wa shirikisho hilo, pamoja team ya mpira wa kikapu ya Mgodi (GGML)
Aidha, tukio hilo liliambatana kufika nyumbani kwa Mama wa Marehemu na kutoa neno la Faraja na uwasilishaji wa salamu za rambirambi, kuzulu mahali alipopumzishwa Mpendwa wetu. Kisha kucheza mchezo wa kirafiki na Home team ambayo alikuwa akiichezea Marehemu enzi za uhai wake, Musoma Heroes.
Tunamshukuru Mama, Ndugu na Marafiki wa Marehemu waishiyo Musoma kwa mapokezi mazuri, hakika mlitukarimu.
K**a Chama, Vilabu vya mpira wa Kikapu Mkoani Geita, Mashabiki na Wadau mbalimbali wa mchezo huu, hatuna budi Kumshukuru Mungu maisha ya Ndg. HASSAN, na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe pumziko la Milele....
Pumzika kwa Amani, HASSAN SWAI.
17/12/2023
Matokeo ya mchezo wa kirafiki kati ya Geita Basketball dhidi ya Sengerema Hoopers, ambapo Geita iliibuka na ushindi wa tofauti za alama 46 yaani 113 -67.
Ulikiwa ni mchezo mzuri. Tunawashukuru wote mliojitokeza kushirikiana nasi.
15/12/2023
WEEKEND HII 🔥🔥Kesho tarehe 16/12/2023 siku ya Jumamosi, Timu ya mkoa wa Geita inataraji kuwakaribisha Sengerema Hoopers (kutoka Sengerema) katika mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kupigwa majira ya Saa 10 jioni,Karibu ujumuike nasi katika kuiitia ushindi huo. HAKUNA KIINGLIO!!!
Don't plan to miss.🔥🔥🔥🔥🏀🏀 karibuni sana.
14/11/2023
CHAMPIONS🏆🏆🏆 2023
14/10/2023
04/10/2023
Alhamisi Hii🔥🔥🔥
Kesho, Tarehe 05/10/2023 uenda ikawa siku ya FURAHA au HUZUNI kwa moja ya Mahasimu hawa, VIPERS v ROCKETS.
Ni mchezo wa tatu, unaokwenda kuamua nani anakwenda FAINALI. Ikumbukwe, ameshinda Nyumbani na kupoteza Ugenini arikadharika, wameshinda Nyumbani na kupoteza Ugenini.
Je, Ni nani anakwenda kukutana na Golden Kings FAINALI?
Majibu yatapatikana kesho. USIPANGE KUKOSA!!!!!!!
MUDA : SAA 10 JIONI (16:00hrs)
ENEO : JIMBONI VTC
02/10/2023
Matokeo ya mchezo wa pili wa mtoano, Playoffs. Jana, Tarehe 01/10/2023
Golden Kings wameendeleza ubabe wa kutofungwa. Mara baada ya kumfunga mpinzani wao KATORO WARRIORS kwa tofauti ya Alama (22) na matokeo hayo, Mashujaa wa Katoro wanakuwa wa kwanza kuaga michuano. GOLDEN Kings wamefuzu Fainali.
Mchezo wa pili, VIPERS dhidi ya ROCKETS Ulimalizika kwa tofauti ya alama (9) ambapo Rockets waliibuka washindi katika mchezo huo. Hivyo mchezo wa TATU (3) unakwenda kuamua nani atafuzu.