Sports Conner

Sports Conner

Share

Pata hadithi za kusisimua zenye kuburudisha, kufundisha, kuelimisha pamoja na kukuacha na tabasamu

14/02/2026

Kivuli Cha Lowe 3

13/02/2026

KIVULI CHA LOWE SEHEMU YA 2

12/02/2026

Kivuli Cha Lowe Sehem ya 1

25/09/2025

Goli la Sowah

18/09/2025

🚨🇿🇦Naona kuna agenda zinapikwa na WanaSimba wameanza kujaa kwenye hiyo presha

Simba imteme Fadlu? Why? Kisa kufungwa na Yanga? Guys,hakuna kocha ulimwenguni atamfundisha mchezaji namna ya kuscore,hayupo ila kocha anaifundisha timu namna ya kutengeneza nafasi hapo ndo mwisho wa maelekezo ya mwalimu

Simba sc ilipata clear chances nyingi dhidi ya Yanga hii inamaanisha Simba sc ilikuwa na uwezo mkubwa wa kushinda mechi kupitia mbinu za huyu genius ila mwisho wa siku Kibu D anapoteza, Maema the same na hata Mukwala,je Fadlu alitakiwa kuvaa njumu aingie yeye?

Guys Simba sc mpaka inafika Fainali ya CAFCC sio quality ya wachezaji,ni tactics za kocha I'm 100% sure ile timu angepewa kocha mwingine ambaye hayupo committed Simba isingetoboa hata kwa Al Masry

Fadlu kwenye match zote dhidi ya Yanga sc mechi ambayo alizdiwa kimbinu nu moja Tu,tena ile ya mwisho wa msimu otherwise ni either wachezaji kutotumia nafasi ama makosa ya wachezaji wenyewe au waamuzi

Mtu aniambie ni sababu zipi inajadiliwa Fadlu aondoke Simba sc? kuna presha imesetiwa hapa,mkijaaa tu mmekwisha

I see the glory days under Mr Davids

17/09/2025

Ameandiks Jemedari

IMEKUWA MUDA MREFU SASA tangu Emile Mpanzu Kibisawala aonyeshe kiwango cha juu kwenye mechi kubwa. Mara ya mwisho kuwa katika kiwango kikubwa na cha kuvutia ni dhidi ya Stellenbosch pale Amaan Zanzibar kwenye mechi ya nusu fainali ya kwanza ambayo Simba walishinda 1-0. Baada ya hapo amekuwa abiria kiwanjani kwenye mechi zifuatazo
Vs Stellenbosch - away
Vs Berkane - away
Vs Berkane - home
Vs Singida - home
Vs Singida - away (FA)
Vs Yanga - away
Vs Yanga - away (Ngao)

Mchezaji mkubwa anajipambanua kwenye mechi kubwa, lakini Kibisawala alituonyesha hicho kwenye mechi 2 za Robo Fainali na Al Masry, kisha nusu fainali ya kwanza halafu akazima gari kwenye gear mpaka wa leo.

Baada ya kucheza nusu msimu wengi walikuwa na imani msimu huu anakwenda kuua, lakini sio tu hawezi kuua hata silaha ya kuulia nadhani haijui ni ipi, anapaswa kuamka Simba inamhitaji kiwanjani kuliko kwenye zile hype za usajili.

Naamini bado kuna muda wa kuendelea kuzoea ligi na mambo mengine, lakini yeye ni mchezaji mkubwa kuna wakati anapaswa kuofa kitu sio kuwa mufilisi kabisa kiwanjani.

BİN KAZUMARI MTIPA.

24/02/2024

UKIJAA TU KWENYE MFUMO ....... utaenda kuhadithia .!

✍🏻Performance ya hali ya juu sana , kila mchezaji katoa 100% yake uwanjani , ufundi , mbinu , umakini ( yes hii ya umakini ngumu kuwa 100% Binadamu hao ) , Yanga SC walihitajika ku turn up na wamwwapa mashabiki wao ladha ya " PACOME DAY "

✍🏻Gamondi alifanya kile ambacho kocha unatakiwa kufanya " wachezaji wako wakae kwenye nafasi hatarishi kwa mpinzani " . Aziz , Pacome na Maxi ni lazima :-

1: Wacheze karibu karibu sana , ili kufanikisha madhara kwenye mita 25 za mwisho

2: Hakikisha wanakuwa katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo wa timu pinzani ( between the lines )

3: Ili kufanikisha hili inahitaji wachezaji wanne takribani watano wafanye kazi zao kwa ufanisi , ambao ni :-

A: Fullbacks wawe wana overlap pembeni ili kufanya Pacome na Aziz kuwa ndani zaidi

B: Mshambuliaji ambao sio static yani yule anayesimama tu bali anayefanya sana runs , kwanini kuwahamisha mabeki wa kati wa timu pinzani

C: Mudathir kufanya sana forward Runs :inahitaji energy ya hali ya juu sana , akifanya hivyo maana yake anateka akili ya viungo wa timu pinzani

D: Aucho passing kupita kwenye mistari hasa mstari ule wa kiungo wa timu pinzani

Na Yanga leo walifanya hivyo vitu kwa umakini wa hali ya juu sana na ufanisi sana.! Gamondi lazima ajivunie .

✍🏻CRB leo hawatokuwa na lawama , kuna ambacho unafanya kwa usahihi halafu kuna mpinzani wako kuwa bora zaidi katika siku husika , spaces walizokuwa wanaziacha leo ziliadhibiwa kwa ufanisi zaidi na pengine watajiona wana bahati sana ya kuruhusu 4-0 pengine ingekuwa 6 au 7 ... ni hatari kuwapa wachezaji wazuri muda na nafasi kwenye mpira

NOTE

1: Mudathir ile energy yake ni kitu muhimu sana kwa kiungo cha Yanga , runs zake 🔥

2: Yanga , walikuwa wanawababua CRB hata wiki leo kwa nafasi bora walizopata

3: Walinzi wa Yanga na Diarra .. perfect game 🔥

4: Wale three AMIGOS ( Aziz Pacome na Maxi ) wakiwa na mechi nzuri kazi unayo

5: PACOME ... unasema nini kwake ? What a player .! Anacheza na swagga sana , maarifa mengi.!

6: Robo fainali ileeeeeeeee.!

7: CRB wanajua wamefungwa na timu bora uwanjani

FT: Yanga SC 4-0 CRB

19/02/2024

Mlinzi bora Ligi Kuu Henock Inonga baada ya kufanya vizuri Afcon 2023 pale nchini Ivory Coast na Taifa lake la DR Congo zipo klabu kadhaa ambazo zinataka kumsajili.

Kwa sasa Inonga ana umri wa miaka 30 na tufahamu kasumba ya wachezaji wa Kiafrika katika ishu ya umri wengi wanadanganya kwa maslahi yao.

FAR Rabat ya Morocco ni miongoni mwa timu ambayo inahitaji saini na Henock Inonga na taarifa zinaeleza wapo tayari kutoa Bilioni 2tsh ila Simba wanaomba thamani ya Inonga ni zaidi ya hiyo pesa.

Katika umri wa miaka 30 alafu inakuja ya Bilioni 2tsh nadhani hapa Simba wanapaswa kumuuza ili wakanunue beki mwenye umri mdogo ambaye pia wanaweza wakaja biashara nzuri baadae.

NB: SIMBA MKIACHA HII PESA HUYU HENOCK ATAKUJA KUONDOKA BURE BAADA YA MKATABA WAKE KUISHA.

12/02/2024

Simba SC imevuna alama 10 kati ya alama 12 kwenye michezo minne mfululizo nje ya Dar Es Salaam, Simba SC imecheza Kigoma, Tabora pamoja na mwanza ambako wamecheza michezo miwili.

Kwenye michezo hiyo minne Simba SC imefunga mabao saba (7) na imefungwa bao moja
▪︎Mashujaa FC 0-1 Simba SC
▪︎Tabora United 0- 4 Simba SC
▪︎Simba SC 1-1 Azam FC
▪︎Geita Gold FC 0-1 Simba SC.

Michezo Ijayo ya Simba SC, NBCPL.
▪︎JKT Tanzania vs Simba SC, Februari 15.
▪︎Simba SC vs Mtibwa Sugar, Februari 18.

12/02/2024

Nimeona leo mshambuliaji Fiston Mayele ameamua kusema hadharani anachukizwa na mashabiki na baadhi ya viongozi wa Yanga SC.

Binafsi mimi naona inaweza kuwa fundisho kwa vilabu kuwa vinapaswa kudili na wachezaji kidemokrasia hata wakiachana iwe ni kwa amani na kuweza kuridhiana.

Wachezaji na makocha ni wafanyakazi na sio mashabiki au wapenzi wa vilabu, hivyo nao wapo kutafuta maslahi wakati vilabu vipo kupambana na malengo yao.

Sasa inapotokea wanatofautiana isiwe chuki na mihemko bali ni demokrasia ya kuachana ili iwe rahisi kurudiana wakati mwengine au kukaribishana hata kwenye matukio na kunywa kahawa kwa pamoja.

09/02/2024

Clatous Chama ameziokoa alama tatu ambazo Azam FC walizishikilia kwa muda mwingi wa mchezo.

Timu zote leo zilistahili ushindi, Azam FC walicheza vizuri na Simba SC pia wamecheza vizuri licha ya kuruhusu bao ambalo limewaondoa kwenye mipango yao mapema.

MATOKEO YAO KWENYE MICHEZO MITANO.
▪︎Simba SC 2-1 Azam FC.
▪︎Azam FC 1-1 Simba SC.
▪︎Azam FC 1-0 Simba SC.
▪︎Simba SC 1-1 Azam FC.
▪︎Azam FC 1-1 Simba SC.

FT. Simba SC 1-1 Azam FC.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Ikwiriri?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Nyerere Road
Ikwiriri