19/12/2025
RONALDO DE LIMA COULD DRIBBLE LIKE A WINGER AND RUN LIKE A SPRINTER, ASANTE MSELA WA BENTO RIBEIRO
Mitaa fulani Jijini Rio de Janeiro pale Brazil, Bento Ribeiro, hapo ni mitaa ya Kaskazini ya Jiji hilo, ilipewa jina jina kwa heshima ya Meya wao bwana Bento Manuel Ribeiro Carneiro Monteiro miaka ya 1910-1914
Ndio mitaa aliyotokea El Phenomeno, Ronaldo De Lima, kumradhi ni Ronaldo wa Brazil sio Ronaldo wa Ureno au Ronald aliyekuwa Rais wa zamani wa Marekani
Kuna masimulizi mengi juu ya fundi huyu, akibeba tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mara 3, 1996,1997 & 2002 bado alibeba mchezaji bora UEFA mara mbili 1997 & 2002
Ubishani ni De Lima yupi bora wa Cruzeiro, PSV, Barca au Inter Milan, sisi hayo hatuwazi sana ila kuna mwamba mmoja kutoka Ufaransa alidai kulikuwa na De Lima wawili mmoja wa kabla ya majeruhi na mwingine wa baada ya majeruhi😀🙌
Mzee mmoja pale Kihesa Iringa anadai kuwa kwenye nafasi ya Center forward kuna watu watatu bora kuwahi kutokea, huyu De Lima, George Weah na Romario pekee 🙌
Hawa walikuja na style yao drop down to the midfield, switch pembeni kwenye flanks, vuta mabeki wa kati wakufate na chenga za maudhi sana 😀
Pale Nou Camp wale Wakatalunya na jeuri zao wakiona mnyama kaushika mpira kuanzia eneo la midfield kila shabiki anainuka, anapasua ngome kwa speed ya umeme, ndie binadamu mwenye kasi zaidi akiwa na mpira kuwahi tokea duniani, hats off Ma'men
Usiku mmoja wa fainali ya UEFA 1998, baada ya De Lima kumpita Alesandro Nesta, commentator aliishia kusema " He passed, he burnt and he humiliated Nesta!🙌... Simply he is extraterestial
Ronaldo anatumia miguu yote, anapiga faulo, mzuri kwenye aerial balls, kifupi ana kila kitu kwa ajili ya namba 9, ikiaminika ndie 9 bora zaidi kuwahi kubariki mchezo wa soka kwa hivi karibuni, kakutana na mabeki na makipa hatari wa zama zake, kumbuka 2002 dhidi ya Oliver Kahn pale Japan 🙌
He would dip the shoulders,stepped over and banged 🔥 Mzee kula tu maisha hapo Copa Cabana, wape hi Masela, Asante kwa kumbukumbu
Binafsi huku Ghetto hatukudai umetupa kila kitu🙏
18/12/2025
SIKU YA MAJONZI VALDEBEBAS MPAKA PLAZA DE CIBELES JIJINI MADRID
Wale wataalam wa Historia, wanadai falme iliyowahi kudumu kwa muda mrefu nchini Korea ni Joseon Dynasty kuanzia 1392-1897. Watu wa mziki wanaamini ngoma ya Ugali ya Juma Nature bado inaishi miongoni mwetu japo Nature sio yule tena, binafsi naamini 'Mtazamo' mkono wa Afande sele itabaki nasi japo Afande sio yule tena
Waswahili wa Pwani husema kila kitabu na zama zake, Wahehe kutoka Iringa wanasema 'Nothing is permanent' YES!
Ilikuwa Kuitazama Real Madrid sio issue sana ila utizamapo Madrid hakikisha umetupa macho kwa Nahodha Sergio Ramos kisha kwenye kiungo pale kwa Luka Modric kutoka nchi ya Kijamaa ya Croatia
Sergio Ramos kutoka Kusini mwa Hispania, Jijini Sevilla kwenye jimbo la Anderlucia, ni moja kati ya mabeki wachache sana kuwaona Ulimwenguni, Madrid watapata kisiki k**a kile?? Kwenye dunia hii yenye watoto mabishoo wengi, bado napata shaka
Luka Modric aliyesafiri kutoka mbali kutoka Mashariki mwa Ulaya mpaka Magharibi kote kueneza soka la burudani, tafsiri sahihi ya number 10, nae kashaaga na kuondoka yuko zake milan
Nizzo Forlove ananiambia Madrid wamepita watu bhana, Gento, Ferenc Puskas, Alfredo Di Stephano, Raul Gonzalez na Cristiano Ronaldo, lakini bado Ufalme uliweza kudumu, sipingani nae ila vipi kuhusu mabadiliko ya soka la kisasa, vipi kuhusu Sera ya Galacticos inawalipa kwasasa?? Jovic, Hazard, Diaz kwa pamoja wameifelisha kalamu ya Almasi ya Perez
Mabadiliko ya soka yanailazimu Madrid icheze k**ari kwa makinda, walienda Santos kumchukua Rodriygo, Vinicius wa Flamengo, Valverde kutoka Uruguay na sasa mbappe kutoka psg , Madrid wapo kwenye sera ya trial and error, Perez anawaza, Mariano Rajoy anawaza tutoke vipi?
Sipati picha hiyo siku miamba hii inarudi na kuaaga pale mazoezi Valdebebas, sipati picha sura ya alonso siku hiyo, wakati wanaenda kupiga makofi na kupata standing aviation pale Bernabeu, Madridista watalia mno
Mitaa ya Co**ha Espina itawakumbuka, Sanamu la Mwanamama pale Plaza de Cibeles litahuzunika, masela wa Calle de Alcala na Paseo Del Prado wote watahuzunika, Galacticos wanasepa zao, Sergio anarudi zake Sevilla na Luka anaenda kusabahi Croatia
16/12/2025
Wakati Mpo Bize mnawaza mambo ya Man United na sare yake kwenye mechi ya jana
Mimi nipo zangu mbali saana nakumbuka baadhi ya mambo.
Nimemiss RFA asubuhi ili usikie matokeo ya mechi za UEFA ambazo hujaziona kwakuwa kwenu TV hakuna basi utasikia NI KATIKA MICHEZO NA VODACOM hapo ule msauti wa Deo Makomba ni hatari!...
Ukishakula hiyo basi jioni baada ya kipindi cha 'KILIMO NA MFUGAJI' pale Radio Tanzania au TBC Taifa saa moja na nusu usiku, utasikia sauti ya Enock Bwigane au Ahmed Salum kukuletea michezo ya bila mchambu*i hiyo! Na anakupa vitu hatari
Tumetoka mbali bwana EPL kupitia TVT chini ya Mzee Juma Nkamia kwa udhamini wa RUNGU!...
Acha tu! Zamani bwana kulikuwa na burudani!
02/12/2025
Ipo siku MO ataondoka zake Simba na kutuachia timu yetu japo sitegemei litokee ila naliona likitokea, ipo siku GSM ataachana na Yanga na kutuachia timu yetu japo sitegemei likitokea ila naliona likitimia
Ipo siku watu wenye maono na fedha zao watatuachia timu zetu k**a tu*iitavyo, lakini najua haujawahi kuwaza watatuachia somo gani kubwa, tumeshafunua chungu na kuchungulia yajae?? Tushawahi kutoka nje ya box na kuwaza zaidi?
Wananiachia somo kuwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na TP Mazembe ni miongoni mwa timu chache Kusini mwa jangwa la Sahara kubeba ubingwa wa Afrika, zote ni timu zinamilikiwa na Maboss, Patrick Motsepe na Moise Katumbi, nimejifunza kitu
Wapo wasiotaka kuchungulia mbali watasema mfumo wa Hisa sio rafiki, ila mwambie kuwa Hispania klabu zao zote 20 ni timu tatu tu za Wanachama, Real Madrid, Barcelona na Bilbao zingine zote 17 ni mfumo wa hisa, tunataka kuwa k**a Madrid na Barcelona?? Kato sidhani
Real Madrid ili uwe Rais na Mjumbe kuna kitu kinaitwa means testing, Mgombea una mali gani, utajiri gani hii ina maana kubwa kwao wanataka maono makubwa ya kiuchumi, bado kuna kundi la Wanachama wanaitwa Socios, wawakilishi wa Wanachama zaidi ya million moja kwenye maamu*i ya klabu
Najua kwa zengwe zetu hawa watapita na kwenda zao, na sisi tumebaki na fikra zetu za kijamaa kwenye dunia ya kibepari, sioni Simba wala Yanga wakipiga hatua kwa mfumo wa Wanachama, tuna vingi vya kutukwamisha, ikiwemo kulipia tu kadi
Watapita na kwenda zao, watatuacha na ubishi wetu
30/11/2025
Bush stars... Nitajie majina ya kila mchezaji wa hiki kikosi
30/11/2025
MIKE TYSON MWAMBA MKUBWA ULIOTIKISA KABURI LA CUS D'AMATO
Mtoto mdogo kwenye mitaa ya Brooklyn Jijini New York Marekani, mbabe haswa anafumua watu bila huruma, kibaka na msela mno Mike Tyson, alihesabika k**a mtoto mtukutu pale New York
Rekodi mbaya za utukutu zilimpeleka Jela ya watoto kwa ajili ya kurekebisha tabia, ndipo huku Tyson alipopata muongozo wa maisha yake, ndipo huko alikutana na Mwalimu wa Ndondi bwana Cus D'Amato
Kumbuka D'Amato alivumbua kipaji kikubwa k**a cha Floyd Patterson, bondia ambaye nae alipata mafanikio makubwa sana, ilimchukua muda mchache kugundua kipaji cha Tyson, huku akiamini atailetea dunia copy ya Muhammad Alli
Ilikuwa ni usiku, asubuhi na mchana kila muda mazoezi tu kila muda ndondi, akiamini anailetea dunia balaa mpya kwenye masumbwi, Tyson aliiva sana ingali bado kijana mdogo
1985 D'Amato aliaga dunia ila akiamini tayari ndoto na kiu yake imetimia, alikubali kufukiwa huku akimpa kazi kijana wake, laiti angesubiri miaka miwili tu angeshuhudia balaa aloleta duniani
Tyson 1987 akiwa na umri wa miaka ishirini, ngumi zikitupwa k**a umeme, akijilinda k**a ngao ya Moran wa kimaasai dhidi ya simba, ndio Tyson mwenye ubora wa kufake miguu na mitupo🙌
Usiku ule wa 1987, anaweka rekodi ya kuchukua Ubingwa wa dunia akiwa na umri mdogo miaka 20 tu, ana IBF, WBA na WBF, ananyoosha mikono juu kwakuwa ni shujaa, ananyoosha mikono juu kumpa salaam Mwalimu wake tangu Jela
Licha ya ukweli kwamba Tyson hakutupa alichotaka Mwalimu wake zaidi, wengi wanaamini mikono ya Don King (Meneja wake) ndio ilimpoteza huku wengine wakiamini ni Wanawake waliommaliza
Nani anamkumbuka mrembo Robin Givens, Monica Turner au skendo yake na Mrembo Desire, wengine wanaamini ujio wa Evander Hoyffield au Lennox Williams ulitishia ufalme wake
Wengi watabaki na sababu nyingi za kupotea mapema kwa Mike Tyson, ni mwendelezo wa Ngonjera za watu weusi wakishafanikiwa pale Marekani, wanapotea mapema, ila popote alipo Tyson, ajue Mwalimu wake analia Kaburini
Tyson Tyson, sawa lakini ulishaamua ila funzo umetuachia, siku ukienda utamwambia nini Mwalimu wako?🤤
30/11/2025
MRISHO KHALFAN NGASSA 'SHIBOBO MASTER', UKISTAAJABU YA M***A UTAYAONA YA MWANA WA HAWA
Nakumbuka sana Mafundisho ya Dini, kile kisa cha Adam na Hawa (Mwanamke) alimshawishi Adam wale tunda la kati, matokeo yake ikawa mateso ila anguko hilo lilikuwa ni hatua muhimu katika maku*i ya Binadamu
Kutokana na anguko lile Mungu aliwaleta Manabii ikiwemo Massih Issa Bin Mariam, walikuja kulipia makosa ya binadamu kwa sharti ya toba, lakini bado kuna vitu vitasalia na mshangao mkubwa sana duniani
Wapo wapi watu wale walioshuhudia Mwanamke akilia kwa furaha na anaweza pia kucheka kwa huzuni, wapo wapi watu wale waliowahi kushuhudia akiacha mbachao kwa msala upitao, wapo wapi watu wale
Bado sijashangazwa sana na yote hapo juu, ila mshangao wangu ni maeneo ya ziwa lilopewa jina na Explorer John Hanning Speke 1858, aliliita Victoria kutokana na jina la Malkia wa Uingereza, hapo ndipo stori yangu inaanzia
Historia yetu inaanzia kwa Mzee Khalfan Ngassa 'Babu' nyota wa zamani wa Pamba 'TP Lindanda', alietamba 1991 kwenye u*i wa Simba akisimama k**a Kiungo aliipa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati, anafanya maajabu mbele ya Ramadhan Lenny, Idi Kibode, Bakari Iddi na Method Mogela
1991 hiyo Mzee anatamba, nyuma yake ana kichanga cha miaka miwili, Mrisho aliyezaliwa 1989, kirusi kingine cha mpira alochokileta kuendeleza jina lake, wakati Mzee anapokezana pass na Ally Bushiri, Kitwana Seleman, Hamza Mponda, Fumo Felician pale Lindanda, lakini kwenye nyumba moja Mama Mrisho anakilea kichanga
Judith Wambura 'Lady Jaydee' aliimba siku hazigandi, ikawa usiku na ikawa mchana, watoto wadogo pale Kirumba walianza kuhisi joto la jiwe na mpira sukari wa Mtoto wa Khalfan, nae ni Mrisho Ngassa, mbele ya Kelvin Yondan, Jerry Tegete na Henry Joseph Shindika
Hakuna aliewajali sana ila ni Toto Africans 'Wanakesha Mapanda' walitengeneza mzinga kwa ajili ya kufaidi asali ya nyuki wale, Haukuwepo Msomaji ila Malaika wako walikuwepo, kila mtu alipita njia yake kwa watoto wale wa Mtaa, ila Mrisho alielekea Kagera Sugar
Mrisho alikuwepo kikosi cha Serengeti Boys kile kilichofuzu Mataifa ya Afrika 2005, japo CAF waliwaondoa kwa sakata la umri wa Nurdin Bakari
Itaendelea
29/11/2025
Sahau kuhusu upinzani, mtazame Roberto Carlos akiburudika na burudani ya Ronaldinho😊
28/11/2025
Binadamu hawa wawili walikua wanaupiga mzigo kimya kimya, ni k**a yai bovu lililovishwa shuka, ni kazi kujua wanafanya nini uwanjani ila ulikua unaona mpira unahama kila sehemu😊
Lionel Messi ni gari moja lililokaa Parking na kuvutia sana, ila nyuma ya abiria aliokuwa anawaendesha kulikua na haya matairi ya mbele, kwenye hilo gari hilo, walikua wanaonesha muelekeo wa gari la Barcelona
Ukisikia Barcelona wanauza binadamu hawa wawili ingekua sio barani Ulaya, hawakua tayari kushuhudia hii miguu minne inapatikana tena Ulaya, watu walikua tayari kuvunja vibubu ku*ipata huduma hizo, ila moja ilienda Japan na moja ikaenda Qatar
Wewe unawaita viungo mimi nawaita grisi kwenye vyuma, nawaita nyundo pale Mahak**ani, nawaita sabuni ya roho kwa wapenzi wa soka, waliufanya mchezo wa soka uwe rahisi na kutazamika machoni, ilikua inaruhusiwa hata mtoto aliyezaliwa siku mbili zilitopita kutazama soka lao
Huku Hispania wale Traffic wakisimamisha ndinga zao walikua wanawaomba radhi kwa foleni, kisha hupiga picha na kwenda kuvimba Instagram, "NIKIWA NA INIESTA" "NIKIWA NA XAVI" ilikua sio rahisi kuwaruhusu wapite bila kula nao picha, haikuwa rahisi
Hakikisha ukipanda gari lao umefunga mkanda, k**a unacheza nao unaweza kuwa jicho nyanya usione wapi wanapeleka mpira, muulize Sir Alex Ferguson pale Wembley alitetemeka, Xavi peke yake aligonga pass kuliko United yote, Iniesta alikua k**a Hi**er mbele ya dimba, pass za mamlaka na maamu*i shupavu
Binadamu wachache kuwahi kutokea na kuufanya mchezo wa soka uwe rahisi, walikuja kubadili akili ya Eusebio kwenye kiungo pale Nou Camp, walikua duplicate ya Zinadine Zidane, walikua version tofauti na wakina Simeone walivyotafsiri kiungo, walikua binadamu wa aina yao peke yako😊
Guardiola aliaminiwa sana na Johann Cruyff, alitamani sana mtu acheze 4-3-3 aliyowaza kichwani mwake, Guardiola akaja kufaulu nayo akiwa Kocha chini ya Binadamu hawa, k**a sheli walikua full tank🙌
Asanteni kwa kumbukumbu Xavi Hernandez La Macquiao na Don Andres Iniesta Lujan
27/11/2025
DIEGO MARADONA, MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA KWENYE MIOYO YA WATU
Mkondo wa maji machafu, kelele za risasi, nyumba za kubanana, watu wengi mpaka hakuna pa kutema mate, udokozi, madawa na vijana wenye silaha mifukoni kila siku Mapolisi wapo doria, ni mitaa iliyomlea Maradona pale Villa Fiorito Jijini Buenos Aires, Argentina
Maradona anakua bila kupata muda mrefu wa kukaa na Baba yake Don Diego, anaamka saa 10 Alfajri na kurudi saa sita usiku, akirejea nyumbani alikuwa ni k**a mfu alie hai, mafukara walivyogundua kipaji chake walimpeleka Boca Juniors, ndio inaaminika ni klabu ya asili yao
Wakati Maradona anaelekea Ulaya, alifikia FC Barcelona ambapo hapo alicheza kwa miaka miwili chini ya Rais mbabe Nunez, hakupata upendo mkubwa sana na walipenda kumbagua na kumwita 'Sudaca' wakimaanisha mtu mweusi wa America Kusini
Aliwahi kuwaambia Wawakilishi wake kuwa hajisikii raha kucheza Barca mbele ya matajiri, wamtafutie timu yoyote yenye watu fukara, waliochoka maisha na hawana uhakika wa kula, anataka kuwa Nuru kwenye giza la maisha yao, alimaliza k**a haipo hiyo timu Ulaya basi arudi Boca Juniors
Ilikuwepo timu moja kutoka Kaskazini mwa Italia, ambapo watu wake maisha magumu, serikali inauchukia mji wa Naples watu waliishi bila uhakika wa kesho yao, ndipo ndani ya Mji huo kulikua na klabu ya SSC Napoli, ndipo hapa kuna ladha k**a za mitaa ya kwao Argentina
Ilimlazimu Mkurugenzi wa Napoli Antonio Juliano ambae pia alikulia maisha ya dhiki na shida Naples, kusafiri mpaka Barcelona kukamilisha dili la Maradona, kitu pekee alimwambia Diego ni kuwa hapa utakua kati ya miungu wanaoishi, tutakupa heshma zote,
Wakati Juliano anakubaliana dau la rekodi ya uhamisho duniani, Rais wa Barca alidai nyongeza ya pauni laki tano, ilibidi Juliano arudi Naples kuwatangazia Wananchi kuwa kiasi hicho kinahitajika na klabu haina pesa, Mashabiki na raia wa Naples wakaanza kuchangishana
Watoto, vijana na wazee chochote kilichopo mfukoni wanatoa ili Diego aje Naples, kuanzia Camorra mpaka mitaa ya Forcella, kila mtu licha umaskini na wengine inasemekana walikosa hata chakula ili kutoa kwa ajili ya usajili.
26/11/2025
✍Ilikua ukikutana na timu iliojaa wahuni ya Stoke City tena kwenye lile dimba lao la Britannia Stadium naongelea kipindi kile Stoke city kweli ya wanaume tena majira Yale ya baridi barani ulaya
✍Ilikua wakipata mpira wa kurusha kuna muhuni mmoja wa kuitwa Rory Delap huyu alikua bingwa wa kurusha mipira aliandaliwa hadi taulo kwajili ya kufuta mpira kabla ya kurusha
✍Moja ya mchezaji aliekua akichukiwa sana na Arsenal Wenger ni huyu kutokana hio style yake mpira unarushwa utafikiri kapiga kwa mguu
✍Crouch,Jonathan Walter,Ricardo Fuller & Kenwayne Jones walifaidika kwa kiasi kikubwa sana na mipira hiyo wakati huo stoke chini ya mwalimu Tony Pulis
22/11/2025
YANGA AFRIKA, PENYE NG'OMBE HAPAKOSI MMASAI
Diego Maradona katikati mwa uwanja pale Camp Nou, anamchukua Kiungo wa Deportivo kisha anamvesha kanzu Kiungo mwingine, anakusanya mabeki na kuweka kambani ila hashangilii bao
Moyoni mwake tu anajiona hafai kucheza kwenye Klabu ambayo yeye anahisi haina deni kwake, aliwakumbuka Wananchi wa Boca Juniors pale La Bombonera, alicheza kwakuwa alikuwa na deni kubwa kwao
Baada ya mchezo akamwambia Wakala wake, nitafutie timu Ulaya k**a Boca, k**a haipo naomba nirudi nyumbani Argentina nikacheze mbele ya watu wangu, wakala alipambana mpaka wakahamia Napoli, Wananchi wengine Kusini mwa Italia
Niliwahi kuandika kitu kuhusu timu zote za Wananchi duniani kote, niliwahi kusema kitu kuwa uvaapo jezi zao una deni kubwa kwao, hawana pesa ya kukulipa mshahara wako, hawana Maisha ya kukugharamia ila wanachoweza ni kusimama nyuma yako kwa Muda wote
Kumradhi kwa kukupeleka Argentina kisha Hispania na Italia, naomba nikulete makutano ya Twiga na Jangwani, shukrani zangu za dhati ni kwa Mpiga Picha wa Yanga Afrika, kanipa picha tatu za maana halisi ya timu ya Wananchi
Picha ya kwanza kutoka kmc complex pale mwenge , Mwananchi mmoja Kijana tu kavua jezi yake na kuipeperusha, huenda hana maisha k**a Rostam Aziz, miamala kam GSM wala fedha k**a za Dewji ila nikuhakikishie ana furaha kubwa kuliko wao, timu yake hii na damu yake hii
Picha ya pili ni Mama na Mwanae, sahau kuhusu foleni ya Dar Es Salaam, sahau huenda hana gari binafsi ila kipi kina nguvu kwake zaidi ya kumbeba Mwanae, kuvaa jezi ya Mwananchi na kujibana asisuke ili aende Taifa, nikuhakikishie ana furaha kuliko Nandy, Zuchu wala Ruby, timu yake hii
Picha ya mwisho ni Mzee wetu, katikati ya vijana kasimama yeye! Kuwarithisha kizazi cha wakina Sunday Manara, Salum Kabunda na sasa wakina pacome zouzou, katika furaha yake kubwa ya uhai ni kupata pia kuiona Yanga Afrika, ndio maana halisi ya Wananchi
Basi popote umwonapo ng'ombe hapakosi Mmasai, Wananchi ni ngome kongwe, hakuna alietawala vichwa vyao bali timu imetawala mioyo yao.. All the best huko zanzibar wananchi mwarabu afe leo