08/03/2024
TAASISI 5 BORA ZA MPIRA WA MIGUU TANZANIA KWA SASA .
Kutokana na utafiti niliyoufanya hizi ndo taasisi 5 bora za mpira wa miguu nchini:
1. YOUNG AFRICANS SC.
Hii ndiyo klabu ya mpira kongwe zaidi nchini Tanzania ikianzishwa mwaka 1935(89yrs) yenye makazi yake katika mitaa ya twiga na jangwani jijini dar es salaam. Young Africans imekuwa timu popular saana kwa sasa barani afrika kutokana na uwezo mkubwa walionao ndani ya pitch kutokana na uwekezaji wao walioufanya miaka ya hivi karibuni. Young Africans imefanya Real football transformation hapa unazungumzia mfumo bora wa uongozi ndani ya timu, mpka sasa klabu ya yanga SC ipo phase Three ya transformation (Fans engagement) ambapo phase four watamalza na kukaribisha wawekezaji ndani ya timu. Ikumbukwe kufanya real football transformation hapa nchini Tanzania imekuwa ngumu saana kwa vilabu vyetu kutokana na mazingira yetu. Hvyo kutokana na transformation hiyoo imewafanya yanga SC kuweza,,,,,
๐Nbc premier league 2x๐
๐CAF CC final ๐
๐CAF CL quarter final ๐น
Nakuweza kuwafanya wakusanye alama 31 za CAF ndani ya miaka 2 tu na klabu pekee africa kufanya hvoo ndani ya misimu 2 tu ya mashindano.
Klabu ya yanga SC pia imeweza kushika nafasi ya 2 Africa Kwa numbers kubwa za mashabiki (35m fans) nyuma ya Al ahly ya misri yenye fans wengi zaidi africa ( 70m+ Fans).
Kwa Data hizo unaweza kutambua ni kwa kiasi gani klabu ya yanga SC imechangia kukuza soka hapa nchini maan haya ni baadhi tu ya mafanikio yanayokeletwa na timu hii kubwa nchini.
2. SIMBA SPORTS CLUB
HII ni miongoni mwa timu kubwa nchini Tanzania ikianzishwa mwaka 1936(88yrs) . Simba sc imejaribu pia kufanya transformation ikiishia phase one na kukwama kutokana na sababu mbali mbali za kimitazamo na kimazingira. Kutokana na uwekezaji walioufanya Simba sc wamefanikiwa kuweka idea of international football in Tanzania kwani wamefanikiwa,,,,
๐Kubeba Vodacom pl 4x๐
๐ Quarter final 4xโ๏ธ CCL
๐ Quarter final 1xโ๏ธ CAF CC
Kutokana na mafanikio hayo Simba sc imeweza kushiriki kwa kiasi kikubwa kukuza mpira hapa nchini Tanzania ikichangia alama 39 ndani ya miaka 5 ya ushiriki wao ktk mashindano ya CAF na kuwafanya kushika nafasi ya 6 kwa vilabu barani afrika. Pia imefanya vilabu vingine hapa nchini kuweza kui implement the idea of international football in Tanzania hivyo kuongezeka kwa vilabu vinavyofanya vzr kimataifa. Simba pia ni Moja ya vilabu maarufu barani afrika inayokadiliwa kuwa na zaidi ya mashabiki 10m kutokana na utafiti uliofanywa na mtandao wa African soccer zone.
Simba imefanikiwa kuwa na kandanda safi ndani ya pitch na kuvifanya vilabu vya mataifa kuheshimu zinapokutana na vilabu vya Tanzania especially waarabu ambao wamekuwa hawatoki na kitu kwa mkapa mbele ya Simba sc .
Nb: nafasi ya 3,4&5 zidaendelea soon get turned ๐ค
22/10/2023
๐๐๐UKIMUITA TU ANASAHAU KILA KITU ๐ฏโ๏ธ
22/10/2023
HII WATOTO WA 2000 HAWAWEZI ELEWA ๐ฏ ila wachina waongo nyiee๐๐๐
21/10/2023
๐๐๐HII INAITWAJE KISAYANSI ๐ค
21/10/2023
SIO TU TANZANIA HATA WAKENYA WENYEWE WAMELIKUBALI VIBE LA WATANZANIA KATIKA SOKA.
18/10/2023
Hahahaha noma saana ๐ฏโ๏ธ
18/10/2023
HILI NDILO GAPE LA SIMBA SC KWA YANGA SC KIMATAIFA.
Ni wazi ushiriki wa Simba sc kimataifa umeleta tija saana kwao na taifa kwa ujumla
Wamefanikiwa kupanda katika rank za timu barani Africa kulko timu yeyote Tanzania, Africa mashariki na kati hiyo imekuja baada ya Simba sc kufika robo final ya club bingwa mara 3 mfululizo na kombe la shirikisho mara 1.
Ukiangalia haya mafanikio hayaji kirahisi tu kwa kukurupka tu na kufanya bali mipango mikakati thabiti na uwekezaji pia. Leo unaambiwa Simba sc ndo timu pekee inayowakilisha ktk mashindano ya juu kabsa barani Africa AFL (African football league) .
Kitu ambacho kitabaki kuwa history katika maisha ya SOKA Tanzania hata k**a kunatimu nyingine tokea Tanzania itakuja kushiriki maana mashindano haya yameanza k**a majarbio round hii jjapo siku za usoni timu zitaongeza zaidi ila history itabaki kuwa Simba sc ilicheza robo final ya AFL.
Mwisho.
Ili Simba sc kuendeleza walichokianza wanahitaji proper football management & more investments . Naiona YANGA SC siku za usoni ikiwa timu bora saana katika uwakilishi wa kimataifa kwasababu ya proper football management na uwekezaji walioanza sababu soka la sasa linahitaji uendeshwaji wa kisasa saana.
Simba sc hongera kwa hatua 1 mbele.
20/08/2023
yanga buru buru, aziz ki huyu hapa ๐ฅ pini za mpilipili
๐good start kwa miguel gamond kimataifa hana presha yanga inaonekana kuwa na balance nzuri na flexibility kuanzia nyuma mpaka unampata aziz ki ushindi wa yanga ulianzia kwenye utamamu wao wa mwili na ubora wa kikosi chao
๐dickson job & mwamnyeto hii ndio combination bora ya ulinzi kwa yanga inapokutana na timu iliyofunga mianya zobe to zone asas djibout waibana sana mianya uwezo wa kupush wa job na mwanyeto uliwasaidia aucho na mudathir kuwasogelea zaidi aiz na wenzake.
๐yao yao na lomalisa was super today walikuwa wanaflow vzr na confidance ya hali ya juu hawakupata bugdha waliinjoy soka yule yao yao beki haswa akiweza kumwaga maji yanga watamuimba sana
๐azik ki amekuwa msupa sana sasa unaweza kusema anaibeba yanga mabegani katka safu ya shabuliaji kwa sasa ndie mhimili wa safu ya ushambuliaji wa yanga ameongeza hai ya kupambana now sio kijana mvivu tena
๐kenedy musonda & mzinze wote ni washambuliaji wanaotegemeana hawawezi kusimaa wenyewe na kuamua mechi inshort sio typical strikers bao zuri lakini anahitaji kuimprove zaidi
๐mrithi w mayele hafidh konkon nj mapema mno kumjudge lakini tumpe benefit of doubt kwa sababu ya kuchelewa kujiunga na kambi tukiamini hayupo fit enough kuanza ndio maaa gamond ameamua mwaba mechi zote atokee benchi hizo chance mbili alizopata alistahili kuwainua yanga pale chamanzi.
๐pacome zouzua ni tactian anajua ball but ni soft sana unapopata zaud ya dakika 30 dhidi ya timu k**a hii ambayo inashida ya wachezaji wao kukosa fitness na ambao hawakudisturb tunategemea angeonyesha zaidi ya 100% ya uwezo wake but haikuwa hivo
๐ukweli mchungu ni kuwa : gamond ball inatembea lakini yule konki master sio yikpe mpya kweli..?
20/08/2023
"YANGA SC YAANZA VYEMA KIMATAIFA"
Katika mchezo wa leo YANGA SC vs ASAS Djibouti Telecom, ni k**a YANGA SC waliingia na pressure hivi kutokana na malengo waliojiwekea msimu huu kimataifa kufika makundi club bingwa pia ukisikiliza mahojiano ya mwalimu MIGUEL ANGEL GAMONDI ni k**a Alikuwa hafahamu vizuri uchezaji wa ASAS DJIBOUTI TELECOM hivo ikapelekea kukosa utulivu wa nyota wa club ya YANGA SC hasa katika idara ya ushambuliaji, musonda & mzinze bado wana pressure nani kuvaa viatu vya mayele. Yote kwa yote idara nyingine walikuwa vema saana wameupiga mwingi, midfielders, defenders ๐ฅ
Note
1. Aucho anatukumbusha kuwa yeye ni daraja la juu๐ฅ saana.
2. Yao ni mtu na NUSU.
3. Job ni yuleyule hajawahi bore๐
4. Zouzoua ni mtu saana apewe muda โ๏ธ
5. Gamondi ni fundi boli linatembea kwa kasi ya 4G ๐ + mipasi
20/08/2023
"SIMBA SC YAKWEA KILELENI ๐ฅ
Baada ya mchezo wa leo Simba sc imejikita kileleni ikimshusha AZAM FC lakin Azam akiwa na mchezo mmoja mkononi.
18/08/2023
"WAMEPATA MATOKEO LAKINI HAWANA FURAHA "
Naweza sema hivo mnyama wa mwituni Simba sc ameshinda lakini hawana furaha kutokana na mpira unachezwa na klabu ya Simba sc siku hz, hasa ukizingatia game tatu walizo cheza msimu huu umekuwa tofauti kabsa yaani hauna structure maalumu angalia game dhidi ya singida fountain game, YANGA SC na mtibwa sugar leo utaelewa nn namaanisha.
Nazan sasa kocha Robertinho kikosi kimekuwa kikubwa kuliko uwezo wake na amekuwa muoga kutumia siraha alizo letewa msimu huu ni wachezaji wa3 tu kati ya zaidi ya 9 walosajiliwa msimu huu ndo amekuwa akiwatumia nazungumzia w***y essomba onana, Fabrice Ngoma & che Malone.
Simba sc sio mbovu lakini kocha Robertinho ndio bado anakuwa mbovu katika upangaji wa kikosi pia Simba sc walifeli kumuacha JUMA MGUNDA, Alikuwa msaidizi mzuri saana wa Robertinho Oliveira. Improvement inahitajika kwa haraka saana vinginevyo Oliveira hatakula Christmas ๐
Note.
1. Jose miqussone amekuwa mzito tutegemee ubora kuanzia mwezi wa 10 hv sio tunayemjua.
2. Chama sometimes anakera lakini anapoza. Slow but sure.
3. Che Malone ni bora lakin leo kapuyanga labda tusubr chemistry yake na Inonga
4. Ally salimu ni kipa sijaona kosa la peke yake leo ISIPOKUWA safu nzima ya ulinzi ya Simba sc.
5. Mganga wa kibu nomaa mzungu anamuona k**a Messi ๐.
6. Mtibwa wamepambana kikubwa leo, matheo Anthony ๐