TAMTHILIYA YA LIMENIKUTA
MTUNZI: REHEMA.D.MUHOZYA
ONYESHO LA KWANZA( SIKITIKO)
Asubuhi na mapema kelele za ndege zinasikika mithili ya watoto walioachwa na mama yao aliyeelekea katika shughuli za kutafuta riziki.Muuza duka anaonekana akifanya usafi nje ya duka lake huku akiwa anaimba
" Kazi yangu ya dukani ooooh!! yaniweka matatani ooooh!! wanaonirudisha nyuma wengi ni majirani ooooh!!"( Ghafla anaonekana mama mmoja aliyevaa nguo mithili ya mwendawazimu akijongea mpaka kwenye mlango wa dukani
Muuza duka: karibu mama shikamoo
Mama: Marhaba mwanangu za mwamko?
Muuza duka: salama tunamshukuru Mungu eeh! nikuhudumie nini mama.
Mama: samahani kijana wangu mimi sina hela ila nahitaji unga wa dona kilo moja,maharage nusu na kipande kimoja cha sabuni ya magadi.Kesho nitaleta hela Yako naishi pale kwa mzee zwazwa.
Muuza duka:. Hivi mama huoni aibu asubuhi yote hii kusimama kwenye maduka ya watu kukopa kweli? Hata k**a unahitaji kukopa ndio asubuhi,samahani kwa hilo sitaweza kufanya hivyo kwasababu ndio kwanza nimefungua na sijauza hata mia mbovu
Mama: kijana wangu nisaidie tu hela nitaleta kesho wala sitakusumbua.
Muuza duka: mama mbona nimeongea kiswahili tu nimesema hivi ndio kwanza nimefungua na bado sijauza
Mama: sawa nimekuelewa,ila nakuomba unisaidie kwa leo.
Muuza duka: mama nenda usije kuniharibia " mood" yangu asubuhi yote hii, Yani Kuna watu wameubwa kuwakera wenzao
Mama: kijana wangu haya ni maisha tu Kuna kupata na kukosa.
Muuza duka: wewe mama ni mchawi mbona uko k**a kupe k**a unaona ni rahisi fungua duka lako uwe unachukua unachokitaka
Mama: sawa kijana wangu nisamehe kwa kukukwaza asubuhi yote hii ila ni shida ndio zinasababisha. Mama aliondoka dukani hapo na kushika njia ya kwenda nyumbani kwake Ili atafute njia nyingine ya kujipatia riziki kwa siku hiyo.
ONYESHO hili litaendelea kesho 16/12/2023.
Mjukuu wa muhozya
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mjukuu wa muhozya, Sport & recreation, Mwanza jiji, Ilemera.
Wale mnaoendelea kujumuika nami karibuni sana ninatambua mchango na nafasi yenu kwangu.
Wadau wapenzi wa hadithi siku ya tarehe 12/12/2023. Hadithi yetu tuliyoisubiri kwa muda itakuwa inatoka naamini mtafurahi.
Wapenda muda unakaribia kaeni mkao wa kula
Mnao jiunga katika ukurasa wangu karibu Sana na mjisikie mpo sehemu salama na mtajifunza vitu vizuri.
Wapendwa samahani kwa usumbufu naamini mnaendelea vizuri kwa msaada wa mungu rasmi 12/12/2023.tamthiliya yetu yetu ndio inakuwa mubashara kwenu wadau kwasababu Kuna sababu za kimaandalizi zimeingiliana naamini wapendwa wangu ni waelewa.
Wadau wangu pendwa katika tasnia hii ya fasihi kwa maandishi naamini mnaendelea vizuri na Leo ndio ile siku ya kuachilia tamthiliya yangu kwa jina la UBINADAMU UTATA hivyo kaeni tayari.Asanteni
Kuanzia tarehe 23/11/2023.Nitaachilia tamthiliya yangu inayotambulika kwa jina la UBINADAMU UTATA wadau wangu naamini mtapata kitu kizuri.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Website
Address
Mwanza Jiji
Ilemera